Hizi ni haki ambazo mtu anazipata mara tu anapozaliwa, na anaendelea kuwa nazo hadi kifo chake. Kwa maneno mengine, kitendo cha kuzaliwa ukiwa mwanadamu na si kiumbe kingine kinakupa moja kwa moja haki fulanifulani ambazo viumbe vingine havina
HAKI YA FIDIA KATIKA ARDHI
Ardhi ni Mali. Mali ni kitu au bidhaa yoyote yenye thamani. Kiwango cha thamani ya mali kinaweza kutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine, ama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine
SHERIA YA MADHARA: MAELEZO NA UFAFANUZI
Madhara ni matokeo hasi yanayompata mtu au kitu au mali kutokana na kitendo kilichofanywa na mtu mwingine au kilichotokea kutokana na mtu Fulani kushindwa kutimiza wajibu na kutokana na madhara hayo mtu aliyepata madhara anastahili kupata fidia
KOSA LA JINAI; MAELEZO NA UFAFANUZI
Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa sheria, ambapo mtu yeyote akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. Katika makosa ya jinai, mlalamikaji anakuwa ni Jamhuri, ikiwakilishwa na mwendesha mashitaka wa Serikali. Mtu binafisi aliyedhurika kwa tendo la kijinai siye anayeshitaki mahakamani.