Kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, maelezo ya mkataba kwa maandishi yanayojumuisha:-
i. Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi
ii. Mahali alipoajiriwa
iii. Kazi yake
iv. Tarehe ya kuanza
v. Muundo na muda wa mkataba
vi. Kituo cha kazi
vii. Masaa ya kazi
viii. Ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu
(Sampuli ya Mkataba wa Ajira inapatikana katika tovuti ya www.sheriakiganjani.co.tz)