Wosia wa maandishi ni lazima uzingatie yafuatayo;
• Uandikwe kwa kalamu ya wino usiofutika kwa rahisi.
• Anayetoa wosia lazima awe na akili timamu.
• Wosia utaje tarehe ulipoandikwa.
• Wosia utaje kuwa anayetoa wosia anafanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.
• Wosia ushuhudiwe na mashahidi wawili wanaojua kusoma na kuandika. Shahidi mmoja awe wa ukoo na mwingine awe mtu baki kama muusia anajua kusoma na kuandika.
• Wosia hushuhudiwa na mashahidi wasiopungua wanne, mashahidi wawili wawe wa ukoo na wawili wawe watu baki kama muusia hajui kusoma na kuandika.
• Wanaotarajia kurithi hawaruhusiwi kushuhudia wosia huo.
• Wosia utiwe na saini ya muusia mbele ya mashahidi wake au kama hajui kusoma na kuandika aweke alama ya dole gumba la kulia.
• Wosia utiwe saini na mashahidi.