Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Ipi ni mifano ya ushahidi wa upili?

+

Baaadhi ya mifano ya ushahidi wa upili ni pamoja na, nakala za hati halisi au maelezo yanayotolewa na mtu ambaye kashuhudia kitu kwa macho.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Ni nini hufuata baada ya maswali mtambuka?

+

Baada ya shahidi kuulizwa maswali mtambuka na upande wa pili basi mahakama pia hutoa nafasi kwa upande wa kwanza kumhoji baadhi ya maswali (maswali ya ukarabati) shahidi huyo ili kufuta maelezo yote babaifu yaliyotokea wakati wa maswali mtambuka.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, ni nini umuhimu wa uchunguzi mkuu wa shahidi?

+

Dhumuni kubwa la maswali mtambuka ni kupata maelezo yakinifu juu ya Ushahidi uliotolewa. Pia maswali haya ni maalumu kwa kuibua maelezo babaifu yaliyotolewa na shahidi husika

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, kila jambo la kusikika linakubalika mahakamani kama ushahidi?

+

Hapana. Ili jambo flani la kusikika likubalike kutumika mahakamani kama ushahidi ni lazima, kusiwe na ushahidi mwingine (bora zaidi) juu ya jambo hilo, shahidi aapishwe kabla ya kutoa ushahidi huo na lazima shahidi ahojiwe kwa kina na pande zote juu ya ushahidi anaoutoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, mahakama inaweza kupokea ushahidi wa kauli zilizopatikana usingizini?

+

Hapana. Kama mtuhumiwa atatoa kauli yoyote ile wakati amelala basi kauli hiyo haiwezi kubalika kutumika kama ushahidi mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, kauli isiyokamilika iliyotolewa na marehemu kama kauli ya mwisho inakubalika mahakamani?

+

Hapana. Kauli ya mwisho ya marehemu isipokamilika basi haiwezi kutumika kama ushahidi mahakamani kwani hakuna mtu anayeweza kujua kitu gani marehemu alilenga kusema.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, inawezekana kumkumbusha shahidi majibu ya maswali pale anaposhindwa?

+

Hapana. Mahakama inazuia upande wowote kuleta utetezi wowote juu ya majibu yaliyotolewa na shahidi wakati wa maswali mtambuka.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je, inawezekana mtu kutoa ushahidi juu ya utata wa hati flani?

+

Hapana. Sheria hairuhusu ushahidi unaotolewa kwa lengo la kutoa tafsiri ya maneno yaliyoandikwa kwa lugha inayoweza kusomeka na kueleweka kwa ufasaha.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, mahakama inapokea maungamo ya mdomo dhidi ya taarifa za hati flani?

+

Hapana. Ungamo linalotolewa na mdomo juu ya taarifa iliyopo katika hati basi taarifa ya hati itazingatiwa zaidi ya ungamo hilo

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, kuna aina ya maswali hayapaswi kuulizwa wakati wa maswali mtambuka (cross examination)?

+

Hapana. Wakati wa kumhoji shahidi maswali mtambuka basi upande wa pili unaruhusiwa kuulizwa swali lolote ambalo hulenga kupata ukweli, kujua yeye ni nani na ananafasi gani katika jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Nini maana ya ushahidi wa tabia?

+

Hii ni aiana ya ushahidi ambayo hutolewa juu ya tabia flani ya mtuhumia. Hapa inaweza kuwa tabia njema au mbaya.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Ni nini maana ya ushahidi wa moja kwa moja?

+

Hii ni aina nyingine ya ushahidi ambao humgusa shahidi moja kwa moja, mfano, kwa kugusa, kunusa, kuona au kusikia. Au ni ushahidi unaotolewa na shahidi ambaye amehusika katika tukio hilo moja kwa moja.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Ushahidi halisia ni upi?

+

Hii ni aina nyingine ya ushahidi ambayo huhusisha nyenzo fulani, katika aina hii ya ushahidi nyenzo husika hupelekwa mahakamani ili kukaguliwa na hakimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Nini maana ya maswali mwongozo?

+

Hii ni aina ya maswali ambayo huonyesha dhahiri kitu anachokusudia kupata kutoka kwa shahidi husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Ni nini maana ya ushahidi wa mdomo?

+

Hii ni aina ya ushahidi amabyo hutolewa kwa mdomo na shahidi mwenyewe wakati wa mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Ni nini maana ya ushahidi wa nje?

+

Hii ni aina ya ushahidi ambao hutokea nje ya ushahidi mwingine (hasa ushahidi wa maandishi). Mfano mzuri wa ushahidi wa nje ni maelezo nje ya mkataba anayopatiwa mtu wakati wa kupewa mkataba, maelezo haya yanaweza kutumika kama ushahidi licha ya kutokuwepo katika mkataba husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je upi ni ushahidi wa kimahakama?

+

Hii ni aina ya ushahidi ambao hutolewa mahakamani ili kuthibitisha au kutodhibitisha jambo lililopo katika shauri. Hii hujumuisha kiapo kukiri mbele ya hakimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Ushahidi wa kusikia ni nini?

+

Huu ni aina ya ushahidi ambao hutolewa na Shahidi ambaye hakuhusika moja kwa moja katika tukio ila amesikia kuhusiana na tukio hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Ni nini maana ya ushahidi wa kimazingira?

+

Huu ni ushahidi ambao haugusi tukio moja kwa moja lakini unaelezea mazingira yanayoendana na shauri husika. Maranyingi ushahidi huu humpa uwanja Hakimu kuunganisha matukio ili kupata hitimisho.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Ni, maana ya ushahidi wa maandishi?

+

Huu ni ushahidi unaotolewa na upande moja wapo wa shauri katika hali ya maandishi (hati) ili ukaguliwe na Hakimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Nani si shahidi mwenye uwezo wa kulazimika mahakamani?

+

Huyu ni aina ya shahidi ambaye amekidhi vigezo vya kuitwa na kutoa Ushahidi mahakamani lakini katika aina flani ya shauri Ushahidi wake si wa lazima mahakamani. Aina hii ya shaidi hawezi kuchukuliwa hatua yoyote iwapo atakataa kutoa Ushahidi mahakamani. Mfano mzuri wa aina hii ya shahidi ni mke na mume.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Nani ni shahidi mwenye uwezo wa kulazimika mahakamani?

+

Huyu ni aina ya shahidi ambaye amekidhi vigezo vya kuitwa na kutoa Ushahidi mbele ya mahakama bila kipingamizi chochote. Mtu wa aina hii kama atashindwa kutoa Ushahidi mahakamani basi mahakama ina uwezo wa kumtia kizuizini kwa kosa hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Shahidi wa macho ni nani?

+

Huyu ni mmoja kati ya mashahidi wanaotumika mahakamani. Shahidi huyu jadi awe amaehakikisha tukio husika kwa macho yake mwenyewe.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Yupi ni shahidi wa kitaalamu?

+

Huyu siyo shahidi wa jambo katika shauri, bali ni mtaalamu anayetoa ushauri na maelezo ya kitaalamu juu ya hitimisho linalopaswa kutolewa juu ya shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Nini kinazingatiwa katika ushahidi unaokubalika?

+

Ili ushahidi ukubalike kutumika mahakamani lazima uzingatie mambo makuu yafuatayo; a) Lazima uendane na suala lililopo katika shauri b) Lazima ushahidi huo uwe ukikubalika kisheria c) Lazima ushahidi huo utolewe na mtu anayekubalika (mwenye ruksa) ya kutoa ushahidi mahakamani. d) Lazima upatikane kwa njia halali.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Mambo gani huthibitisha muunganiko wa matukio?

+

Ili ushahidi utumike katika kigezo cha muunganiko wa matukio lazima kuwe na mfuatano wa matukio yanayolenga hatima moja. Hapa hujumuisha, wakati wa kutendeka kwa jambo, sehemu ya tukio, mwendelezo wa tukio husika na malengo mahususi ya matukio. Kama lengo la matukio ni moja basi hata kama matukio hayo hayakufanyika nyakati sawa au eneo sawa bado huthibitisha muunganiko wa matukio.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Nini hufanyika kama shahidi ni mtoto mahakamani?

+

Ili ushahidi wa mtoto ukubalike lazima mahakama ijilidhishe kwamba mtoto huyo anauwezo wa kukumbuka matukio ya nyuma, anaweza kuongea vizuri pia anauwezo wa kuelewa baadhi ya mambo.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Nini hutokea kama shahidi atabadili upande? (Shahidi wa uadui).

+

Kama ikitokea shahidi akabadili upande wakati wa kutoa ushahidi na kwenda kinyume na upande uliomuita kutoa ushahidi au kuamua kusema uongo dhidi ya upande wake basi mahakama itatoa nafasi kwa upande husika kumhoji baadhi ya maswali shahidi huyo ili kuthibitisha kuwa kinachoongelewa hapo si cha kweli.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Yupi ni shahidi upande wa mshtakiwa?

+

Kama ilivyo upande wa mashtaka vilevile upande wa mshatakiwa, kuna nafasi ya kuleta shahidi ambaye atatoa ushahidi ili kukanusha tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa katika shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Nini hutokea kama mahakama imekataa ushahidi kimakosa?

+

Kama itagundulika kuwa mahakama ilikataa ushahidi flani kimakosa basi italazimika shauri hilo kurudiwa. Ili shauri hilo lirudiwe lazima kwanza idhihirike kwamba kutokuwepo kwa ushahidi huo kumepelekea maamuzi hayo yaliyotokea na kama ushahidi huo hauwezi kuathiri maamuzi ya mwanzo basi shauri hilo halitarudiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Nini hutokea kama mahakama imepokea ushahidi kimakosa?

+

Kama itagundulika kuwa mahakama imepokea na kutumia ushahidi flani kimakosa basi italazimika shauri hilo kurudiwa. Ili shauri hilo lirudiwe lazima kwanza idhihirike kwamba kuwepo kwa ushahidi huo kumepelekea maamuzi hayo yaliyotokea na kama ushahidi huo hauwezi kuathiri maamuzi ya mwanzo basi shauri hilo halitarudiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Nini hufanyika mahakamani kama hati ina utata uliofichika?

+

Kama itathibitika kuwa hati ina maneno yenye utata uliojificha ndani yake basi mahakama itaruhusu ushahidi kutolewa ili kukosoa utata uliojificha katika hati husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Je, nini hutokea kama shahidi wa mwanzo hawezi tena kupatikana katika mwendeleo wa shauri?

+

Kama itathibitika kuwa shashidi wa mwanzo hawezi tena kupatikana basi mahakama itatumia ushahidi wake wa mwanzo (uliotolewa mbele ya mahakama au mbele ya hakimu au mtu yeyote mwenye dhamana hiyo).

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Kitu gani huthibitisha utekelezaji wa hati flani?

+

Kama kuna hati inadaiwa kusainiwa au kuwa imeandikwa na mtu flani, basi kulithibitisha hilo mahakama itaomba mtu huyo kuonyesha mwandiko wake (akaguliwe mwandiko) ili kung’amua uhusika wake katika hati hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Nini hutokea kama mtu aliyetoa ushahidi awali hawezi kupatikana tena?

+

Kama mtu wa mwanzo aliyetoa ushahidi flani hawezi kupatikana tena basi suala hilo hutoa upekee katika sheria ya ushahidi wa kusikia. Kwa maana hiyo ushahidi huo unaweza kutumika katika mahakama pasi na kuzingatia mchakato maalumu wa kukubali ushahidi wa kusikia.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, mahakama inapokea kauli zilizopatikana kwa njia ya udanganyifu?

+

Kama mtuhumiwa atashawishiwa kwa namna yoyote ile bila kutumia nguvu na akatoa kauli inayoweza kusaidia utetezi katika shauri flani basi kauli hiyo itapokelewa kama ushahidi pasi na kujali njia gani imepatikana.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, kauli iliyopatikana kwa ahadi ya usiri inapokelewa mahakamani?

+

Kama mtuhumiwa atatoa kauli flani baada ya kuahidi kutunziwa siri basi kauli hiyo ikipelekwa mahakamani itapokelewa kama ushahidi kwa kuwa haikupatikana kwa nguvu.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je, nini kifanyike na upande uliosalitiwa na Shahidi mahakamani?

+

Kama shahidi amegeuka upande wako basi huna budi kutoa mashtaka juu yake kwa kuonyesha uhalisia wake mbele ya mahakama ili kile anachokiongea kisiaminike tena na mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Je, nini hutokea kama shahidi amegoma kutoa ushahidi mahakamani?

+

Kama Shahidi ataitwa na mahakama kwa lengo la kutoa ushahidi ila akakataa kutoa ushahidi au kuapishwa kutoa ushahidi mbele ya mahakama basi italazimu kesi kusimamishwa kwa muda usiozidi siku nane na katika wakati wote huo Shahidi huyo anapaswa kuwekwa kizuizini mpaka pale atakapoamua vinginevyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je, nini cha kuzingatia katika kumshtaki shahidi wa uadui katika mahakama?

+

Kama shashidi atabadili upande basi, upande ule hauna budi kuthibitisha kuwa shahidi huyo alihongwa na upande wa pili ili atoe ushahidi dhidi ya upande wa kwanza.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je, nini hutokea kama upande mmoja umeshindwa kuzalisha hati kama ilivyoombwa na upande wa pili?

+

Kama upande moja wapo umeshindwa kupata hati iliyoombwa na upande mwingine basi, upande huo pia hautaweza kuitumia hati hiyo kama ushahidi wakati shauri linaendelea.

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je, nini hutokea kama mtuhumiwa atakataa maelezo yake ya mwanzo

+

Kama, mtuhumiwa amekiri juu ya jambo flani kabla na baadae akakana kuwa hakukiri jambo hilo basi mahakama italazimika kuanzisha shauri mpya juu ya ile ya mwanzo ili kupata mwafaka wa jambo hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je, nini anapaswa kufanya mtu aliyeita shahidi alafu akageukwa na shahidi huyo?

+

Kitu cha msingi cha kufanya kama shahidi amehama upande basi upande wa mwanzo unapaswa kudharau au kupuuza maelezo yatakayotolewa na shahidi huyo mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Je, ni kitu gani huzingatiwa ili kupokea kauli ya marehemu kama ushahidi mahakamani?

+

Kitu kikubwa na muhimu kinachozingatiwa katika kauli ya mwisho ya marehemu ni taarifa juu ya chanzo na sababu za kifo chake. Kama kauli ya mwisho ya marehemu hailengi kutoa mwangaza juu ya chanzo cha kifo chake basi kauli hiyo haifai kuwa ushaidi katika shauri hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Kuna umhimu gani wa kukubali kutumia ushahidi wa kauli ya mwisho ya marehemu?

+

Kwa mujibu wa kanuni za sheria kama kauli ya mwisho ya marehemu ndiyo ushahidi pekee uliopo katika kuamua shauri flani basi kutokutumia ushahidi huo ni kitendo cha ukosefu wa haki.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Je, nani anapaswa kupokea ungamo kutoka kwa mtuhumiwa?

+

Kwa mujibu wa sharia ya Ushahidi, ungamo mara nyingi hufanyika mbele ya afisa wa polisi kama ni kabla ya shauri kusikilizwa au mbele ya hakimu husika kama shauri litakuwa ikisikilizwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Nini hutokea kama shahidi kaungama kwa lazima?

+

Kwa mujibu wa sheria ungamo lolote linalotokea kwa shinikizo, kulazimishwa au kuahidiwa kitu basi ungamo hilo ni batili na halifai kutumika mahakamani.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Nini cha kuzingatia katika kutumia ushahidi wa maneno ya mwisho ya marehemu?

+

Kwanza lazima mtoa ushududa huo awe kweli kafariki, tofauti na hapo ushahidi huo haukubaliki, maelezo yanayotolewa yanapaswa kuwa na mahusiano na tukio husika katika shauri, chanzo cha kifo kinatakiwa kuwa moja ya mambo yanayotatuliwa katika shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je, ni nini umuhimu wa uchunguzi mkuu wa shahidi?

+

Lengo mahususi la uchunguzi wa shahidi ni kutafuta ushuhuda madhubuti kuendana na tendo au matendo yanayolengwa katika shauri husika, hivyo majibu ya maswali atakayoulizwa shahidi hutoa majibu kwa maswali yaliyoibuliwa katika shauri.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Je, tamko la mwisho la marehemu lipo katika kundi gani la ushahidi?

+

Licha ya kuwa maneno ya mwisho ya marehemu ni ya kusikia lakini maneno hayo hutumika moja kwa moja kama ushahidi mahakamani tofauti na ushshidi mwingine wa kusikia ambao hauruhusiwi kutumika mahakamani labda tu kama vigezo kadhaa vimezingatiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Je, mahakama inapokeaje kauli za mtuhumiwa zilizopatikana akiwa chini ya ulinzi wa polisi?

+

Mahakama inakubaliana na maelezo/kauli zilizotolewa na mtuhumiwa pindi awapo chini ya ulinzi wa polisi bila kujali kama kauli hizo ni maungamo au la. Kitu cha msingi hapa ni kwamba lazima kauli hizo ziendane na matendo au vitendo vinavyozungumziwa kwenye shauri.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Je, nani hupanga wakati wa kuuliza na kujibiwa maswali mtambuka?

+

Mahakama pekee ndiyo yenye dhamana ya kuruhusu shahidi kuulizwa na maswali na pia mahakama ndiyo inayoamuru shahidi husika kujibu maswali aliyoulizwa na upande wa pili.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Nini hufanya ushahidi wa kusikia kutokubalika mahakamani?

+

Mara nyingi ushahidi wa kusikia haukubaliki mahakamani kama, kuna ushahidi mwingine (bora zaidi) juu ya jambo hilo, shahidi hakuapishwa kabla ya kutoa ushahidi huo na shahidi hakupitia mtihani tambuka (hakuhojiwa kwa kina) na pande zote juu ya ushahidi anaoutoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Je, ni kwanamna gani tabia ya mtu hutumika kama ushahidi?

+

Mara nyingi ushahidi wa tabia hutolewa pale mtuhumiwa anapojaribu kuhadaa mahakama kwa kuonyesha upande mzuri wa tabia zake, hivyo mahakama hulazimika kutafuta ushahidi wa kuonyesha uhalisia wa tabia ya mtuhumiwa. Mfano mzuri wa ushahidi wa tabia ni kama mtuhumiwa amewai kukumbana na aina hiyohiyo ya shauri.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Je, ni kwa namna gani mawazo ya wataalamu hutumika kama ushahidi?

+

Mawazo ya wataalamu yanaweza kutumika kama ushahidi katika maswala yanayohusiana na sheria za nje, sayansi, ugunduzi wa miandiko na ugunduzi wa alama za vidole.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, nini maana ya mtihani/maswali mtambuka (cross examination)?

+

Mtihani mtambuka au maswali mtambuka ni aina ya maswali anayoulizwa shahidi na upande wa pili wa shauri.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Je, ungamo (kukiri) lililofanyika nje ya mahakama hupokelewaje mahakamani?

+

Mtu yeyote akikiri kufanya jambo flani mbele ya mashahidi wengine basi kukiri kwake hupokelewa mahakamani kama ushahidi usio wa kimahakama japo unaweza kutumika kama ushahidi wa mahakama katika kuupima uhalisia wa ushahidi huo.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je, shahidi anaweza kutoa ushahidi akirejelea kauli za watu mbalimbali?

+

Ndiyo. Inaruhusiwa shahidi kurejelea kauli za watu mbalimbali katika jamii juu ya jambo analolitolea ushuhuda. Kama kauli flani imesemwa na zaidi ya mtu mmoja basi itapokelewa kama ushahidi dhidi ya jambo flani.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Je, inawezekana ushahidi uliopokelewa wakati mtuhumiwa amelewa kutumika mahakamani?

+

Ndiyo. Kama afisa wa polisi atatumia kilevi ili kumfanya mtuhumiwa atamke kauli muhimu basi kauli hizo zinaweza kutumika kama ushahidi mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Je, mahakama inaweza kuingilia suala la hati flani kuletwa kama ushahidi?

+

Ndiyo. Kama hati flani itatakiwa kutumika kama ushahidi na upande husika umeshindwa kuzalisha hati hiyo basi mahakama ina uwezo wa kuamuru upande husika kuzalisha hati hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je, inawezekana mtoto kutoa ushahidi wa kujitegemea?

+

Ndiyo. Kama mahakama itajiridhisha kuwa mtoto huyu anachokiongea ni kweli tupu basi ushahidi wa mtoto utakubalika bila kujali maelezo ya usaidizi.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, mtu anaweza kuhukumiwa kwa ushahidi wa kitabia?

+

Ndiyo. Kama mahakama itajiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa juu ya tabia ya mtuhumiwa ni moja ya chanzo cha maovu aliyotenda basi ushahidi huo utatumika katika kutoa hukumu juu ya mtuhumiwa huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, mahakama inaweza kukataa ushahidi uliotolewa na mtaalamu?

+

Ndiyo. Kama mahakama itajiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na mtaalamu hauna mashiko basi haitautumia ushahidi huo badala yake ushahidi mwingine wa msingi utatumika katika shauri hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je, mahakama inapokea kauli zilizotendwa na mtuhumiwa kabla ya kuonywa kuwa zitamuathiri baadaye?

+

Ndiyo. Kama mtuhumiwa atatoa kauli au maelezo flani kabla ya kuonywa yanaweza kumtia hatiani basi kujua kwake hakuzuii kauli ya mwanzo kutumika dhidi yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, kauli ilyopatikana kwa kusikilizwa kwa bahati inakubalika mahakamani?

+

Ndiyo. Kama mtuhumiwa atatoa kauli bila kujua kama kuna mtu anamsikiliza basi kauli hiyo inaweza kutumika kama ushahidi dhidi yake mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je, inawezekana upande mmoja wa shauri kuomba upande wa pili wazalishe hati flani kama ushahidi?

+

Ndiyo. Kama upande mmoja wa shauri utaamua kuwa kuna baadhi ya hati iko mikononi mwa upande pinzani basi itaomba upande husika kuleta hati hiyo mbele ya mahakama ili itumike kama ushahidi.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Je, inawezekana shahidi katika shauri la madai kugeuka upande?

+

Ndiyo. Katika shauri lolote (Jinai au Madai) Shaihidi anaweza kubadili upande kwa sababu zake binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, inawezekana kauli ya mwisho ya marehemu ikawa kwa njia ya mazungumzo?

+

Ndiyo. Kauli ya mwisho ya marehemu inaweza ikawa kwa njia ya mazungumzo baina yake na mtu wa mwisho kuwa nae (shahidi), ambapo mazungumzo yao yanapaswa kutolewa kama yalivyo. Kama kulikuwa na majibizano baina yao basi majibizano hayo yanatakiwa yatolewe kama ilvyotokea ili kupima uzito wa kauli zao kabla ya kutumia kama ushahidi.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je, inawezekana mahakama kumkataa mtu flani kutumika kama shahidi?

+

Ndiyo. Kila upande wa shauri unapewa ruksa ya kudhihirisha uhalisia wa mashahidi walioitwa kwenye shauri. Kama mahakama itajiridhisha kuwa mtu flani hafai kuwa shahidi wa shauri husika basi mtu huyo atazuiliwa kusimama kama shahidi mahakamani.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, ni sahihi kwa wazee wa mahakama kumuuliza maswali shahidi?

+

Ndiyo. Kwa ruhusa kutoka kwa hakimu basi wazee wa mahakama wanauwezo wa kumhoji shahidi juu ya ushahidi anao utoa mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je, mahakama inaweza kuzuia baadhi ya maswali kuulizwa kwa shahidi?

+

Ndiyo. Mahakama ina haki ya kuzuia baadhi ya maswali yasiulizwe kwa shahidi kama tu itajiridhisha kuwa maswali hayo yatamdhalilisha shahidi au kuleta tafrani katika mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, ushahidi wa kuamua fidia unakubalika mahakamani?

+

Ndiyo. Mahakama inapokea ushahidi unaoonyesha fidia gani inapaswa kutolewa kwa upande flani. Ushahidi huu hupokelewa pasi na kujali kama umeendana na tendo au matendo yaliyoelezwa katika shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, mahakama inauwezo wa kuita shahidi wake mwenyewe?

+

Ndiyo. Mahakama inauwezo wa kumuita mtu yeyote kama shahidi kwenye shauri flani kama itajiridhisha kuwa haki itapatikana kwa uwepo wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je, inawezekana shahidi kuulizwa maswali na upande wake mwenyewe?

+

Ndiyo. Mahakama inaweza kutoa nafasi kwa shahidi kuulizwa baadhi ya maswali na upande wake kwa lengo la kuuweka ukweli hadharani.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, maneno ya mwisho ya marehemu yanaweza kutumika kama ushahidi mahakamani?

+

Ndiyo. Maneno ya mwisho ya marehemu kama maneno hayo kwa namna moja ama nyingine yanahusiana na kifo cha marehemu basi maneno hayo yatakubalika kama ushahidi.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, shahidi anaruhusiwa kusoma au kujikumbusha kitu wakati wa maswali mtambuka?

+

Ndiyo. Shahidi anapewa wasaa wakupitia hati alizoandaa ili kujibu maswali ya mtambuka kwa ushahihi na ufasaha mkubwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je, shahidi anaweza kutoa ushahidi unaohusisha hati yenye kumtia hatiani?

+

Ndiyo. Shahidi anaruhusiwa kutoa ushahidi wa hati ambayo inaweza kumtia hatiani japo hapa sheria humlinda kama tu hatakuwa mhusika wa shauri hilo. Pia hati hiyo atapaswa kuitoa kwa njia ya maandishi.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, kuna maswali hayaruhusiwi kuulizwa wakati wa maswali ya ukarabati (re- examination)?

+

Ndiyo. Wakati mahojiano ya kurekebisha maswali mtambuka basi hairuhusiwi shahidi kuulizwa maswali ya mwongozo, labda kama upande wa pili utaruhusu kufanya hivo au kwa ruhusa maalumu ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, inawezekana ushahidi juu ya shahidi aliyetoa ungamo?

+

Ndiyo. Wakati mwingine ushahidi unahitajika ili kuthibitisha kama kauli ya ungamo iliyotolewa na shahidi ni ya kweli.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, ni upi ushahidi usiokubalika?

+

Ni ushahidi ambao ambao hutolewa bila kuzingatia mambo ya msingi pamoja na kutoendana na suala lililopo katika shauri, kupatikana kwa njia isiyo halali au uwe umetolewa na mtu asiyefaa kutoa ushahidi mahakamani.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Je, ushahidi wa mtu mmoja unakubalika katika kitendo cha njama?

+

Njama ni kitendo cha watu wawili au zaidi kushiriki katika kutenda jambo flani. Katika sheria ya ushahidi ikithibitika kwamba watu wamekula njama basi kauli yoyote itakayotendwa na mmoja wapo wa watu hao huwahusisha wote katika kundi. Ili kujua kama watu flani wamekula njama lazima katika namana zote ithibitike kuwa watu hao wametenda tendo kwa umoja wao na kwa lengo moja.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je, ni kwa nini ushahidi wa kusikia haukubaliki mahakamani?

+

Sababu moja wapo ya kutokubalika kwa ushshidi wa kusikia ni kwamba ushahidi huu hautoi nafasi ya maswali mtambuka kwa shahidi husika hivyo ushahidi huu humyima haki mtuhumiwa ya kupata ukweli juu ya ushahidi huo.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je, ushahidi unaotolewa na shahidi wa uadui ni muhimu katika mahakama?

+

Shahidi kubadili upande haidhihirishi kwa kila neno alilotoa ni la uongo badala yake Hakimu atapata wasaa wa kuchambua baadhi ya maelezo yatakayo saidia mahakama. Ushahidi wa mtu huyu unaweza kutumika kama itathibitika kuwa alihongwa na upande wa kwanza ili atoe ushahidi au amejua ukweli kuwa upande aliopo siyo sahihi.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Yupi ni shahidi mtoto?

+

Shahidi mtoto ni kitendo cha kuhitaji maelezo flani ya utetezi kutoka kwa mtoto mdogo mwenye uwezo wa kuona, kuongea na kusikia.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Shahidi ni nani?

+

Shahidi ni mtu yeyote aliyeruhusiwa na mahakama kutoa ushuhuda juu ya tukio lililotokea, amabalo linamahusiano ya shauri linaloendelea.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Yupi ni shahidi upande wa mashtaka?

+

Shahidi upande wa mashtaka ni shahidi ambaye maranyingi huhusika katika kesi za jinai. Shahidi huyu maranyingi huwa mwanasheria upande wa serikali anayesimamia shauri dhidi ya uhalifu. Kazi kubwa ya shahidi huyu ni kuhakikisha anatoa ushahidi kwa lengo la kumtia hatiani mtuhumiwa wa shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je, inawezekana shahidi kufunguliwa mashtaka juu ya ushahidi alioutoa mahakamani?

+

Sheria inamlinda shahidi kwa ushahidi atakaoutoa mahakamani hata kama maelezo yake yanamfanya kuonekana mkosefu mbele ya sheria. Kitu peke cha kumtia hatiani shahidi ni kama atatoa ushahidi wa uongo mbele ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Je, ni umri gani mtu anaruhusiwa kutoa ushahidi mahakamani?

+

Sheria inaruhusu mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye anajitambua kutoa ushahidi mahakamani, ambapo kwa mtoto mdogo basi kitafanyika kipimo maalumu ili kujua kama mtoto huyo ana uwezo wa kujieleza kabla ya kusikiliza ushahidi wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Je, upande upi wa shauri unajukumu la kuthibitisha ukweli wa ungamo lililotendeka?

+

Uapande wa mwendesha mashtaka ndio hupewa jukumu la kuthibitisha ukweli juu ya ungamo lilofanywa na mtuhumiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Nini maana ya uchunguzi mkuu wa shahidi (examination in chief)?

+

Uchunguzi mkuu wa shahidi ni uchunguzi unaofanywa na upande mmoja wa shauri kwa kumuuliza maswali shahidi wake mwenyewe katika mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Nini maana ya ungamo katika sheria ya Ushahidi?

+

Ungamo (confession) ni maelezo yanayotolewa na mtuhumiwa ili kukiri shauri au baadhi ya mambo yanayomkabili katika shauri husika. Maelezo haya yanaweza kutolewa mapema shauri linavyosikilizwa au wakati shauri likiendelea.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Nini maana ya ushahidi?

+

Ushahidi ni kitu au maelezo yanayotolewa hususani katika vyombo vya sheria kwa mfano mahakama, ili kuthibitisha kuona au kusikia jambo fulani lililotokea.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Ushahidi wa awali ni nini?

+

Ushahidi wa awali ni aina ya ushahidi ambao hutolewa kwa lengo la kuthibitisha kuwa jambo fulani lilitendeka zaidi ya kuthibitisha kuwa jambo hilo ni la kweli.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Zipi sababu za kutumia ushahidi wa upili wa hati mahakamani?

+

Ushahidi wa upili wa hati utakubalika tu iwapo, hati ya msingi imepotea/kuharibika, hati ya msingi haiwezi kuhamishika, hati ya msingi haijazalishwa au hati ya msingi ni hati ya umma.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Je, ni nani hutoa ushahidi?

+

Ushahidi wote hutolewa na Shahidi/Mashaidi, ambaye anaweza kuwa mtu yeyote, askari mpelelezi au mtuhumiwa mwenyewe wa shauri husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Je, ushahidi hutolewa mahakamani kwa kufuata misingi ya sheria gani?

+

Ushahidi wote unaotolewa mahakamani lazima ufate misingi ya Sheria ya Ushahidi ya mwaka 2022.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Nini maana ya ushahidi wa msingi?

+

Ushashidi wa msingi ni ushahidi ambao unaamuriwa na sheria kutolewa kwanza mahakamani kabla ya aina yeyote ile ya ushahidi mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Nini maana ya ushahidi wa upili?

+

Ushashidi wa upili ni ushahidi ambao unaamuriwa na sheria kutolewa mahakamani iwapo tu kutakosekana ushahidi wa msingi. Ushahidi huu unahitaji maelezo ya kina ili kuweza kutumika mahakamani. 

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand