Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Mtoto ana haki ya mawasiliano na wazazi, ndugu na rafiki zake wakati akiwa kwenye makazi yaliyothibitishwa au shule ya maadilisho. Je, ni kwa mazingira gani anaweza asipewe haki hiyo licha ya kwamba kuna uwezekano wa kupata mawasiliano hayo?

+

anaweza kunyimwa haki hiyo kama ikionekana kwamba si kwa maslahi bora ya mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, mtoto ana haki ya kupumzika na kuwa huru kwa kiwango atakacho hata kama uwezo wa mzazi wake hauendani na uhuru huo?

+

Hapana, haki ya mtoto kupumzika na kuwa huru inazingatia uwezo na mwongozo wa mzazi wake (rejea kifungu namba 9 (2) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, mtoto anapolelewa na mlezi wa kambo, analazimika kuabudu kulingana na dini ya mlezi wake wa kambo?

+

Hapana, kwa mujibu wa kifungu namba 53 (4) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019 si lazima mtoto aliye chini ya malezi ya kambo kuabudu kulingana na dini ya mlezi wake wa kambo. Mtoto anaendelea kuwa na haki ya kuabudu kulingana na dini yake ya kuzaliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, mtoto anaweza kuhukumiwa kifungo kama watu wazima?

+

Hapana, Mtoto hawezi kuhukumiwa kifungo kama watu wazima (kifungu namba 119 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, mzazi au mlezi anaweza kutomruhusu Afisa Ustawi wa Jamii kumtembelea mtoto kuona maendeleo yake?

+

Hapana, mzazi au mlezi anatakiwa kumruhusu Afisa Ustawi wa Jamii kumtembelea mtoto (kifungu namba 21 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, mzazi au mlezi wa mtoto ana haki ya kumchukua mtoto wake kutoka katika shule iliyothibitishwa bila amri ya Mahakama na kabla ya muda wa kukaa kizuizini kuisha?

+

Hapana, mzazi au mlezi hana haki hiyo. Mtoto anaweza kutolewa kwenye shule iliyothibitishwa kwa amri ya Mahakama au baada ya muda wa kukaa kizuizini kuisha.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, unadhani ni halali kisheria mtu kutumia wadhifa wake kumshawishi mtoto kufanya ngono ili ampatie huduma yoyote?

+

Hapana, ni kosa la jinai chini ya kifungu namba 138B (d) cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kwa mtu yeyote kutumia cheo au wadhifa wake kumshawishi mtoto kufanya tendo la ngono, na adhabu yake ni si chini ya miaka 15 na isiyozidi miaka 30 jela.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Kwanini mtoto anapelekwa shule ya maadilisho (shule iliyothibitishwa) baada ya kukutwa na hatia yoyote?

+

Ili aweze kujifunza tabia na maadili mema na hatimaye kuachana na tabia ya kutenda maovu.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Mtu yeyote anayo haki ya kuoa au kuolewa. Licha ya kuwepo kwa haki hiyo, sheria imeweka katazo ya umri wa chini wa mtu kuoa au kuolewa. Je, ni umri gani kisheria ambao mtoto anaweza ingia kwenye ndoa kwa jinsia zote mbili?

+

Jinsia ya kiume umri wa chini ni miaka 18 Jinsia ya kike umri wa chini ni miaka 15 endapo kutakuwa na ruhusa ya mzazi, mlezi au mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Kwa mujibu wa Sheria, hairuhusiwi kumwajiri au kumshughulisha mtoto katika kazi yoyote ambayo ni hatarishi. Unaelewa nini kuhusu kazi hatarishi kwa mtoto na ipi ni mifano yake?

+

Kazi hatarishi kwa mtoto ni ile ambayo inaweza kuhatarisha afya, usalama au maadili ya mtoto. Kazi hizo ni kama vile ubaharia, ubebaji wa mizigo mizito, uchimbaji madini au upasuaji mawe, kazi za baa, hoteli na sehemu za starehe n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je, ikiwa mtoto atafanya kosa ambalo adhabu yake ni hukumu ya kunyongwa mpaka kufa. Je, mtoto anaweza hukumiwa kunyongwa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 26(2) cha sheria ya makosa ya jinai, mtoto hawezi kuhukumiwa kunyongwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, kisheria nani anatakiwa kuishi na mtoto mwenye chini ya umri wa miaka saba kati ya baba au mama hasa pale wanapokuwa wametengana au kutalakiana?

+

Mama ndiye anapaswa kuishi na mtoto mwenye umri chini ya miaka saba(7).

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Kwa mujibu wa kifungu namba 103 (2) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019, Mahakama ya Watoto inatakiwa kusikiliza kesi ya mtoto na kutoa maamuzi siku hiyo hiyo isipokuwa kama ni kosa la mauaji. Nini umuhimu wa jambo hili?

+

Mtoto anapata haki yake haraka na kama ikigundulika hana hatia anaendelea na masomo bila usumbufu wowote. Pia, inamfanya mtoto asiendelee kushikiliwa mahabusu kwa muda mrefu.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Mlezi wa kambo ni mtu ambaye si mzazi wa mtoto ila ana nia na uwezo wa kumlea mtoto na kumpatia matunzo. Je, ni mtu mwenye umri gani anaweza kuwa mlezi wa kambo wa mtoto?

+

Mtu mwenye umri unaozidi miaka ishirini na moja (kifungu namba 52 (1) cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 2019)

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Ikiwa wazazi wa mtoto wametengana au kutalakiana. Amri ya mahakama ya kumtunza mtoto itatolewa ambapo mtoto atakwenda kuishi na moja ya mzazi. Je, ni haki gani anayoipata mzazi asiye na haki na uangalizi wa mtoto huyo?

+

Mzazi asiye na haki ya kumlea mtoto ana haki ya kumtembelea na kumuona mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je, mtoto ana haki ya kupewa jina?

+

Ndio, hii ni haki ambayo mtoto anastahili kuipata. Mtoto anastahili kupewa jina kwa mujibu wa kifungu namba 6(1) cha sheria ya mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, mtoto ana haki ya kupata dhamana baada ya kukamatwa kwa kosa lolote?

+

Ndiyo, mtoto ana haki ya kupata dhamana isipokuwa kama shitaka ni la mauaji, ni lazima kwa maslahi ya mtoto kumwondoa asikae pamoja na mtu asiyefaa au kuachiliwa kwake kunaweza kuathiri utoaji wa haki.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je, ni haki ya mtoto kupewa jina au inategemeana na maamuzi au utashi wa wazazi wake?

+

Ni haki ya mtoto kupata jina na hii haitegemei utashi wa wazazi (kifungu namba 6 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Ni vema kuwa na taifa lenye vijana wenye maadili mema ili tuweze kuwa na taifa lenye vijana wenye maadili mem ani vema tukaanza kuwafundisha na kuwajengea msingi mzuri wa maadili mema kwa watoto. Je, ni jukumu la nani kuhakikisha watoto wanakuwa katika misingi ya maadili mema?

+

Ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha watoto wanakuwa kwa kufuata misingi ya maadili mema.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Nini maana ya makazi au taasisi zilizothibitishwa?

+

Ni makazi au taasisi zinazoanzishwa na Serikali au mtu yeyote kwa idhini ya Serikali kwa ajili ya matunzo ya watoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Unaelewaje kuhusu Mpango wa Usalama wa Mtoto?

+

Ni programu yenye lengo la kumlinda mtoto asidhurike na kuboresha afya na maendeleo ya mtoto wakati mtoto yupo nyumbani na mzazi, mlezi au msimamizi.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Ipi nafasi ya mtoto katika urithi ikiwa jina lake limetajwa kama msimamizi wa mirathi kwenye wosia wa wazazi wake?

+

Sheria imeweka katazo kuwa Pamoja na kuwa jina la mtoto limetajwa kwenye wosia lakini hana sifa za kuweza kuwa msimamizi wa urithi. Utaratibu umewekwa kuwa urithi huo utasimamiwa na walezi wawili mpaka pale mtoto huyo atakapofikisha umri wa miaka 18.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je, watoto ambao ni yatima, wazururaji au wale ambao wanalelewa na wazazi au walezi ambao kutokana na tabia za kihalifu au ulevi hawawezi kuwalea watoto hao wanahitaji nini?

+

Watoto hao wanahitaji amri ya malezi, matunzo na ulinzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je, unadhani ni sababu gani zinazosababisha kuwe na watoto wengi wa mitaani nchini Tanzania?

+

Zipo sababu nyingi zinazosababisha kuwe na watoto wengi wa mitaani. Baadhi ya sababu hizo ni kama vile watoto kuwa yatima, uwezo mdogo wa kifamilia, mateso wanayoyapata katika familia zao yamesababisha baadhi yao kutoroka majumbani kwao na kuelekea mitaani.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Afisa Kazi ni mmojawapo wa watumishi wa Serikali wenye wajibu wa kumlinda mtoto. Fafanua mamlaka ya kipekee ya Afisa Kazi katika kumlinda mtoto katika suala zima la ajira kwa watoto.

+

Afisa kazi ana mamlaka ya kuingia katika eneo lolote na kufanya ukaguzi kujiridhisha kuwa kazi anayofanya mtoto au wanazofanya watoto zinaendana na matakwa ya sheria. Anaweza kufanya udadisi na kumhoji mtu yeyote anayeona inafaa.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Mtu binafsi anayetaka kuanzisha makazi au taasisi iliyothibitishwa anatakiwa kuwasilisha ombi lake kwa nani?

+

Anatakiwa kuwasilisha maombi yake kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Ni haki zipi ambazo mtoto anapaswa kuzifurahia kama mtoto?

+

Haki ambazo mtoto anastahili kuzipata na kuzifurahia ni kama zifuatazo; Haki ya kupata elimu, haki ya kutoa maoni, haki ya mali za wazazi,

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Je, mtu anaruhusiwa kuchapisha taarifa yoyote au picha kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram na kusababisha kumtambua mtoto katika shauri lolote lililoko mahakamani?

+

Hapana, kwa mujibu wa kifungu namba 33 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019, hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya hivyo isipokuwa tu kwa idhini ya Mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kurithi kutoka kwa wazazi wake wa kumzaa pale wanapofariki bila ya kuacha wosia?

+

Hapana, mtoto aliyeasiliwa hawezi kurithi kutoka kwa wazazi wake wa kumzaa isipokuwa tu kama waliacha wosia unaompa haki hiyo (kifungu namba 65 (2) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Mtoto anatakiwa kulipwa ujira mdogo hata kama amefanya kazi yenye thamani kubwa?

+

Hapana, mtoto ana haki ya kulipwa ujira unaoendana na thamani ya kazi aliyofanya.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Sheria inamruhusu mtoto mwenye umri kuanzia miaka kumi na nne (14) kuajiriwa katika kazi nyepesi. Je, mtoto ana haki ya kuajiriwa kufanya kazi zinazompelekea kujihusisha na masuala ya kimapenzi kwa malipo?

+

Hapana, mtoto hatakiwi kuajiriwa katika kazi inayompelekea kujihusisha na masuala ya kimapenzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Kwa mujibu wa Sheria, mzazi aliyemuasili mtoto anakuwa na wajibu wa kumlea mtoto huyo kama wa kwake wa kumzaa. Je, mzazi aliyemuasili mtoto anaweza kumlazimisha mtoto huyo kubadili dini na kuacha dini aliyokuwa nayo kabla ya kuasiliwa?

+

Hapana, mzazi aliyemuasili mtoto hatakiwi kumlazimisha mtoto kubadili dini kwani ni kosa chini ya Sheria ya Mtoto (2019) kifungu namba 158 (d).

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Je, ni halali kisheria kumtumia mtoto katika maonyesho ya harusi wakati wa usiku?

+

Hapana, si halali kisheria kumtumia mtoto katika maonyesho ya harusi wakati wa usiku.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je, ni sahihi na halali kumbagua mtoto mlemavu?

+

Hapana, si halali kumbagua mtoto mwenye ulemavu kwasababu ana haki ya kuwa sawa na watoto wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Je, ni halali kwa mtoto kuwekwa mahabusu moja na watuhumiwa wengine ambao ni watu wazima na ambao hata si ndugu zake?

+

Hapana, si halali mtoto kuwekwa mahabusu moja na watu wazima isipokuwa kama ni ndugu zake wote.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, ni sahihi kumwadhibu mtoto hata kama kutokana na umri wake hawezi kuelewa lengo la adhabu hiyo?

+

Hapana, si sahihi na ni kinyume na sheria kumpa mtoto adhabu ambayo kutokana umri wake au kiwango chake hawezi kuelewa lengo la adhabu hiyo (kifungu namba 13 (2) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, mtoto mwenye umri wa miaka kumi na tatu (13) na ambaye hajamaliza elimu ya msingi ana haki ya kupata weledi katika nyanja za ufundi na mafunzo ya ufundi?

+

Hapana, umri wa chini wa mtoto kuanza mafunzo ya ufundi ni miaka kumi na nne (14) au aliyemaliza elimu ya msingi.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Mzazi au mlezi anaweza kuamua kumnyima mtoto haki ya kupata huduma ya afya kwasababu dini ya mzazi au mlezi huyo hairuhusu kupatiwa huduma ya afya.

+

Hapana, watoto wote wana haki sawa ya kupatiwa huduma za msingi bila kuangalia dini ya mzazi au mlezi wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Ni madhara gani mtoto anaweza kuyapata kama akiruhusiwa kuingia katika maeneo kama kumbi za muziki, baa au klabu ya usiku?

+

i. Anaweza kudhuriwa na watu wabaya, ii. Anaweza kujifunza maadili ambayo si mema katika jamii kama vile kunywa pombe, kuvuta sigara, kuvuta bangi n.k. iii. Anaweza kupoteza muda wa kwenda shuleni au kwenye mafunzo n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Mara nyingi watoto wamekuwa wahanga wa makosa mbalimbali ya kingono kama vile kubakwa, kunajisiwa, kunyanyaswa kijinsia na kulawitiwa. Nini kifanyike kukomesha tatizo hili?

+

i. Elimu itolewe kwa umma kuachana na imani potofu kwani badhi ya watu hufanya vitendo hivyo kutokana na imani potofu kama vile kuamini kuwa watapata mali n.k. ii. Adhabu kali zitolewe kwa wanaothibitika kutenda vitendo hivi viovu ili iwe funzo kwa jamii nzima na watu wengine wasiendelee kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Pamoja na kuwa sheria imeruhusu mtoto wa umri fulani kuweza ajiriwa lakini imeweka katazo mtoto kuajiriwa kwa kazi ya kinyonyaji. Ni vitu gani vitaonesha kuwa kazi aliyoajiriwa mtoto ni ya kinyonyaji?

+

i. Ikiwa inadhuru afya ya mtoto na kuathiri maendeleo yake ii. Inazidi saa sita kwa siku iii. Hailingani na umri wake iv. Mtoto anapata malipo pungufu

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Kikawaida, Mahakama haiwezi kutoa amri ya uasili wa mtoto bila ridhaa ya wazazi au mlezi wake. Lakini kuna mazingira Mahakama inaweza kuachana na ridhaa ya wazazi au mlezi; mazingira hayo ni kama yafuatayo:

+

i. Kama Mahakama imejiridhisha kuwa mzazi au mlezi huyo amemtelekeza au amekuwa akimtesa mtoto huyo. ii. Kama Mahakama imejiridhisha kuwa mzazi au mlezi husika hapatikani au hawezi kutoa ridhaa au anakataa kutoa ridhaa bila sababu za msingi.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Sheria imetoa katazo kwa baadhi ya kazi zenye madhara kwa mtoto kiafya au kazi ambazo haziwezi kumfanya mtoto apate haki yake ya elimu. Kazi hizo ni zipi?

+

i. Kazi za ubaharia ii. Kazi za uchimbaji madini au upasuaji mawe iii. Kazi za ubebaji wa mizigo mizito iv. Kazi za viwanda vya uzalishaji ambapo kemikali zinazalishwa au kutumika v. Kufanya kazi ambazo machine zinatumika vi. Kufanya kazi sehemu kama vile baa, hoteli, na sehemu za starehe.

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Kwa mujibu wa kifungu namba 166 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, ni kosa la jinai kwa mzazi, mlezi au mtu yeyote mwenye wajibu wa kumlea na kumtunza mtoto na akiwa na uwezo wa kufanya hivyo kumtelekeza mtoto huyo kwa makusudi na bila sababu ya msingi. Kifungu hiki cha sheria kinalindaje maslahi bora ya mtoto?

+

i. Kifungu hiki kinamfanya mzazi kutimiza wajibu wake wa kumlea na kumtunza mtoto ipasavyo bila kuyakimbia majukumu yake ilihali ana uwezo wa kumtunza. ii. Kifungu hiki kinamfanya mtoto apate haki zake za msingi na mahitaji muhimu kama vile chakula na elimu kutoka kwa mzazi, mlezi au mtu yeyote aliyepewa wajibu huo kwa amri ya Mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Kila mtoto ana haki ambazo anapaswa kuzifurahia lakini hii haimaanishi kuwa mtoto hana wajibu wa kutimiza; Je wajibu wa mtoto ni upi?

+

i. Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamano wa familia ii. Kuheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake na watu wazima muda wote na atawasaidia pale inapohitajika. iii. Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kimwili na kiakili kadiri ya umri na uwezo wake iv. Kutunza na kuimarisha mshikamano wa jamii na taifa v. Kutunza na kuimarisha mambo mema katika utamaduni wa Taifa kwa ujumla katika uhusiano na wanajamii au taifa

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Taja sababu tatu zinazowafanya watoto kutenda makosa ya jinai kama vile wizi.

+

i. kujifunza kutoka kwa watu wanaowazunguka kama vile wazazi, walezi, marafiki au majirani, ii. Kukosa mahitaji ya msingi kama vile chakula na mavazi, iii. Kutokufunzwa maadili mema na wazazi wao.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Yapi ni majukumu na wajibu wa mzazi kwa mtoto?

+

i. Kumlinda mtoto dhidi ya utelekezwaji, ubaguzi, vurugu, unyanyasaji, na madhara ya kimwili na kiakili. ii. Mbili, kutoa malezi, mwongozo, msaada na matunzo kwa mtoto wake iii. Tatu, kuhakikisha mtoto anapata haki zake zote za msingi kama vile haki ya elimu, haki ya huduma ya afya n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Yapi ni majukumu ya Afisa Ustawi wa Jamii kuhusiana na malezi au usimamizi wa mtoto?

+

i. Kumshauri na kumnasihi mtoto na familia yake, ii. Kufanya mapitio ya mara kwa mara katika mpango wa maendeleo ya mtoto kwa kushauriana na mtoto na wazazi wake au mlezi, iii. Kuchukua hatua zinazostahili ili kuhakikisha kwamba mtoto hapati madhara yoyote.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je ni zipi ni haki za mtoto pindi wazazi watakapotengana au kutalakiana?

+

i. Matunzo na elimu yenye ubora ule ule aliyokuwa anaupata kabla wazazi wake hawajatengana ii. Kuishi kwa mzazi ambaye, kwa maoni ya mahakama, ana uwezo wa kumlea mtoto kwa kuzingatia maslahi yam toto iii. Kutembelea na kukaa kwa mzazi mwingine wakati wowote atakapotaka isipokuwa kama mpango huo hautaingilia programu ya masomo au mafunzo.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Ni kosa kisheria kumwajiri mtoto kufanya kazi muda wa usiku (yaani kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi). Unadhani ni kwanini?

+

i. Mtoto anaweza kudhuriwa nyakati za usiku kama vile kubakwa au kufanyiwa vitendo vingine viovu. ii. Mtoto anaweza kukosa muda wa kujiandaa kuhudhuria shuleni siku inayofuata kwasababu anaweza kuchoka wakati wa usiku

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Je? ni zipi mila na desturi hapa nchini Tanzania ziko kinyume na haki za watoto?

+

i. Ukeketaji wa watoto wa kike ii. Ndoa za utotoni ambazo huwakosesha watoto haki yao ya elimu

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Toa ushauri nini kifanyike kupunguza au kuondoa tatizo la baadhi ya watoto kujihusisha na vitendo vya wizi na udokozi mitaani bila kuvunja haki za watoto hao.

+

i. Wazazi na walezi wawajibike ipasavyo kuwalinda watoto wawapo majumbani ii. Kama wazazi au walezi wa hao watoto hawana uwezo kiuchumi wa kuwalea watoto hao, basi waombe Mahakama itoe amri ya malezi na ulinzi ili watoto hao walelewe na ndugu au watu wengine wanaofaa au wapelekwe kwenye shule za maadilisho au taasisi zilizothibitishwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Sheria inampa wajibu mzazi, mlezi au mtu yeyote anayemtunza mtoto kutoa mahitaji ya chakula, malazi, mavazi, matibabu, elimu, uhuru wa mawazo na haki ya kucheza na kuburudika. Jukumu hilo hukoma pale mtoto anapotimiza umri wa miaka kumi na nane. Ni kwa mazingira gani jukumu hilo linaweza kuendelea ilihali mtoto ametimiza miaka kumi na nane?

+

Jukumu hilo linaweza kuendelea pale ambapo” mtoto” huyo ametimiza miaka kumi na nane kama bado anaendelea na masomo au mafunzo.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Ni kwa mazingira gani mtu anaweza kumnyima mtoto haki ya kushiriki katika michezo au katika shughuli chanya za kiutamaduni na kisanii au katika shughuli nyingine za starehe?

+

Kama ushiriki wa mtoto katika shughuli hizo si kwa maslahi bora ya mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Nchini Tanzania sio kila mtu anatambulika kama mtoto kisheria. Ni umri gani unaotambulika kisheria kwa mtu kutambulika kama mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 4(1) cha Sheria ya mtoto Sura ya 13, mtoto ni mtu aliye chini ya umri wa miaka 18.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, wazazi wa mtoto wakifariki wote, jukumu la kumlea mtoto huyo linaweza kuhamishiwa kwa mtu gani mwingine?

+

Kwa mujibu wa Kifungu namba 9 (4) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019, endapo wazazi wa mtoto wamefariki wote, jukumu la kumlea mtoto huyo linaweza kuhamishiwa kwa ndugu au mlezi aliyeteuliwa kwa amri ya mahakama au taratibu za kimila.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Endapo mtoto atafanya kosa ambalo litasababisha kufikishwa mahakamani. Ni mahakama gani ambayo itakuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo?

+

Mahakama ya Watoto ndio yenye mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusisha Watoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Pamoja na kuwa mtoto ana haki ya kupata mahitaji mbalimbali. Je, ni mahitaji gani ya msingi ambayo mtoto anastahili kuyapata?

+

Mahitaji ya msingi ambayo mtoto anastahili kuyapata ni kama vile chakula, mavazi na mahali salama pa kuishi.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Ni sawa kwa serikali kupitia waraka wa elimu namba 02 wa mwaka 2023 ambao umeweka katazo kwa wamiliki wa shule kutoruhusu watoto kuanzia darasa la awali mpaka darasa la nne kukaa bweni?

+

Malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa wa unaotolewa na familia kupitia wazazi/walezi wa watoto hao. Hivyo, watoto wengi wamekuwa wakipata malezi shuleni na sio malezi sahihi ya wazazi au walezi. Pia, kuwepo kwa watoto bweni kwa muda mrefu inaondoa dhana ya “Elimu ni Maisha na Maisha ni kazi” hivyo kuna juhudi hafifu za kujenga maadili ya wanafunzi na kuwajengea moyo wa kupenda, kuthamini na kufanya kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Kwa mujibu wa sheria, jambo la msingi kuzingatia katika kufanya maamuzi yanayomhusu mtoto ni maslahi bora ya mtoto husika. Mambo gani ya yanayozingatiwa wakati wa kuamua nani amlee mtoto kati ya baba na mama baada ya kutengana kwa wazazi wake.

+

Mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa ni kama vile: i. Umri na jinsia ya mtoto mfano, mtoto chini ya umri wa miaka saba (7) anatakiwa kukaa na mama yake. ii. Maoni ya mtoto ikiwa maoni hayo yametolewa huru. iii. Kama itaonekana ni muhimu kuwaweka watoto pamoja na kuzingatia umuhimu wa mwendelezo wa malezi na usimamizi wa mtoto iv. Sababu nyingine ambayo mahakama itaona inafaa

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Ni mamlaka gani hapa nchini yenye wajibu wa kusajili kuzaliwa kwa mtoto na ni nani ana wajibu wa kuomba usajili huo.

+

Mamlaka yenye wajibu wa kusajili kuzaliwa kwa mtoto ni Ofisi ya Msajili Mkuu wa vizazi na vifo (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini). Mzazi au mlezi wa mtoto ndio wanapaswa kuomba usajili wa kuzaliwa kwa mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

je, mama wa mtoto anaweza kukataa kumwambia mtoto jina la baba yake mzazi kwasababu tu baba huyo alishawahi kukana mimba ya mtoto huyo kuwa siyo yake?

+

Mtoto ana haki ya kujua wazazi wake waliomzaa. Hivyo, pale mama anapokataa kumwambia mtoto jina la baba yake, mtoto anaweza kuomba Afisa Ustawi wa Jamii au ngazi zingine mama alazimishwe kumtaja baba wa mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, ni zipi haki za mtoto katika kuhakikisha anakuwa katika misingi iliyo bora?

+

Mtoto anazo haki mbalimbali kama vile haki ya kutambuliwa kibinadamu, haki ya kutobaguliwa kutokana na rangi, jinsia, asili ya kitaifa, ulemavu, dini, kabila au sifa nyingine. Pia, haki ya kuishi, kulindwa, kushiriki katika kutoa mawazo na maamuzi yanayohusu maendeleo yake, haki ya kulindwa dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je, sheria imeweka utaratibu gani kwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano kwenye suala la afya?

+

Mtoto chini ya umri wa miaka 5 amepewa nafasi ya kupata matibabu bure bila malipo.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, mtoto ana haki ya kuchagua uraia?

+

Mtoto hana (hawezi) haki ya kuchagua uraia. Hii ni kwa mujibu wa kifungu namba 13 cha sheria ya uraia.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Mkataba ni makubaliano baina ya pande mbili au zaidi ambayo yanaingiwa kwa maslahi Fulani ya kila upande. Japokuwa mtu yeyote anaweza ingia kwenye mkataba lakini sio mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kuingia kwenye mkataba. Je, ni kwanini mtoto haruhusiwi kuingia kwenye mikataba?

+

Mtoto haruhusiwi kuingia kwenye mkataba kwasababu sheria inamtambua kama mtu asiye na uwezo wa kuingia kwenye mikataba kutokana na umri ambao inaaminika kuwa hawezi kuwa na maamuzi ambayo yana busara ya kutosha kuingia kwenye mkataba huo, Japokuwa kuna nyakati ambazo mtoto anaweza ingia kwenye mkataba.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Katika kuhakikisha mtoto analindwa na ajihusishi na mambo au matumizi ambayo yanaweza kumletea madhara nchini Tanzania, yapo makatazo ambayo yamewekwa. Taja walau sehemu mbili ambazo mtoto haruhusiwi kuingia, pia taja vitu ambavyo mtoto hatakiwi kuuziwa.

+

Mtoto hatakiwi kuingia kwenye ukumbi wa muziki baa au klabu ya usiku. Pia, mtoto haruhusiwi kuuziwa sigara, pombe, pombe kali, madawa ya kulevya au kitu chochote kinacholewesha.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, ni haki zipi za kipekee ambazo mtoto mwenye ulemavu anazistahili?

+

Mtoto mwenye ulemavu anastahili uangalizi maalum, matibabu na huduma nafuu kwa ajili ya kumrekebisha na kupata fursa sawa katika elimu na mafunzo kwa kadri inavyowezekana ili aweze kuendeleza kipaji alicho nacho, uwezo wake na kuweza kujitegemea.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je, ni wajibu wa nani kutoa taarifa juu ya kudhurika, kupotea, kutengwa au kuteketezwa kwa mtoto?

+

Mwanajamii yeyote mwenye sababu ya msingi ya kuamini hivyo (Kanuni ya 11 (1) ya Kanuni za Usalama wa Mtoto, 2014)

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, mzazi ana wajibu upi kwa mtoto wake?

+

Mzazi au mlezi ana wajibu wa kulinda maisha ya mtoto wake, kulinda utu, heshima, kupata elimu, chakula na malazi. (kifungu namba 9 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Kila kitu katika jamii kinaongozwa kwa sheria. Je, kuna sheria ya mtoto nchini Tanzania?

+

Ndio, kuna sheria yam toto iliyotungwa na Bunge na kutiwa Saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2019 ambayo kwa ujumla wake imeweka bayana sheria mbalimbali zinazomuhusu mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, mtoto ana haki ya kupata uraia?

+

Ndio, kwa mujibu wa kifungu namba 6(1) ya sheria ya mtoto, mtoto anayo haki ya kupata uraia.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, mtoto ana haki ya kufahamu ndugu zake?

+

Ndio, mtoto ana haki ya kufahamu ndugu zake kwa mujibu wa kifungu namba 6(1) ya sheria ya mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je, mtoto anaweza kuwa shahidi katika kesi yoyote?

+

Ndiyo

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, ni kosa la jinai kumchukua mtoto kinyume na sheria kutoka kwa mtu aliyepewa amri ya malezi ya mtoto huyo na mahakama?

+

Ndiyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu namba 114(1)(i) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, ili kulinda maslahi bora ya mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, maombi ya amri ya malezi ya mtoto yanaweza kuwasilishwa mahakamani baada ya mtoto kutimiza umri wa miaka kumi na nane?

+

Ndiyo, maombi ya amri ya malezi ya mtoto yanaweza kuwasilishwa mahakamani baada ya mtoto kutimiza umri wa miaka kumi na nane LAKINI kwa kibali maalumu cha Mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je, mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kurithi mali za marehemu mzazi aliyemuasili hata pale ambapo marehemu amefariki bila kuacha wosia?

+

Ndiyo, mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kurithi sawa na watoto wengine waliozaliwa na marehemu.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kujulishwa kuwa aliasiliwa? Na ni nani mwenye wajibu wa kumjulisha hivyo?

+

Ndiyo, mtoto ana haki ya kujulishwa kuwa aliasiliwa. Mtu mwenye wajibu wa kumjulisha mtoto huyo ni mzazi aliyemuasili.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, mtoto aliyekutwa na hatia ya ubakaji anaendelea kuwa na haki ya kupata elimu baada ya kukutwa na hatia hiyo?

+

Ndiyo, mtoto anaendelea kuwa na haki ya kupata elimu hata kama amekutwa na hatia ya kukinzana na sheria yoyote.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, mtoto anaweza kukamatwa tena baada ya kutoroka kutoka kwenye shule iliyothibitishwa?

+

Ndiyo, mtoto anaweza kukamatwa bila hata ya kibali na kurudishwa shuleni hapo.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Je, mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana haki ya kupata matunzo kutoka kwa baba yake?

+

Ndiyo, mtoto yeyote ana haki ya kupata matunzo kutoka kwa baba yake bila kujali uzao wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je mtu asiye raia wa Tanzania anaweza kumwasili mtoto wa Tanzania? Na sifa za mtu huyo ni zipi?

+

Ndiyo, mtu ambaye sio raia wa Tanzania anaweza kumwasili Mtanzania iwapo mtoto huyo hatoweza kutunzwa kwa namna yenye maslahi kwake wakati akiwa Tanzania. Sifa za mtu huyo ni kama zifuatazo: i. Awe ameishi Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ii. Amemlea mtoto husika kama mlezi wa kambo kwa kipindi cha angalau miezi mitatu. iii. Hana kumbukumbu ya makosa ya jinai na iv. Ameidhihirishia Mahakama kuwa nchi yake ya asili inatambua amri ya kuasili (kifungu namba 74 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2019).

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Nini maana ya Mahabusu ya Watoto?

+

Ni mahali ambapo mtoto anapata hifadhi salama wakati shauri lake linashughulikiwa

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Unaelewa nini kuhusu “Mtoto anayekinzana na sheria’’ na nini mfano wake?

+

Ni mtoto mwenye hatia ya kutenda jambo ambalo ni kosa kisheria. Mfano ni mtoto aliyefanya kitendo cha wizi au ubakaji.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Nini maana ya shule ya maadilisho au shule iliyothibitishwa?

+

Ni shule iliyoanzishwa au iliyotamkwa kwa ajili ya kuwafunza maadili watoto wanaokutwa na hatia za kutenda makosa.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Ni vitu gani huzingatiwa na Mahakama kama ushahidi au uthibitisho kuwa mtu fulani ni mzazi wa mtoto husika?

+

Ni vitu gani huzingatiwa na Mahakama kama ushahidi au uthibitisho kuwa mtu fulani ni mzazi wa mtoto husika?

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je, ni nani mwenye wajibu wa kutoa taarifa (kuripoti) katika Serikali za Mitaa ya eneo husika iwapo haki za mtoto zinakiukwa?

+

Ni wajibu wa kila mwanajamii ambaye ana ushahidi au taarifa kwamba haki za mtoto zinakiukwa na mtu yeyote kuripoti suala hilo katika Serikali za Mitaa.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Ni watu gani wanaweza kuiomba Mahakama kutoa amri ya kuthibitisha malezi ya mtoto?

+

Ni watu gani wanaweza kuiomba Mahakama kutoa amri ya kuthibitisha malezi ya mtoto?

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Je, kwanini Mahakama ya Watoto inatakiwa kukaa katika jengo tofauti na jengo ambalo kwa kawaida hutumika kusikiliza kesi za watu wazima na mashauri yanatakiwa yaendeshwe kwa faragha?

+

Sababu ya kwanza ni kumtunzia siri mtoto kwasababu yeye ni taifa la kesho na hakuna ajuaye mtoto huyo anaweza kuwa na wadhifa gani hapo baadaye. Sababu ya pili ni kumwepusha mtoto kutengwa na kupewa majina na wenzake yanayoashiria kuwa yeye ni mhalifu.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je, mtoto ana haki gani ya kurithi mali za mzazi/wazazi wake baada ya kufariki.

+

Sheria imeelekeza kuwa mtoto anayo haki ya kurithi toka kwa wazazi wake

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Je, mtu anaetambulika kama mtoto anaweza kuridhia kujihusisha na mapenzi?

+

Sheria inamtambua mtoto kama mtu asiye na uwezo wa kufanya maamuzi, hivyo hata kama alikubali mwenyewe itachukuliwa kama hakukuwa na ridhaa yoyote.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je, ni sahihi kumlazimisha mtoto kufanya kazi kwa vitisho vya kumpa adhabu?

+

Si sahihi na ni haramu mtu kumlazimisha mtoto kufanya kazi kwa vitisho vya kumpa adhabu na kazi ambazo hazina maslahi ya moja kwa moja kwa jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Taasisi zipi Tanzania zina wajibu wa kulinda haki za watoto?

+

Taasisi ambazo zinapaswa kulinda haki za watoto ni: Ustawi wa Jamii, Mahakama, Familia, Jamii na Jeshi la Polisi.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Unaelewa nini kuhusu uasili wa mtoto?

+

Uasili wa mtoto ni mchakato wa kisheria unaohamisha uwajibikaji wa mzazi kutoka kwa wazazi wa kumzaa mtoto kwenda kwa mtu mwingine au watu wengine kwa ajili ya malezi ya mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Sheria nchini Tanzania imefafanua kuwa mtoto anayo haki ya kufanya kazi nyepesi. Je, ni umri gani unaoruhusiwa kisheria kwa mtoto kuajiriwa nchini Tanzania?

+

Umri wa chini wa mtoto kuajiriwa ni miaka kumi na nne (14).

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Uthibitisho ni jambo la msingi ili kuweza kuthibitisha umri sahihi wa mtoto. Ni kitu gani kinachothibisha umri wa mtoto nchini Tanzania?

+

Umri wa mtoto unathibitshwa na Cheti cha kuzaliwa kilichotolewa na mamlaka husika (RITA). Pia, vithibitisho vingine vinaweza tumika kuthibitisha umri wa mtoto ikiwa mtu anayesema kuwa ni mtoto ataonekana na mahakama kuwa na umri wa miaka kumi na nane au zaidi, kama vile umri utakaotajwa na mzazi au mlezi wa mtoto au Afisa Ustawi wa jamii ndio utakuwa umri sahihi wa mtoto huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Kuna wakati mama mwenye mtoto mchanga anawekwa gerezani akiwa na mtoto wake. Katika hali kama hii, uongozi wa magereza unakuwa na wajibu gani kwa mtoto huyo?

+

Uongozi wa magereza una wajibu wa kuhakikisha kuwa mtoto anapata matunzo yanayohitajika katika namna inayostahili, mlo kamili, virutubisho na huduma ya afya pamoja na chanjo.

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Takwimu zinaonesha kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wa mitaani nchini Tanzania. Ni jambo gani lifanyike ili kuweza kupunguza wimbi la watoto wa mitaani nchini Tanzania?

+

Wazazi wajitahidi kuwalea watoto kwa upendo hasa pale wanapokuwa wakiishi na baba wa kambo au mama wa kambo. Pia, kuwekwe mazingira mazuri ya kuwakusanya na kuwalea katika vituo vya kulelea watoto yatima na wasiojiweza ili kuwafanya watoto hao kuendelea kupata mahitaji ya msingi, lakini pia kupata haki zao wanazostahili.

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Kuna wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, watoto kama kundi maalumu hapa nchini wako chini ya wizara gani?

+

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu

Sheria Kiganjani
Learn More
100

Je, unadhani nani ana kosa kati ya mzazi anayemruhusu mtoto kwenda baa na mmiliki wa ukumbi wa baa anayemruhusu mtoto huyo kuingia baa?

+

Wote wana makosa. Mzazi hatakiwi kumruhusu mtoto kwenda baa na wala mmiliki wa baa hatakiwi kumruhusu mtoto kuingia baa.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand