Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Kuna baadhi ya watu huwa wana tabia ya kupanda nyuma ya magari madogo ya mizigo, malori na magari mengine yaliyotengenezwa kwa ajili ya kubeba mizigo tu. Je, hii imeruhusiwa kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, hii hairuhusiwi kisheria. Sheria inakataza mtu yeyote kupanda nyuma ya gari la mizigo.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, magari ya dharula yanaruhusiwa hata kuhatarisha maisha ya watu kwasababu ni ya dharula na yanawahi?

+

Hapana, magari ya dharula yanaruhusiwa tu kutotii baadhi ya kanuni bila kuhatarisha maisha ya watu wala mali za watu.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, mifugo kama vile ng\'ombe na kondoo wanaruhusiwa kisheria kutumia barabara bila usimamizi wa watu?

+

Hapana, wanyama wanatakiwa kuwa chini ya usimamizi wa watu wanaowachunga ili kulinda wasisababishe ajali barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila mtu ana haki ya kumiliki mali yoyote halali. Je, mtu anaweza kusajiliwa kuwa mmiliki wa gari akiwa na umri wa kuanzia miaka mingapi?

+

Mtu anaweza kusajiliwa kama mmiliki wa gari akiwa na umri wa kuanzia miaka kumi na nane (18) tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

: Sheria inaweka katazo kwa mtu asiye na utimamu wa akili kusajiliwa kama mmiliki wa gari. Je, kuna mbadala uliotolewa na Sheria juu ya namna mtu mwenye utimamu wa akili anaweza kuwa na haki ya kusajiliwa gari lake kwa njia yoyote?

+

Mtu asiye na akili timamu gari lake linaweza kusajiliwa kwa jina la mdhamini wake ambaye ndiye atakayesajiliwa kama mmiliki halali wa gari hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Gari lolote linatakiwa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria. Je, ni nani mwenye wajibu wa kufanya maombi kwa Msajili ili gari lisajiliwe?

+

Mtu mwenye wajibu wa kuomba usajili wa gari ni mmiliki wa gari husika

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, dereva au mtu yeyote anayehojiwa na askari ana wajibu wa kutoa majibu ya ukweli kwa askari huyo?

+

Ndiyo, dereva au mtu yeyote anayehojiwa na askari ana wajibu wa kutoa majibu ya ukweli na ni kosa la jinai kutoa majibu au kauli za uongo.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je, ni muhimu kwa abiria kuvaa kofia ngumu?

+

Ndiyo, inashauriwa abiria wa nyuma pia avae kofia ngumu. Hii ni kwasababu za kiusalama, yaani kumkinga abiria mwenyewe wakati wanapopata ajali.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, gari la abiria linatakiwa kusimama kwanza kabla ya kuvuka reli?

+

Ndiyo, linatakiwa kusimama kwanza ya kabla ya kuvuka reli

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, ni lazima kisheria baiskeli kuwa na kengere au honi?

+

Ndiyo, ni lazima kwa mujibu wa sheria baiskeli kuwa na kengere au honi.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je, mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne (14) anaweza kusajiliwa kama mmliki wa pikipiki?

+

Ndiyo, Sheria inamruhusu mtoto mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nne (14) kusajiliwa kama mmiliki wa pikipiki.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, pikipiki inatakiwa kupakia abiria wangapi kwa mujibu wa Sheria?

+

Pikipiki inatakiwa kupakia abiria mmoja tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Nini maana ya Rejesta ya magari?

+

Rejesta ya magari ni daftari linalotunza taarifa za magari baada ya kufanyiwa usajili kwa mujibu wa sheria. Taarifa hizo ni kama vile mmiliki wa gari, aina ya gari na kadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Ni kawaida leseni kupotea au kunyeshewa na mvua. Je, unaweza kumshauri afanye nini dereva ambaye leseni yake imepotea ili aendelee kuendesha gari lake?

+

Sheria inampa haki dereva yeyote ambaye leseni yake imepotea au kuharibika kwa namna yoyote kuomba nakala halisi ya leseni hiyo kwa Msajili wa magari na atapewa nakala hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Unaelewa nini kuhusu maana ya \"Alama za barabarani\"?

+

Alama za barabarani ni mwandishi, michoro au vitu vyovyote ambavyo huwekwa barabarani kwa lengo la kutoa maelekezo, taarifa au amri fulani kwa watumiaji wa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Nini maana ya \"alama za pundamilia\"?

+

Alama za pundamilia ni alama za kivuko cha watembea kwa miguu inayoonyeshwa na mistari myeupe sambamba na mwelekeo wa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, baiskeli inaruhusiwa kubeba watu wangapi jumla akiwemo na dereva?

+

Baiskeli inaruhusiwa kubeba watu wawili tu akiwemo na dereva wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je, Baraza linalohusika na mambo ya usalama barabarani hapa Tanzania Bara linaitwaje?

+

Baraza linalohusika na mambo yote ya usalama barabarani hapa Tanzania Bara linaitwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Kwa mujibu wa Sheria, mtu yeyote ndani ya gari haruhusiwi kumsumbua dereva au kumfanyia kitendo chochote ambacho kinaweza kumpunguzia umakini dereva akiwa anaendesha gari. Je ni kwanini?

+

Bunge liliona kuwa kuna hatari ya baadhi ya watu kumsumbua dereva kwenye gari na kumpotezea umakini wake katika uendeshaji na hatimaye kuweza kusababisha ajali kirahisi. Ndiyo maana Bunge likaamua kuweka katazo hilo katika Sheria kwamba mtu akiwa ndani ya gari haruhusiwi kumfanyia dereva vitendo vyovyote ambavyo vina uwezo wa kupoteza au kupunguza umakini wa dereva katika jukumu lake la kuendesha.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Ni mambo gani anapaswa kuyazingatia dereva pindi anapokuwa barabarani?

+

Dereva anapokuwa barabarani anapaswa kuzingatia mambo mbalimbali kama vile i. Kuendesha kwa usalama ii. Kuendesha kwa umakini iii. Kuwathamini wengine kama watembea kwa miguu, watu wenye ulemavu n.k iv. Kuendesha kwa kuangazaangaza wakati wote v. Kuendesha kwa kujihami vi. Kutumia ishara kuwaonya na kuwataarifu watumiaji wengine wa barabara vii. Kuendesha kwa kufuata alama zote za barabarani

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Je, ni vitu gani vinatakiwa kwa mujibu wa sheria kubandikwa na dereva kwenye gari lake?

+

Dereva anatakiwa kubandika kibandiko au stika ya leseni yake ya udereva pamoja na kibandiko au stika ya bima isipokuwa kwa magari yanayomilikiwa na Serikali.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je, dereva wa gari au chombo chochote cha moto ana wajibu gani kisheria baada ya kusababisha ajali kwa mtu, gari lingine au chombo chochote cha moto au mali yoyote barabarani?

+

Dereva baada ya kusababisha ajali anatakiwa kusimama na kutoa msaada inavyowezekana kwa mtu huyo aliyepata ajali isipokuwa kama kutokana na sababu za kiusalama haruhusiwi kusimama mahali hapo. Dereva ana wajibu pia wa kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu juu ya kutokea kwa ajali hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je, kwa maoni yako ni vitu gani ambavyo dereva anapaswa kuvibeba kila mara anapoendesha gari?

+

Dereva kila mara anapoendesha gari anatakiwa kuwa na leseni halisi ya udereva inayomruhusu kuendesha gari ya daraja hilo; pia, anatakiwa kuwa na cheti halisi cha usajili wa gari au nakala halisi.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Kwa maoni yako unadhani ni kwanini sio sawa kwa dereva kuendesha chombo cha moto huku akiwa amelewa?

+

Dereva wa chombo cha moto hatakiwi kuendesha huku akiwa amelewa kwani kwa kufanya hivyo yupo katika hatari kubwa ya kusababisha ajali.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, mwongozo wa usalama barabarani unatoa maelekezo kwa dereva wa gari au chombo chochote cha usafiri kuendesha upande gani wa barabara?

+

Dereva wa chombo chochote cha usafiri anatakiwa kuendesha upande wa kushoto mwa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je, kwa mujibu wa mwongozo wa usalama barabarani, dereva wa gari anapolipita gari lingine barabarani kwa kuelekea upande mmoja anatakiwa kulipita gari hilo kwa upande gani?

+

Dereva wa gari anapotaka kulipita gari lingine barabarani wakielekea upande mmoja anatakiwa kupita upande wa kulia.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Je, mwongozo wa usalama barabarani unatoa maelekezo ya kutembea upande gani kwa mtembea kwa miguu

+

Endapo kuna njia ya watembea kwa miguu, sheria inamtaka kupita upande wa kulia wa magari ili aweze kuyaona magari yanayokuja.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Kwa maoni yako unadhani gari linatakiwa kuwa na sifa gani ili likidhi vigezo kabla ya kuendeshwa na dereva barabarani?

+

Gari linatakiwa kuwa katika hali nzuri ya kiufundi, liwe ndani ya eneo linaloruhusiwa, liendane na viwango vyote vya utengenezaji na kikomo cha idadi ya abiria ambao wanaweza kubebwa na lipakie mizigo kiusalama kulingana na kanuni.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, gari la mwalimu wa sekondari anayewahi kazini kufundisha wanafunzi katika shule inayomilikiwa na Serikali ni mojawapo ya magari ya dharula ambayo si lazima kutii baadhi ya kanuni za usalama barabarani?

+

Hapana, gari la mwalimu si mojawapo ya magari ya dharula.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

e, madereva wa magari ya mizigo wana haki ya kusimama na kupakia mizigo sehemu yoyote barabarani?

+

Hapana, madereva wa magari ya mizigo wanapaswa kusimama na kupakia mizigo maeneo maalum kwa kazi hiyo tu na si mahali popote barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Je, ni kosa kisheria mtu kutozwa kiasi cha fedha ili kupatiwa rejesta ya magari kwenye ofisi ya Msajili wa Magari?

+

Hapana, ni halali kabisa kwa mujibu wa sheria mtu kutozwa kiasi cha fedha ili apatiwe rejesta ya magari kwa ajili ya kufanya ukaguzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Je, ni sawa kwa abiria kusafiri kwenye gari bila kufunga mkanda?

+

Hapana, ni kinyume na sheria mtu kusafiri kwenye gari bila kufunga mkanda na ni kosa la jinai.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Je, mtu mwenye ujuzi mzuri wa kuendesha gari lakini leseni yake imefutwa anaruhusiwa kuendesha gari barabarani kwasababu tu ana ujuzi mzuri wa kuendesha?

+

Hapana, ni kosa la jinai kuendesha gari kama leseni imefutwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je, mtu anaruhusiwa kuendesha gari kwa spidi ndogo sana bila sababu ya msingi kwa lengo tu la kuwasumbua watumiaji wengine wa barabara?

+

Hapana, ni kosa la jinai kwa dereva yeyote kuendesha gari kwa spidi ndogo sana isiyo ya kawaida yenye kiwango cha kuwasumbua na kuwazuia watumiaji wengine wa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Leseni za kuendesha magari zina madaraja tofauti. Je, dereva mwenye leseni anayeruhusiwa kuendesha magari ya daraja fulani tu anaruhusiwa kisheria kuendesha magari ya madaraja mengine kinyume na leseni yake?

+

Hapana, sheria imeweka katazo kwa dereva kuendesha gari ambalo si la daraja analoruhusiwa kuendesha kwa mujibu wa leseni yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, mtu asiye na akili timamu anaweza kusajiliwa kama mmiliki wa gari?

+

Hapana, Sheria imeweka katazo kwa mtu ambaye hana utimamu wa akili kusajiliwa kama mmiliki wa gari.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, mtu anaweza kuhukumiwa kwa kosa la kushindwa kutoa leseni yake kwa askari ndani ya masaa sita tu?

+

Hapana, Sheria inaelekeza kuwa mtu anaweza kuhukumiwa kwa kosa la kushindwa kutoa leseni kwa askari kama ameshindwa kuitoa ndani ya siku tatu zinazofuata baada ya kuamriwa kufanya hivyo. Kwahiyo kama ni ndani ya masaa sita tu, mtu hawezi kuhukumiwa kwa kosa tajwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je, inaruhusiwa kisheria dereva kumpa leseni yake mtu mwingine ili aitumie kuendesha gari lake?

+

Hapana, sheria inakataza kwa mtu mwenye leseni yenye jina lake kumkabidhi mtu mwingine aitumie.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Je, sheria inamtambua mtoto mwenye umri chini ya miaka mitatu na ambaye hajakaa kwenye kiti cha gari kama abiria?

+

Hapana, Sheria inamtambua mtoto mwenye umri chini ya miaka mitatu na ambaye hajakalia kiti kama si abiria.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je, ni sahihi dereva wa gari kuegesha gari kwenye njia ya watembea kwa miguu?

+

Hapana, si sahihi gari kuegeshwa kwenye njia ya watembeao kwa miguu.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je, ni sahihi kuweka alama za barabarani mahali ambapo dereva wa chombo cha usafiri au mtumiaji yeyote wa barabara hawezi kuona?

+

Hapana, si sahihi kabisa kuweka alama za barabarani mahali ambapo dereva au mtumiaji yeyote wa barabara hawezi kuona. Hii ni kwasababu zinatakiwa zionekane ili zimpe maelekezo, taarifa au amri mtumiaji wa barabara husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je, ni sahihi kwa mujibu wa sheria wananchi kumpiga mtu aliyesababisha ajali barabarani?

+

Hapana, si sahihi kisheria wananchi kumpiga wala kumpa adhabu mtu yeyote kwa kusababisha ajali kwani inakuwa ni kujichukulia hatua mkononi ambayo ni kinyume na sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je, kwa maoni yako ni sahihi kujenga uwanja wa mpira karibu zaidi na barabara?

+

Hapana, si sahihi kujenga uwanja wa mpira karibu zaidi na barabara kwani ni rahisi watu kupata ajali hasa watoto wakiwa kwenye michezo.

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Je, ni sahihi kwa mujibu wa sheria kumbeba mtoto wa chini ya umri wa miaka saba kwenye baiskeli?

+

Hapana, si sahihi kwa mujibu wa sheria kumbeba mtoto mwenye chini ya umri wa miaka saba kwenye baiskeli.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Kwa mujibu wa Sheria, mtu yeyote ana wajibu wa kuendesha gari kwa makini barabarani na kwa kujali watu wengine. Je, kuna umuhimu gani?

+

Hii huwafanya madereva wa magari na watu wote wanaoendesha vyombo vya moto kuwa makini na kutokuendesha vyombo hivyo kwa uzembe na hatimaye kusababisha ajali. Hii pia huwafanya watumiaji wengine wa barabara kuwa salama na kujiamini wakati wanapotumia barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Taja rangi mbili za taa za barabarani na eleza maana ya kila moja katika suala zima la usalama barabarani.

+

i. Kijani; hii kazi yake ni kumruhusu mtumiaji wa barabara kuvuka au kuendelea na safari ii. Nyekundu; hii kazi yake ni kumwelekeza mtumiaji wa barabara asimame ili watumiaji wengine wa barabara wapite kwanza

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je, ni wastani gani wa spidi ambao dereva anapaswa kuendesha hasa akiwa kwenye maeneo ya makazi ya watu?

+

Ikiwa ni kwenye makazi ya watu, dereva anatakiwa kuendesha kwa wastani wa spidi ya km 50 kwa saa hata kama eneo hilo halina alama za barabarani zinazoelezea juu ya wastani wa spidi wa kuendesha.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Sheria ya usalama barabarani imeelekeza kuwa ni marufuku kwa dereva au kondakta ambae anasafiri kwenye usafiri wa umma kuzidisha abiria kulingana na uwezo wa gari kwenye safari zote ambazo zinazidi kilomita mia moja (100)

+

Imekuwa ikizoeleka magari mengi kuzidisha abiria tofauti na maelekezo ya gari husika. Je, sheria inasemaje kuhusiana na kuzidisha abiria tofauti na maelekezo ya gari?

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Kuna Wizara nyingi za Serikali nchini Tanzania. Je, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liko chini ya Wizara gani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.?

+

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Je, unadhani ni sababu zipi zinaweza kumfanya askari asimamishe gari lolote?

+

Kama ana sababu za kuamini kuwa gari au chombo hicho cha usafiri hakiko katika hali nzuri kufanya kazi husika, kama uendeshaji wa chombo hicho unaweza kuhatarisha maisha ya mtu au watu, kama gari au chombo hicho kimezidisha mzigo au kimebeba mzigo katika hali ambayo inaweza kusababisha hatari kwa mtu au watu.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Sheria inamtaka dereva aliyesababisha ajali kutoa taarifa kituo cha polisi ndani ya masaa kumi na mbili baada ya kutokea kwa ajali. Je, unadhani ni kwa mazingira gani ambapo dereva anaweza kutokutoa taarifa hiyo ndani ya muda sahihi na asikutwe na hatia?

+

Kama kwa mfano, dereva huyo hawezi kutoa taarifa kutokana na maumivu makubwa aliyoyapata na yeye kwenye ajali, kama hakuwa na kifaa chochote cha mawasiliano na kituo cha polisi kipo mbali sana au kutokana na sababu zozote zile ambazo zitaonekana za msingi.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Je, zipi ni kazi za Baraza linalohusika na mambo ya usalama barabarani hapa Tanzania Bara?

+

Kazi za Baraza hilo ni pamoja na kuhamasisha tafiti kuhusu vyanzo vya ajali, kutoa mapendekezo ya namna ya kukabili vyanzo vya ajali, kushauri mamlaka husika kuchukua hatua stahiki, kutoa mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani, kutoa hamasa na mafunzo kwa watumiaji mbalimbali wa barabara kupitia vyombo vya habari na njia mbalimbali na kadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Je, ni vitu gani huzingatiwa kabla ya kumpa leseni ya dereva aliyekuwa anajifunza kuendesha (dereva mwanafunzi)?

+

Kuangalia kama mwombaji wa leseni ana uwezo mzuri wa kuendesha gari la daraja aliloomba kupatiwa leseni pamoja na kama mwombaji anazijua kanuni na taratibu zote za usalama barabarani ikiwemo Sheria ya Usalama Barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Unadhani kwa maoni yako kwanini ni muhimu kumzuia mtu aliyelewa pombe kuendesha chombo cha moto?

+

Kwasababu mtu akiwa amelewa pombe si rahisi kuwa na uwezo wa kuongoza vizuri chombo hicho na kufuata kanuni za usalama barabarani kutokana na kupungua kwa uwezo wa fahamu yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Mtumiaji wa chombo cha moto anao wajibu gani endapo atafika katika eneo la kuvukia watembea kwa miguu?

+

Kwenye eneo la watembea kwa miguu dereva wa chombo cha moto ana wajibu wa kusimama na kuwaacha watu wapite. Pia, dereva anao wajibu wa kusimama umbali wa mita tano (5) kabla ya alama za pundamilia ambapo ni sehemu maalumu ya kuvuka kwa watembea kwa miguu wa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, magari ya dharula yanatakiwa kuwa na vitu gani viwili vya msingi kwa ajili ya kutambulika kuwa ni magari ya dharula ama vikiwa kwa pamoja au kimojawapo?

+

Magari ya dharula yanatakiwa kuwa na ving\'ora au taa inayoonekana na yenye rangi iliyotangazwa na Waziri mwenye dhamana. Gari moja la dharula linaweza kuwa na vyote hivi au kimojawapo ilimradi tu litambulike kuwa ni gari la dharula.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Kwa mujibu wa Sheria, magari ya dharula yanaruhusiwa kutotii baadhi ya kanuni za usalama barabarani kama vile kutotii kiwango cha spidi, kusimamisha magari sehemu yoyote, kutosimama sehemu yoyote na kadhalika. Magari hayo ni kama yafuatayo:

+

Magari ya polisi, magari ya Jeshi la zimamoto na uokoaji, magari ya wagonjwa (ambulance), magari ya jeshi la wananchi na mengine ambayo huweza kutangazwa na Waziri mwenye dhamana.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je, sheria inasemaje kuhusu magari ya usafiri wa umma kuzidisha idadi ya abiria wanaotakiwa kwenye gari husika hususani kama ni ndani ya kilomita mia moja?

+

Magari ya usafiri wa umma yanaruhusiwa kuzidisha idadi ya abiria kama gari husika linasafiri ndani ya kilomita mia moja tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Je, mama mwenye mtoto wa umri wa miaka miwili anaruhusiwa kuendesha gari akiwa na mtoto huyo karibu yake?

+

Mama au mtu yeyote mwenye mtoto mdogo haruhusiwi kuendesha gari akiwa yuko na mtoto huyo karibu sana kwani huweza kumpotezea au kumpunguzia umakini katika kuendesha gari au chombo cha moto.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Je, mtu mwenye leseni ya kigeni (yaani kutoka nje ya nchi) anaruhusiwa kutumia leseni hiyo kwa muda gani kuendesha gari kwa mara ya kwanza nchini Tanzania?

+

Mtu mwenye leseni ya kigeni anaruhusiwa kuitumia kwa miezi sita tu baada ya kufika Tanzania kwa mara ya kwanza.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je, nani mwenye wajibu kutoa leseni za udereva kwa watu wenye sifa hapa nchini?

+

Mtu mwenye wajibu wa kutoa leseni kwa watu wenye sifa na waliofanya mambo hayo ni Msajili wa Magari.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, nani anawajibika kulipa fidia na gharama zote zinazotokana na ajali iliyosababishwa na mtu ambaye alikuwa anaendesha gari ambalo halijakatiwa Bima?

+

Mtu yeyote anayesababisha ajali akiwa anaendesha gari ambalo halijakatiwa Bima anawajibika yeye mwenyewe kulipa fidia na gharama zote zitokanazo na ajali hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, mtu yeyote anayehitaji kuchunga wanyama zaidi ya hamsini anahitaji kuwa na nini kwa mujibu wa sheria?

+

Mtu yeyote anayetaka kuchunga wanyama zaidi ya hamsini kwenye barabara yoyote anahitaji kuwa na kibali cha polisi.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Kwa mujibu wa sheria, kila chombo cha moto kinapaswa kufanyiwa usajili. Je, ni nani ana wajibu wa kufanya maombi ya usajili huo?

+

Mwenye wajibu wa kufanya maombi ya usajili wa chombo cha moto kwa mujibu wa sheria ni mmiliki wa chombo husika mwenyewe.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, askari ana mamlaka ya kumhoji dereva kuhusu jina lake pamoja na anwani yake?

+

Ndiyo, askari ana mamlaka hayo ilimradi tu awe na sababu maalum.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je, unadhani madereva wa mabasi yaendayo haraka (magari ya mwendokasi) katika jiji la Dar es Salaam yana wajibu wa kutii kanuni zozote za usalama barabarani?

+

Ndiyo, madereva wa mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) pia wana wajibu wa kutii kanuni za usalama barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Je, mtu yeyote ana haki ya kwenda kwa Msajili wa Magari na kuomba kupatiwa na kukagua rejesta ya magari?

+

Ndiyo, ni haki ya kila raia kuomba na kupatiwa rejesta ya magari kwa ajili ya ukaguzi wowote.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, ni kosa kwa mujibu wa Sheria kusimamisha gari barabarani bila sababu ya msingi na bila kujali watumiaji wengine wa barabara?

+

Ndiyo, ni kosa kisheria kusimamisha gari barabarani bila kujali watumiaji wengine wa barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je, ni kosa kwa abiria kupanda pikipiki ambayo tayari imebeba abiria mwingine?

+

Ndiyo, ni kosa kisheria kwa abiria kupanda pikipiki ambayo tayari imebeba abiria mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, ni kosa la jinai kumsababishia maumivu ya mwili au kifo mtu mwingine kwa kuendesha pikipiki au baiskeli?

+

Ndiyo, ni kosa la jinai kumsababishia maumivu au kifo mtu mwingine kutokana na kuendesha pikipiki au baiskeli kwa uzembe.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je, dereva ana wajibu kutoa leseni yake kwa askari anapoamriwa kufanya hivyo?

+

Ndiyo, ni wajibu wa dereva kutoa leseni yake kwa askari anapoamriwa kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, chombo cha moto kinachotumiwa na dereva mwanafunzi barabarani kwa ajili ya kujifunzia kinahitaji kuwekwa alama kuonesha kuwa kinatumiwa na dereva mwanafunzi?

+

Ndiyo, Sheria inaelekeza kuwa chombo chochote cha moto kinachotumiwa na dereva mwanafunzi kwa ajili ya kujifunzia kinatakiwa kuwa na alama kuonesha hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, wanafunzi wakiwa wanafanya mazoezi ya kukimbia barabarani wana wajibu wa kutii Sheria ya Usalama Barabarani?

+

Ndiyo, wanafunzi wana wajibu wa kutii Sheria ya Usalama Barabarani wanapokuwa wanafanya mazoezi ya kukimbia barabarani. Wanafunzi hao, wakiwa wanakimbia kwa pamoja wanatakiwa mmoja wao kwenda mbele yao katika umbali wa kawaida na akiwa na bendera au alama yoyote ya kuwajulisha madereva wa magari mbele juu ya kinachoendelea.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je, Waziri mwenye dhamana ya mambo ya usalama barabarani ana mamlaka ya kutoa tamko linalozuia baadhi ya aina za magari au vyombo vya moto kutotumia barabara fulani kwa wakati fulani?

+

Ndiyo, Waziri mwenye dhamana ana mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Kwa ufupi, eleza maana ya sheria ya usalama barabarani.

+

Ni kanuni na taratibu ambazo zimewekwa kwa ajili ya watumiaji wa barabara ili kufanya matumizi ya barabara kuwa na tija na manufaa.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, Sheria inasemaje kuhusu watu walioko nje ya gari kurusha mawe au vitu vyovyote vinavyoweza kumuumiza mtu yeyote akiwa kwenye gari?

+

Ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kurusha mawe au vitu vyovyote vinavyoweza kumuumiza mtu akiwa kwenye gari.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je, Sheria inasemaje kuhusu mtu fulani kuchukua gari au chombo cha usafiri cha mtu na kukiendesha au kujaribu kukiendesha bila ridhaa ya mmiliki halali?

+

Ni kosa la jinai mtu kuchukua gari au chombo chochote cha usafiri na kukitumia bila ridhaa au idhini ya mmiliki halali.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, si kosa kwa mujibu wa Sheria mtu kuweka vitu barabarani vinavyoweza kusababisha pancha kwa magari na vyombo vyote vya usafiri?

+

Ni kosa la jinai mtu kuweka vitu vyovyote barabarani ambavyo huweza kusababisha uharibifu wa aina yoyote kwenye gari au chombo chochote cha usafiri kama vile pikipiki na baiskeli.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, Sheria inasemaje kuhusu mtu kubadilisha namba za usajili za gari lake?

+

Ni kosa la jinai mtu yeyote kubadili namba za usajili za gari lolote baada ya kufanyiwa usajili na mamlaka husika kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Unadhani ni kwanini magari ya dharula yanaruhusiwa kutotii baadhi ya kanuni na taratibu za usalama barabarani?

+

Ni kwasababu magari hayo yanakuwa yanawahi kuokoa maisha ya watu, kushughulikia matukio ya dharula kama vile kuzima moto na kadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Ni kwanini inashauriwa mtu asivuke barabara mbele ya magari ya dharula yenye ving\'ora na vimulimuli.

+

Ni kwasababu ni rahisi kumgonga mtu kwani magari ya dharula mara nyingi hayafuati Sheria ya Usalama Barabarani. Hivyo, inabidi mtu awe makini kuhakikisha anachukua hatua mapema na kutovuka mbele ya magari hayo akiamini kwamba lazima yatatii kanuni muda wote.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Unaelewa nini kuhusu \"Leseni halali ya dereva mwanafunzi\"?

+

Ni leseni ya uendeshaji anayepatiwa mtu anayejifunza udereva.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je, ni sawa kwa dereva wa chombo cha moto kuendesha huku akiwa anaongea na simu?

+

Ni marufuku kwa dereva wa chombo chochote cha moto kuendesha huku akiwa anaongea na simu kwani anaweza sababisha ajali.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Unadhani kwa maoni yako kwanini ni muhimu kufanya usajili wa magari na vyombo vyote vya moto?

+

Ni muhimu kufanya usajili wa magari na vyombo vyote vya moto kwani husaidia kutambua wamiliki wa vyombo hivyo, kurahisisha ulipaji wa kodi na kuongeza mapato ya nchi na hurahisisha upatikanaji wa taarifa wakati wa upelelezi baada ya matukio ya kijinai.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Kwa mujibu wa sheria, gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi linatakiwa kuwa na alama inayoonesha kuwa gari hilo linaendeshwa na dereva mwanafunzi (yaani dereva anayejifunza). Kwanini jambo hili ni muhimu katika suala zima la usalama barabarani?

+

Ni muhimu kuweka alama kwenye gari linaloendeshwa na dereva mwanafunzi ili kuwafanya watumiaji wengine wa barabara kama vile madereva wa magari mengine kuwa makini kwani dereva anajifunza na wakati wowote anaweza kushindwa kuongoza vizuri gari hilo au kushindwa kufuata baadhi ya kanuni za barabarani na hatimaye kusababisha ajali.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Nini umuhimu wa kuwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani?

+

Ni muhimu sana kuwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwani husaidia sana katika suala zima la kutii Sheria ya Usalama Barabarani na hivyo kupunguza ajali mbalimbali zinazoweza kutokea kwa watumiaji wa barabara. Askari wana jukumu muhimu sana barabarani katika kuhakikisha upunguaji au uondoaji wa ajali mbalimbali barabarani.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Sheria inasema nini kuhusu matumizi ya taa kwenye vyombo vya moto?

+

Sheria imeelekeza kuwa ni lazima kwa mtumiaji wa chombo cha moto kuwasha taa kuanzia nusu saa kabla ya jua kuchwa hadi kuchomoza, au mchana ambapo ni vigumu kwa dereva kuona ikiwa kuna ukungu, au mvua kubwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Sheria inasema nini juu ya mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano kukaa siti ya mbele kwenye gari?

+

Sheria imeweka katazo kuwa mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano haruhusiwi kukaa siti ya mbele kwenye gari akiwa peke yake au na mtu mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Ni sawa kwa mtu asiye na leseni kuendesha chombo cha moto barabarani?

+

Sheria imeweka katazo kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto bila ya kuwa na leseni ya udereva ambayo bado ipo kwenye matumizi.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je, ni nani hudhaniwa kuwa mmiliki halali wa gari kati ya dereva wa gari na mtu ambaye jina lake linaonekana katika rejesta ya magari?

+

Sheria inaelekeza kuwa atakayedhaniwa kuwa mmiliki halali wa gari ni yule ambaye jina lake linaonekana katika rejesta ya magari. Kwahiyo dereva hawezi kudhaniwa kuwa mmiliki wa gari mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Je, mtu anayejifunza udereva (dereva mwanafunzi) anaweza kuendesha chombo cha moto akiwa peke yake barabarani?

+

Sheria inamtaka dereva mwanafunzi awe anaongozwa na mwalimu wa udereva aliyesajiliwa anayefanya kazi kwenye shule ya udereva iliyothibitishwa. Hivyo, dereva mwanafunzi hatakiwi kuendesha chombo cha moto barabarani akiwa peke yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Kwa mujibu wa Sheria, askari polisi anaweza kumtaka dereva yeyote wa gari kuchukuliwa vipimo vya damu ili kugundua kiwango cha pombe mwilini make akiwa na sababu ya kuamini kuwa dereva huyo amekunywa pombe. Je, dereva anayetakiwa na polisi kuchukuliwa vipimo ana haki ya kukataa kuchukuliwa vipimo?

+

Sheria inasema kuwa ni kosa la jinai kwa dereva yeyote anayemkatalia askari polisi kuchukuliwa vipimo baada ya kuhisiwa kuwa amekunywa pombe.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Je, sheria inasemaje kuhusu mtu kuendesha barabarani chombo cha moto ambacho baadhi ya sehemu zake kama vile magurudumu au injini zina hitilafu?

+

Sheria inasema kuwa ni kosa na mtu yeyote haruhusiwi kuendesha chombo cha moto barabarani ambacho kina hitilafu katika sehemu zake kama vile injini na magurudumu.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Kwa maoni yako, mtoto chini ya umri wa miaka 5 anaruhusiwa kupakizwa kwenye pikipiki?

+

Sheria ya usalama barabarani imeelekeza kuwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano haruhusiwi kupakizwa kwenye pikipiki mwenyewe bila usaidizi na uwepo wa mtu mzima.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Je, ni sawa kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu mpaka mitano kulipa nauli kwenye usafiri wa umma kama vile daladala, bajaji nk.?

+

Sheria ya usalama barabarani imeeleza kuwa mtoto kati ya umri wa miaka mitatu na mitano hatakiwi kulipa nauli kwenye vyombo vya usafiri wa umma.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Je, ni sawa kwa mtumiaji wa chombo cha moto kama vile gari, pikipiki, bajaji Kwenda kujaza mafuta kwenye vituo vya mafuta na abiria wakiwa wamepanda?

+

Sheria ya usalama barabarani imeweka katazo kwa madereva wa vyombo vya moto kujaza mafuta huku abiria wakiwa ndani ya chombo hicho cha moto.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Kwa maoni yako, ni sawa kwa msafiri kusafiri pasipo kufunga mkanda?

+

Sheria ya usalama barabarani inamtaka kila mtu anaesafiri kwa kutumia gari kufunga mkanda na endapo atakaidi agizo hilo atakuwa ametenda kosa kisheria,

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Sheria imeweka katazo kuwa mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano haruhusiwi kukaa siti ya mbele kwenye gari akiwa peke yake au na mtu mwingine.

+

Sheria ya usalama barabarani inamtaka kila mtu anaesafiri kwa kutumia gari kufunga mkanda na endapo atakaidi agizo hilo atakuwa ametenda kosa kisheria,

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Sheria inasemaje kuhusu mtu anayeendesha pikipiki pasipo kuvaa kofia ngumu?

+

Sheria ya usalama barabarani, imeweka wazi kuwa ni kosa endapo mwendesha pikipiki ataendesha chombo hicho pasipo kuvaa kofia ngumu kwa ajili ya usalama. Kofia hiyo inatakiwa iwe imefungwa vizuri chini ya kidevu cha dereva.

Sheria Kiganjani
Learn More
100

Je, ni mambo gani yamekatazwa kwa dereva kuyafanya ili kulinda usalama wa watumiaji wa barabara?

+

Yapo mambo mengi ambayo yamekatazwa kwa dereva kuyafanya kama vile, kuendesha wakati dereva akiwa mgonjwa, kuendesha wakati dereva amechoka, kuendesha wakati dereva amelewa.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand