Kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Kanuni ya Adhabu (The Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kutokujua sheria hakuwezi kumwondolea hatia mtuhumiwa. Utaratibu huu hutumika katika mataifa yote pale ambapo shauri linasikilizwa mahakamani au katika vyombo vingine vyenye hadhi ya kimahakama (Quasi-Judicial bodies). Utaratibu huu hutumika katika masuala yote ya kisheria, ikujumuisha pia mashauri ya madai. Kwa hiyo, ni wajibu wa kila mtu katika jamii kujua sheria, angalau zile zinazozunguka maisha yake ya kila siku, ili inapotokea kwamba ameingia katika mgogoro basi ujuzi alionao umsaidie. Hakuna anayehurumiwa kwa kigezo cha kutokujua Sheria.
Kwa bahati mbaya, kutokana na uhaba wa wanasheria katika nchi yetu, na ukweli kwamba wengi kati ya wanasheria wachache waliopo wanafanyia shughuli zao mijini, sehemu kubwa ya Watanzania ...
Soma Zaidi...Fahamu Kwa undani kuhusiana na Ajira, kazi na Hifadhi ya Jamii
Soma zaidi
Kupitia
ushirikiano wa taasisisi ya LANDESA na SheriaKiganjani, tumeweza kushirikiana
katika kuwezesha wasimamizi wa haki za ardhi kutoka kijiji cha Chamgoe-Mkuranga
kupata mafunzo zaidi na njia rahisi ya kujifunza sheria mbali mbali za ardhi
kupitia teknolojia ya Sheriakiganjani.
Binafsi nashukuru sana kwa uwepo wenu katika kusaidia watu kujua sheria kupitia huduma zenu za Sheria Kiganjani. Maoni yangu kwenu nawaomba sana muwe na moyo huo wa kusaidia watu katika nyanja nzima ya Sheria haswa pale mtu atakapohitaji msaada, maana lengo ni moja “kuwa na haki sawa na kuijenga nchi moja”;
“Shukrani
za kipekee kwa msaada wenu wa kisheria katika Shauri langu la Jinai, ambapo
kupitia njia ya simu mliweza kunielekeza taratibu za mahakamani na jinsi ya
kutoa ushahidi, hivyo kupelekea kushinda kesi hiyo ya Jinai iliyokuwa
inanikabili”;
“Kupitia huduma, ushauri na msaada wenu wa kisheria nimefanikiwa
kumpata mwanangu ambaye nilizuiwa kumuona, Mungu awabariki.”
“Nimeweza kushinda kesi yangu ya rufaa, kupitia msaada wa
kisheria kutoka ofisi zenu, asanteni sana.”
“Kwa njia
ya urahisi pasipo gharama kubwa nimepata nyaraka ya kiapo cha kuzaliwa kupitia
App ya Sheria Kiganjani, asante sana kwa kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania
walio kwenye uchumi mdogo”.
“Kupitia
msaada wa Sheria Kiganjani, nimeunganishwa na wakili wa karibu yangu ambaye
aliweza kunisaidia na kunisimamia katika tatizo langu la kisheria nililokuwa
nalo”.