Muusia anaweza kumnyima mrithi sehemu ya urithi wake ikiwa mrithi;
• Amezini na mke wa muusia.
• Amejaribu kumuua, amemshambulia au amemdhuru vibaya muusia au mama mzazi wa mrithi.
• Bila sababu ya haki, hakumtunza muusia kutokana na njaa au ugonjwa.
• Ameharibu mali ya muusia. Uharibifu huo utahesabika katika kukadiria kiwango cha urithi atakachostahili kupata.