Kwa mujibu wa kifungu namba 16 cha sheria ya mtoto, mtoto anahitaji uangalizi maalumu endapo akiwa na sifa zifuatazo, • Mtoto yatima • Mtoto aliye na wazazi au walezi wasiotoa malezi bora • Mtoto aliye chini ya malezi ya wazazi au walezi ambao ni walevi au kwa sababu za kiuhalifu hawafai kuishi na mtoto huyo. • Mtoto ambaye anatendewa ukatili na wazazi au walezi wake • Mtoto ambaye anahusishwa na ukahaba au kuishi na walezi au wazazi wanaotuhumiwa kufanya ukahaba.