Wosia unaweza kuhifadhiwa ama kutunzwa mahali popote palipo na usalama na ulinzi ili kuepuka kughushiwa mfano;
Ofisi ya kabidhi wasii mkuu (RITA)
Kwenye vyombo vya kutoa msaada wa kisheria
Asasi za kidini kama kanisani au msikiti
Katika kampuni ya uwakili
Kwa mtu yeyote asiye mrithi katika wosia husika
Benki
Mahakamani, n.k.