Kwa mujibu wa kifungu namba 16 cha sheria ya mtoto, mtoto anahitaji uangalizi maalumu endapo akiwa na sifa zifuatazo,
Mtoto yatima
Mtoto aliye na wazazi au walezi wasiotoa malezi bora
Mtoto aliye chini ya malezi ya wazazi au walezi ambao ni walevi au kwa sababu za kiuhalifu hawafai kuishi na mtoto huyo.
Mtoto ambaye anatendewa ukatili na wazazi au walezi wake
Mtoto ambaye anahusishwa na ukahaba au kuishi na walezi au wazazi wanaotuhumiwa kufanya ukahaba.