Wajibu wa Msimamizi wa mirathi unajumuisha mambo yafuatayo:
Kufungua shauri la maombi ya usimamizi wa mirathi.
Kuainisha na kutambua mali na madeni yaliyoachwa na na marehemu.
Kulipa na kukusanya madeni yalioachwa na marehemu.
Kugawanya mali kwa warithi kulingana na sheria husika.
Kuwasilisha mahakamani hati inayoorodhesha mali na jinsi zilivyogawanywa katika mahakama ambapo shauri lilifunguliwa.