Sheria ya urithi na usimamizi wa mirathi imebainisha jinsi ambavyo madeni ya marehemu yanatakiwa kulipwa kwa kutoa kipaumbele kama ifuatavyo:
• Kwanza: Gharama za mazishi na matibabu.
• Pili: Gharama za ufunguzi na usimamizi wa shauri la mirathi zikiwemo gharama za kuendesha shauri hilo.
• Tatu: Malipo kwa huduma zilizotolewa kwa marehemu na mfanyakazi, kibarua au mtumishi wa nyumbani.
• Nne: Malipo kwa madeni mengine yaliyoachwa na marehemu.