Ndugu wa marehemu na wale wenye maslahi na mirathi ya marehemu, kwa mfano wale ambao wanatarajia kupata sehemu ya mirathi ya marehemu.
Mtu au watu wanaomdai marehemu, mtu huyu hufungua mirathi pale ambapo ndugu wa marehemu wameshindwa au hawataki kufungua mirathi. Kabidhi wasii mkuu. Muwakilishi wa kisheria au mtu aliyetajwa kama msimamizi wa mirathi kwenye wosia. Mtu yeyote ambaye mahakama kwa kuangalia vigezo mbalimbali vikiwamo undugu,maslahi ya muhusika katika mirathi hiyo, usalama wa mali za mirathi pamoja na uwezekano wa kusimamia vizuri, anaweza kuteuliwa na mahakama.