Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je, nani hutoa leseni kwa watoa huduma ya mawasiliano hapa nchini?

+

Anayetoa leseni kwa watoa huduma ya mawasiliano hapa nchini ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, sheria inazungumziaje suala la mtu kutuma bidhaa yoyote ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watu kwa njia ya posta?

+

Hairuhusiwi kisheria kutuma bidhaa yoyote ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watu wakati wa usafirishaji kwa njia ya posta.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, Sheria inasemaje kuhusu suala la kutuma mzigo wenye madawa ya kulevya kama vile bangi na mirungi kwa njia ya posta kwenda nchi nyingine?

+

Hairuhusiwi kutuma madawa ya kulevya kwa njia ya posta isipokuwa kama yameruhusiwa kisheria na mamlaka zinazohusika na uchunguzi wa kisayansi nchini.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina mamlaka ya kusimamia maudhui ya redio na televisheni kwa pande zote mbili za muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar?

+

Hapana, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inasimamia maudhui ya redio na televisheni kwa Tanzania Bara tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, Wakala wa mtoa huduma (mtandao wa mawasiliano) anawajibika mwenyewe kwa makosa aliyoyafanya wakati anasajili laini ya mteja?

+

Hapana, mtoa huduma ndiye anapaswa kuwajibika kwa mujibu wa sheria ilimradi tu kosa lile limefanyika wakati wakala akitenda kazi yake ya kusajili laini na kosa lenyewe linahusiana na suala la kusajili laini kwa ajili ya mteja.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, mtoto mwenye umri wa miaka kumi anaruhusiwa kusajiliwa laini ya simu kwa matumizi yake kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, mtoto mwenye chini ya umri wa miaka kumi na mbili (12) haruhusiwi kusajiliwa laini ya simu.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, mtu anaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kutoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki bila kupata leseni kutoka katika mamlaka husika?

+

Hapana, mtu yeyote haruhusiwi kwa mujibu wa sheria kutoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki bila kupewa leseni kutoka katika mamlaka husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je? Mtoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki (mtandao wa mawasiliano) ana wajibu wa kufungia huduma au matumizi laini yoyote ya simu iliyotolewa taarifa na mtumiaji kuwa imeibiwa.

+

Hii ni muhimu kwasababu huwazuia watu wengine wanaoweza kuiokota laini hiyo na kuitumia katika matukio ya kihalifu. Pia, hii inasaidia kujua kuwa laini fulani haiko kwenye matumizi kutokana na kupotea.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, Idara ya Uhamiaji hapa nchini Tanzania inahusikaje au inasaidiaje katika suala zima la usajili wa laini za simu?

+

Idara ya Uhamiaji husaidia kuthibitisha kuwa mteja fulani ni raia wa Tanzania na si mhamiaji kutoka nchi nyingine. Idara ya Uhamiaji pia huweka kanzidata maalumu kwa ajili ya wageni wa muda mfupi.

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, inaruhusiwa kisheria kuwa na simu ambayo laini yake imejengewa ndani?

+

JIBU: Ndiyo, sheria inatambua wazi uwepo wa laini zilizojengewa kwenye simu na ambazo zinaweza kuondolewa na kurudishwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina mamlaka ya kufuta leseni ya mtoa huduma ya mawasiliano ya posta. Je, ni sababu gani ya msingi inaweza kupelekea kufutwa kwa leseni ya mtoa huduma ya posta?

+

Leseni ya mtoa huduma ya mawasiliano ya posta inaweza kufutwa na Mamlaka kama, kwa mfano, anafanya kazi kinyume na masharti ya leseni hiyo au kinyume na masharti ya sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, sheria inasemaje kuhusu suala la mafundi au makandarasi wanaoweka na kufunga mifumo na mitandao ya mawasiliano katika majengo na kwenye miundombinu mingine kuwa na leseni kutoka katika mamlaka husika?

+

Makandarasi au mafundi hao wanatakiwa kuwa na leseni iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je, nani ana uwezo wa kuchukua hatua yoyote kama maudhui ya redio au televisheni yako kinyume na maadili ya jamii?

+

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndiyo yenye mamlaka ya kuchukua hatua kama maudhui ya redio au televisheni yako kinyume na maadili ya jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Sheria inampa mamlaka mtoa huduma kutunga na kuunda hatua za kufunga simu. Je, mtoa huduma ana wajibu gani wa msingi baada ya kutunga na kuunda hatua hizo?

+

Mtoa huduma anatakiwa kuzichapisha hatua hizo ili zijulikane kwa wateja au watumiaji wa huduma yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je, mtoa huduma ya mawasiliano ya mtandao wa simu anatakiwa kisheria kutoa huduma ya mtandao mpaka siku za jumamosi na jumapili?

+

Ndiyo, huduma ya mawasiliano ya mtandao inatakiwa kutolewa kwa siku saba za wiki zikiwemo siku za jumamosi na jumapili.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je, kampuni inaweza kumiliki laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la kampuni husika?

+

Ndiyo, kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria inaweza kumiliki laini iliyosajiliwa kwa jina lake (jina la kampuni husika).

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, leseni moja ya kutoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki inaweza kutolewa kwa kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni?

+

Ndiyo, leseni moja inaweza kutolewa kwa kampuni ilimradi tu imesajiliwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je, mtoa huduma ya posta anawajibika kwa upotevu wa mizigo au barua zinazotumwa na wateja wake?

+

Ndiyo, mtoa huduma ya posta anawajibika kwa upotevu wa mizigo au barua zilizotumwa na wateja wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Je, inaruhusiwa kisheria kuwa na simu ambayo laini yake imejengewa ndani?

+

Ndiyo, sheria inatambua wazi uwepo wa laini zilizojengewa kwenye simu na ambazo zinaweza kuondolewa na kurudishwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Je, wakala wa mtoa huduma anayesajili laini kwa ajili ya wateja kwa niaba ya mtoa huduma ana wajibu wa kutunza siri za mteja huyo?

+

Ndiyo, wakala ana wajibu wa kutunza siri za mteja.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Je, watu wenye ulemavu wana haki ya kutumia vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki?

+

Ndiyo, watu wenye ulemavu wana haki ya kutumia vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kama watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je, ni sahihi kwa ofisi ya posta kutofikisha kwa makusudi barua iliyotumwa kwa mlengwa?

+

Ni kosa kwa posta kutofikisha kwa makusudi barua iliyotumwa kwa mlengwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Baadhi ya watu huweza kuandika kwenye kuta, madirisha au milango ya nyumba zao maneno ambayo yanaweza kuwafanya watu kuamini kuwa eneo hilo hutoa huduma ya posta. Mfano wa maneno hayo huweza kuwa \"OFISI YA POSTA\". Je, Sheria inalizungumziaje hili?

+

Ni kosa la jinai kuandika maneno ambayo yanaweza kuufanya umma uamini au kudhani kuwa eneo hilo kuna huduma halali ya posta wakati si kweli.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je, Sheria inasemaje kuhusu mtu kukataa kuwasilisha mzigo au kifurushi chochote katika mamlaka husika kwa mujibu wa sheria kama vile polisi kwa ajili ya ukaguzi baada ya kuamriwa kufanya hivyo?

+

Ni kosa la jinai mtu yeyote kukataa kuwasilisha mzigo au kifurushi kwa ajili ya ukaguzi baada ya kuombwa au kuamriwa kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, nani mwenye mamlaka ya kutoa leseni ya kutoa huduma ya mawasiliano ya posta kwa upande wa Zanzibar?

+

Ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwani ndiyo yenye mamlaka hayo kwa Tanzania Bara na Zanzibar (ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Kuna wizara nyingi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ni wizara moja tu yenye dhamana ya mambo ya mawasiliano ya kielektroniki na posta. Je, ni wizara gani?

+

Ni Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Nini maana na jukumu la Tume ya Utangazaji ya Zanzibar?

+

Tume ya Utangazaji ya Zanzibar ni chombo kinachoshughulikia maudhui ya redio na televisheni kwa upande wa Zanzibar.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Je, ni lini au kwa mazingira gani barua iliyotumwa kwa njia ya posta inadhaniwa kuwa imeshamfikia mlengwa?

+

Barua iliyotumwa kwa njia ya posta inadhaniwa kuwa imeshamfikia mlemgwa kama imeshawekwa kwenye sanduku binafsi la mlengwa, kama imefikishwa nyumbani au ofisini kwa mlengwa, kama amepewa mlengwa mwenyewe moja kwa moja au mwakilishi wake au mtu kupitia kwa mtu yeyote aliyethibitishwa kupokea barua hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, sheria inasemaje kuhusu mtoa huduma mwenye leseni kufanya shughuli za utoaji wa huduma ya mawasiliano ambazo ni kinyume na masharti ya leseni aliyopewa?

+

Hairuhusiwi kwa mtoa huduma ya mawasiliano mwenye leseni kufanya shughuli yoyote ya mawasiliano ambayo iko kinyume na masharti ya leseni aliyopewa.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Redio na televisheni kama vyombo vya habari vina uhuru wa kutoa habari na kurusha vipindi mbalimbali. Je, sheria inasemaje kuhusu televisheni au redio kurusha vipindi ambavyo vinahimiza unyanyasaji wa watoto?

+

Hairuhusiwi televisheni au redio kurusha vipindi ambavyo vina maudhui yanayolenga kuhimiza unyanyasaji wa watoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Je, ni haki ya mtu yeyote kwenda katika ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kuomba na kupewa taarifa za mteja wa mtoa huduma yeyote?

+

Hapana, hakuna haki hiyo kisheria kwasababu Mamlaka pia ina wajibu wa kutunza siri za taarifa za watumiaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Je, magazeti kama vile \"Mwanaspoti\" na \"Mwananchi\" ni moja ya huduma za mawasiliano ya kielektroniki kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta?

+

Hapana, magazeti si huduma za mawasiliano ya kielektroniki kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Sheria inaelekeza kuwa maombi ya leseni yanapofanywa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina wajibu wa kuchapisha maombi hayo kwenye gazeti ili kuwakaribisha watu kutoa maoni. Je, matakwa haya ya kisheria yanatumika hata pale leseni inayoombwa ni ya kutumika kwa muda ulioko chini ya miaka mitano?

+

Hapana, matakwa haya ni kwa maombi ya leseni ambazo ni za zaidi ya miaka mitano na si chini ya hapo.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je, mteja anatakiwa kulipa gharama yoyote kwa mujibu wa sheria katika zoezi la usajili wa laini kibayometriki kutumia kitambulisho cha taifa?

+

Hapana, mfumo wa kibayometriki katika usajili wa laini hautakiwi kulipiwa gharama yoyote kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Kwa mujibu wa sheria, mtu yeyote anayetaka kutoa huduma ya mawasiliano kwa njia ya posta anatakiwa kuomba leseni kutoka katika Mamlaka husika. Je, maombi ya leseni yanaweza kufanyika kwa njia ya simu ya maongezi?

+

Hapana, Sheria inaelekeza wazi kabisa kuwa maombi yote ya leseni ya kutoa huduma ya mawasiliano kwa njia ya posta yanatakiwa kufanywa kwa njia ya maandishi tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, ni sahihi laini ya simu ya mtu binafsi kusajiliwa kwa jina tofauti na ambalo limeandikwa katika kitambulisho chake cha taifa?

+

Hapana, si sahihi kabisa. Sheria inaelekeza kuwa laini ya simu isajiliwe kwa jina lile lile lililoandikwa kwenye kitambulisho cha taifa.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, ni sahihi kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii kama vile \"Facebook\" na \"Instagram\" zenye lengo la kiuchochezi?

+

Hapana, si sahihi kuchapisha taarifa za uongo na zenye lengo la kiuchochezi katika mitandao ya kijamii kwani ni kinyume na sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je, Kiongozi wa dini ana mamlaka ya kupewa taarifa za mtumiaji yeyote wa huduma ya mawasiliano ilimradi tu ni mfuasi wa dini yake ili kufanya uchunguzi wa mwenendo wake wa kidini?

+

Hapana. Kiongozi wa dini hana mamlaka yoyote kupewa taarifa za mtumiaji wa huduma ya mawasiliano. Kumpa kiongozi wa dini taarifa za mteja ni kinyume na haki ya usiri na faragha kwa mteja.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Hatua gani za msingi zinazohusika baada ya laini ya simu kuibwa, kupotea au kuharibika.

+

Hatua ya kwanza ni mtumiaji wa laini hiyo ya simu kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake (mtandao wa mawasiliano) kuwa laini yake imepotea, imeibwa au imeharibika. Hatua ya pili ni mtoa huduma (mtandao wa mawasiliano) kuifunga laini husika (kuifungua huduma zote).

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je, huduma ya usajili wa laini kibayometriki kwa kutumia kitambulisho cha taifa inapatikana wapi?

+

Huduma ya kusajili laini kibayometriki inapatikana katika maduka ya watoa huduma za mawasiliano pamoja na mawakala wao waliothibitishwa kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je, mtandao wa simu unatakiwa kutoa huduma ya mawasiliano (huduma ya mtandao) kwa masaa mangapi kwa siku kisheria?

+

Huduma ya mawasiliano ya mtandao inatakiwa kutolewa kwa masaa ishirini na nne kwa siku (muda wote).

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je, ni taasisi au huduma gani zinatakiwa kupigiwa simu bure (yaani bila malipo) kwa mujibu wa sheria kwa kutumia mtandao wowote wa mawasiliano bila malipo yoyote?

+

i. Huduma za dharula ii. Huduma kwa wateja iii. Udhibiti wa makosa ya jinai iv. Huduma za misaada kwa watoto v. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vi. Huduma za magari ya wagonjwa (ambulance services) vii. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) viii.Msaada wa kiafya

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je, mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroniki ana haki gani kwa mujibu wa sheria?

+

i. Mtumiaji ana haki ya usiri (faragha). Taarifa zake zisisambazwe na mtoa huduma kwa watu wengine bila ridhaa yake. ii. Mtumiaji ana haki ya kuelimishwa (kupata elimu) juu ya huduma za mawasiliano zinazotolewa na mtoa huduma husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Licha ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroniki kuwa na haki mbalimbali kwa mujibu wa sheria, watumiaji hao pia wana wajibu kisheria katika suala zima la matumizi ya huduma za mawasiliano ya kielektroniki kama ifuatavyo:

+

i. Mtumiaji ana wajibu wa kutii sheria za nchi kama vile kutoingilia uhuru na haki za watumiaji wengine, kutotumia huduma za mawasiliano kama nyenzo ya kufanya uhalifu na kufanya mawasiliano yenye maudhui maovu. ii. Mtumiaji ana wajibu wa kulipia huduma za mawasiliano popote pale inapohitajika. iii. Mtumiaji wa huduma za mawasiliano pia ana wajibu wa kuhakikisha kuwa matumizi yake ya huduma hizo hayaathiri mazingira kwa ujumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Je, Sheria inasemaje kuhusu matumizi ya laini ya simu ambayo haijasajiliwa na mtoa huduma kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha mteja?

+

Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Kuhusu Usajili wa Laini za Simu, 2023 zinasema kuwa ni kosa la jinai kutumia laini ya simu ambayo haijafanyiwa usajili na mtoa huduma kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha mteja.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Je, upi ni wajibu wa kwanza wa mtu baada ya kupoteza simu au laini ya simu?

+

Kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je, ni kigezo gani cha msingi sana ambacho unadhani huzingatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kabla ya kutoa leseni kwa mwombaji wa leseni ya kutoa huduma ya posta?

+

Kwa mujibu wa sheria, Mamlaka inaweza kutoa leseni kwa mwombaji wa leseni anayetaka kutoa huduma ya posta kama tu imejiridhisha kuwa taarifa zilizotolewa na mwombaji zinatosha na zinakidhi suala zima la uendeshaji wa huduma inayoombewa leseni.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Unaelewa nini juu ya \"malalamiko ya huduma za mawasiliano\"?

+

Malalamiko ya huduma za mawasiliano ni hoja ambazo zinawasilishwa na mhusika kwenye ngazi husika dhidi ya upande mwingine (ambapo kikawaida huwa kati ya mteja na mtoa huduma) kutokana na kasoro au kutokukamilika kwa huduma au bidhaa husika katika suala zima la mawasiliano ya kielektroniki na posta kama alivyotarajia.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je, baada ya kupokea maombi ya leseni kutoka kwa mwombaji anayetaka kutoa huduma ya posta, Mamlaka inatakiwa kutoa maamuzi ya kutoa leseni au kukataa maombi ndani ya siku ngapi kisheria?

+

Mamlaka inatakiwa kutoa maamuzi ya kukubali au kukataa maombi ndani ya siku sitini (60).

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Aina gani za leseni ambazo hutolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

+

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania hutoa leseni kama vile leseni ya kutoa huduma ya mawasiliano na leseni ya maudhui kwa ajili ya redio na televisheni.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Kwa mujibu wa Sheria, mtu mwenye leseni ya kutoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania anaweza kuiuza kwa mtu mwingine. Je, nini kinahitajika cha msingi kabla ya kufanya hivyo?

+

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inabidi itoe kwanza idhini hiyo. Bila idhini ya Mamlaka tajwa, mwenye leseni haruhusiwi kuiuza kwa mtu mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Onyesha ni kwa namna gani Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inahusika katika suala zima la mawasiliano ya kielektroniki hapa Tanzania.

+

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inahusika sana katika suala zima la mawasiliano ya kielektroniki hapa nchini kwani mamlaka hii ndiyo inayotoa vitambulisho vya taifa au namba za vitambulisho vya taifa ambazo ni za lazima ili mtu aweze kusajiliwa laini ya simu. Hivyo, bila Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kutimiza wajibu wake ipasavyo, watu wanaweza kukosa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki kwani kusajili laini ni lazima kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha mfumo mpya wa anwani za makazi na postikodi. Je, mfumo huu ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania una manufaa gani katika sekta ya mawasiliano kwa njia ya posta hapa nchini?

+

Mfumo huu wa anwani na postikodi unatambulisha mhusika alipo katika kijiji/mtaa, kata, wilaya na mkoa husika na hatimaye inaongeza ufanisi katika uchambuzi, usafirishaji na usambazaji wa barua kwa njia ya posta.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Je, pale mtumiaji wa huduma anapokuwa na malalamiko ya huduma zitolewazo na mtoa huduma wake anatakiwa kufanya nini kabla ya kuwasilisha malalamiko yake katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania?

+

Mlalamikaji anatakiwa kwanza kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake ili kuona kama lalamiko hilo linaweza kupatiwa suluhu na mtoa huduma mwenyewe ndani ya muda mwafaka.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Taja wadau wanne wa sekta ya mawasiliano hapa nchini Tanzania.

+

Moja, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (ambaye ndiye msimamizi na mdhibiti) Mbili, watoa huduma (hawa ni watu au makampuni ambayo yamethibitishwa kutoa huduma ya mawasiliano) Tatu, watumiaji wa huduma (hawa ni wanaotumia huduma za mawasiliano) Nne, Serikali (Serikali inahusika kwa kutunga sera, sheria na kanuni zinazoongoza sekta pamoja na kukusanya kodi zinazotokana na shughuli za sekta kwa maendeleo ya nchi na watu wake)

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, sheria inasemaje kuhusu mitandao ya mawasiliano kupanga bei za huduma zao ambazo ni za kibaguzi au zinaonesha ubaguzi baina ya watumiaji wa mtandao mmoja wa simu?

+

Mtandao wa simu hautakiwi kupanga bei za huduma zake ambazo zina ubaguzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Je, ni kwa mazingira gani mtoa huduma anaweza kutoa taarifa za siri za mteja?

+

Mtoa huduma anaweza kutoa siri za mteja pale ambapo imeruhusiwa na sheria, kukiwa na uchunguzi wa kosa la jinai unafanyika au kwa amri ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je, mtandao wa simu (mtoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki) ana wajibu gani baada ya kupanga bei za huduma zao na kabla ya bei hizo kuanza kutumika?

+

Mtoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki ana wajibu wa kupeleka bei hizo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania walau wiki mbili kabla ya kuanza kutumika na pia kuzichapisha bei hizo katika vyombo vya habari walau wiki moja kabla ya kuanza kutumika.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Nambari ya IMEI ni kodi ambazo huthibitisha ubora wa simu. Je, mtumiaji wa simu hapa nchini Tanzania anaweza kubonyeza namba gani ili apate IMEI ya simu yake na kuweza kuthibitisha kuwa simu yake ni bora?

+

Mtumiaji wa simu anatakiwa kubofya *#06# ili kupata IMEI ya simu.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Baadhi ya vifaa vya mawasiliano vinavyouzwa madukani vimekuwa vikilalamikiwa kutokuwa salama kwa matumizi hasa katika suala la usalama wa watumiaji kiafya. Je, nani ana wajibu kuhakikisha kuwa vifaa vyote vinavyouzwa vinakuwa salama kwa matumizi ya watumiaji?

+

Mwenye wajibu kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kuwa vifaa vinavyoingizwa dukani kwa ajili ya kuuzwa kwa watumiaji ni salama ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na mtoa huduma, mwagizaji au msambazaji wa vifaa hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je, kwa mujibu wa sheria, vifurushi au mizigo iliyotumwa kwa njia ya posta inakuwa ni mali ya nani wakati wote kabla ya kufika kwa mlengwa aliyetumiwa mzigo huo?

+

Mzigo unaendelea kuwa mali ya mtumaji (aliyetuma mzigo) wakati wote hadi pale mzigo unapofika kwa mlengwa husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kufanya miamala yoyote ya kifedha kwa kutumia simu za mkononi?

+

Ndiyo, inaruhusiwa kisheria kutumia simu za mkononi katika miamala ya kifedha.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, ombi la leseni linatakiwa kuchapishwa kwenye magazeti ya hapa nchini?

+

Ndiyo, Mamlaka ina wajibu wa kuchapisha ombi la leseni kwenye magazeti ili kukaribisha maoni ya wadau mbalimbali.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaweza kukataa maombi ya leseni ya mtu yeyote anayetaka kutoa huduma za mawasiliano. Je, Mamlaka ina wajibu wa kumtaarifu mwombaji wa leseni kuwa ombi lake limekataliwa?

+

Ndiyo, Mamlaka ina wajibu wa kumtaarifu kwa maandishi mwombaji wa leseni kuwa ombi lake limekataliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, kuna uwezekano wowote kisheria kwa Mamlaka ya Mawasiliano kubadilisha au kuboresha baadhi ya masharti yaliyoko kwenye leseni ya mtoa huduma baada ya kuwa Mamlaka ilishampa leseni yake?

+

Ndiyo, Mamlaka inaweza kubadilisha au kuboresha masharti yaliyoko kwenye leseni ya mtoa huduma.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina mamlaka yoyote kisheria kufuta leseni ya mtoa huduma ya mawasiliano ya posta wakati wowote?

+

Ndiyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina mamlaka ya kufuta leseni ya mtoa huduma ya mawasiliano ya posta wakati wowote.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Je, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaweza kusikiliza malalamiko kati ya mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za mawasiliano?

+

Ndiyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaweza kusikiliza malalamiko kati ya mtoa huduma na mteja au mtumiaji na kutoa maamuzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Mdiplomasia ni mtu ambaye yuko kwenye kazi ya kidiplomasia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, mdiplomasia anaruhusiwa kusajiliwa laini ya simu kwa jina lake?

+

Ndiyo, Mdiplomasia anaweza kusajiliwa laini ya simu kwa jina lake.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Ni kawaida katika hali ya kawaida kwa mtoa huduma ya mawasiliano kutaka kusitisha ama kwa muda mfupi au jumla utoaji wa huduma hiyo. Je, katika hali kama hii mtoa huduma ana wajibu kisheria wa kutoa taarifa kwa watumiaji wa huduma au wateja wake?

+

Ndiyo, mtoa huduma ana wajibu wa kisheria kutoa taarifa kwa watumiaji wa huduma au wateja wake pale anapotaka kusitisha huduma ya mawasiliano. Kufanya kinyume chake ni uvunjaji wa haki ya watumiaji.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, mtu ana haki ya kubadilisha mtandao wa mawasiliano wakati wowote anapotaka kufanya hivyo?

+

Ndiyo, mtu ana haki ya kubadilisha mtandao wa mawasiliano wakati wowote anaoona inafaa kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je, mtu anapotuma kifurushi kwa njia ya posta anakuwa na wajibu wa kuweka bayana kwa mtoa huduma maelezo ya vitu vilivyomo ndani ya kifurushi husika?

+

Ndiyo, mtu anayetuma kifurushi kwa njia ya posta anakuwa na wajibu kisheria kuweka bayana vitu vilivyomo ndani ya kifurushi husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaweza kukataa maombi ya mwombaji wa leseni kama, kwa mfano, mwombaji hajaambatanisha nyaraka zinazohitajika. Je, mwombaji anaweza kuleta maombi mengine baada ya maombi yake ya kwanza kukataliwa?

+

Ndiyo, mwombaji anaweza kuleta maombi mengine ilimradi tu amekamilisha vitu vyote ambavyo hakuwa navyo kwa mara ya kwanza.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, maombi ya leseni yanamtaka mtu kulipia kiasi fulani cha ada?

+

Ndiyo, mwombaji wa leseni anatakiwa kulipa kiasi fulani cha ada kama itakavyoamuliwa na Mamlaka husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Imezoeleka kuona mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki ikijipangia bei za vifurushi na huduma mbalimbali wanazotoa kwa wateja wao. Je, hii ni halali wao kupanga bei?

+

Ndiyo, ni halali kabisa. Sheria inawaruhusu watoa huduma ya mawasiliano ya kielektroniki kupanga bei za huduma zao ilimradi tu wafuate sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, ni kosa la jinai mtu kuwa na stempu feki na ambayo haijathibitishwa na Mamlaka husika kutumika katika shughuli za posta?

+

Ndiyo, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kumiliki stempu feki.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, ni kosa la jinai mtu kuwa na stempu feki na ambayo haijathibitishwa na Mamlaka husika kutumika katika shughuli za posta?

+

Ndiyo, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kumiliki stempu feki.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Imezoeleka kuona polisi wakiingia katika vituo vya redio wakifanya ukaguzi na upelelezi pale ambapo wanahisi kuwa kuna kosa lolote limefanyika linalohusiana na suala zima la mawasiliano. Je, ni sahihi kisheria polisi kuingia katika vituo vya redio na kufanya ukaguzi?

+

Ndiyo, ni sahihi polisi kufanya hivyo kwani inaruhusiwa na sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ina mamlaka ya kushughulikia mambo yote ya mawasiliano ya kielektroniki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (pande zote za muungano)?

+

Ndiyo, sheria inaelekeza kuwa Mamlaka ya Mawasiliano ina mamlaka ya kushughulikia mambo yote ya mawasiliano ya kielektroniki ndani ya Jamhuri ya Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar).

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, mmiliki au mtumiaji wa laini ya simu ana wajibu kisheria kutoa taarifa pale anapotoa laini hiyo kutumiwa na mtu mwingine?

+

Ndiyo, sheria inaelekeza kuwa mtu yeyote anayemiliki au anayetumia laini ya simu anatakiwa kutoa taarifa kwa mtoa huduma au kwa mtandao husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, kusajili kibayometriki laini za simu zinazoweza kuondolewa au zilizojengwa ndani ya simu ya mkononi ni lazima kwa mujibu wa sheria?

+

Ndiyo, Sheria inaelekeza kuwa ni lazima laini zote za simu zisajiliwe kwa njia ya kibayometriki.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Je, watoa huduma za mawasiliano ya posta wana wajibu wa kutunza siri za wateja wao?

+

Ndiyo, Sheria inaelekeza wazi kwamba watoa huduma za posta wana wajibu wa kuhakikisha kuwa hawatoi siri za wateja wao bila idhini ya wateja wao.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je, mtu mmoja anaruhusiwa kusajili zaidi ya laini moja kwa kutumia kitambulisho chake cha taifa?

+

Ndiyo, Sheria inaruhusu kusajili laini zaidi ya moja kwa kutumia kitambulisho cha mtu mmoja.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je, kuna uwezekano wa kuhuisha au kusasisha leseni ya huduma ya mawasiliano ya kielektroniki au posta baada ya muda wake kuisha?

+

Ndiyo, Sheria inatoa haki hiyo ya kuhuisha au kusasisha leseni baada ya muda wake kuisha.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Je, watumiaji wa mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na WhatsApp wana wajibu wa kutii Sheria ya Kielektroniki na Posta?

+

Ndiyo, watumiaji wa mitandao ya kijamii wana wajibu wa kutii Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta inatoa tofauti kati ya \"mtumiaji\" na \"mteja\" wa huduma au bidhaa za mawasiliano, maneno haya yanatofautianaje?

+

Neno \"Mteja\" hutumika kumtambulisha mtu ambaye ana uhusiano wa kimkataba na mtoa huduma au bidhaa za mawasiliano wakati neno \"mtumiaji\" humtambulisha mtu ambaye anatumia au anafaidika na huduma au bidhaa yenyewe. Hivyo, kuna uwezekano wa mteja kutokuwa mtumiaji wa huduma husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Je, sheria inasemaje kuhusu mtu yeyote kufungua barua iliyotumwa kwa njia ya posta bila idhini ya mtumaji au mlengwa?

+

Ni kosa kufungua barua iliyotumwa kwa njia ya posta bila idhini ya mtumaji au mlengwa isipokuwa polisi pale wanapokuwa na sababu za kuamini kuwa barua hiyo inaeleza jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria au kwa amri ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je, sheria inasemaje kuhusu mtu yeyote anayeamua kuharibu au kubomoa ofisi au jengo lolote linalotoa huduma za posta kwa makusudi?

+

Ni kosa la jinai kubomoa au kuharibu jengo au ofisi yoyote inayotoa huduma za posta kwa makusudi.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Imekuwa jambo la kawaida kwa baadhi ya wafanyabiashara kubandika mabango yao katika kuta za majengo mbalimbali mijini na hata vijijini. Je, Sheria inasemaje kuhusu watu kubandika matangazo yao ya kibiashara na yasiyo ya kibiashara katika ofisi za posta?

+

Ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mtu yeyote kubandika matangazo katika ofisi za posta bila idhini maalumu.

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Ni mamlaka gani hapa nchini Tanzania yenye wajibu wa kushughulikia mambo yote ya mawasiliano?

+

Ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Kwa maoni yako, unadhani upi ni umuhimu wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta?

+

Ni muhimu kutoa elimu kwa jamii kuhusu Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kwasababu jamii itapata kufahamu namna nzuri ya kutumia huduma ya mawasiliano ya kielektroniki na posta bila kuvunja sheria za nchi na pia wadau wote wa mawasiliano wataweza kufahamu haki na wajibu wao katika suala zima la utoaji na ufaidikaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroniki na posta hapa nchini.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Je, sheria inalizungumziaje suala la baadhi ya matapeli wanaouza laini mitaani bila kuthibitishwa na watoa huduma (yaani bila kuthibitishwa na mitandao ya mawasiliano)?

+

Sheria inaeleza wazi kuwa ni kosa la jinai kujihusisha na suala la kusajili laini bila uthibitisho halali wa mtoa huduma.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je, Sheria inasemaje kuhusu suala la televisheni na redio kuwa na vipindi vyenye maudhui yanayolenga kuidhalilisha au kuikashifu dini fulani?

+

Sheria inasema moja kwa moja kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kurusha vipindi ambavyo maudhui yake hayaoneshi ishara ya kuitenga, kuifhalilisha au kuikashifu dini yoyote ile.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Je, polisi wanaruhusiwa kufanya ukaguzi wa vifurushi au mizigo iliyotumwa kwa njia ya posta bila ridhaa ya mteja wa mtoa huduma?

+

Sheria inawaruhusu polisi kufanya ukaguzi wa vifurushi au mizigo iliyotumwa kwa njia ya posta katika kutimiza majukumu yao ya kisheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Unaelewaje maana ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta?

+

Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ni Kanuni na taratibu ambazo huongoza matumizi bora ya vifaa na vitu vinavyotumika na kuwezesha mawasiliano kwa njia ya Kielektroniki na posta.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

TEHAMA ni mojawapo ya maneno maarufu katika suala zima la mawasiliano ya kielektroniki. Nini kirefu cha TEHAMA?

+

TEHAMA ni Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Kuna umuhimu gani kusajili laini ya simu kibayometriki na kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba za kitambulisho cha taifa?

+

Umuhimu wa kusajili laini za simu kibayometriki kwa kutumia kitambulisho cha taifa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa wahalifu na matapeli mbalimbali wa mitandao ambao mara nyingi hutumia laini ambazo hazisajiliwa kwa majina yao halali. Ni rahisi kufanya upelelezi wa makosa mbalimbali ya jinai yanayofanywa kupitia njia za mawasiliano ya kielektroniki.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Je, ni nani anatakiwa kutii Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta?

+

Wadau wote wa mawasiliano ya kielektroniki na posta wana wajibu wa kutii Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. Hii ni pamoja na watumiaji, watoa huduma, Serikali pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Kuna Kitengo cha Dharura cha Kitaifa cha Kushughulikia Masuala ya Usalama wa Mitandao (Tanzania Computer Emergency Response Team- CERT). Je, kitengo hiki kina wajibu gani hapa nchini Tanzania?

+

Wajibu wa kitengo hiki ni kuratibu matukio ya kiusalama katika mitandao na pia kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa katika kusimamia katika kusimamia matukio ya kiusalama mitandaoni.

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Je, ni makosa gani ya jinai na yasiyo ya jinai ambayo mara nyingi yanafanyika katika utumiaji wa mitandao ya kijamii kama vile \"Facebook\" na \"Instagram\"?

+

Yapo makosa mengi yafanyikayo katika mitandao ya kijamii ambayo ni pamoja na kuchapisha taarifa za uongo au za uchochezi, taarifa zenye lengo la kuwashushia heshima watu wengine, kufanya mambo ya kiutapeli n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand