Wosia humpa muusia fursa ya kufanya mgao wa mali yake kwa kadri anavyotaka kabla ya kufariki.
Muusia anapata fursa ya kuamua ni nani msimamizi wa mirathi yake.
Wosia huepusha ugomvi wa wana familia.
Wosia ni chombo cha kuhakikisha kwamba urithi unakwenda kwa watu ambao marehemu aliwaridhia.