Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je, mtu anaruhusiwa kukusanya au kuchakata taarifa binafsi bila kusajiliwa kama mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, sheria haimruhusu mtu yeyote kukusanya au kuchakata taarifa binafsi bila kusajiliwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda haki ya faragha ya kila mtu. Je ni Ibara gani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayozungumzia haki ya faragha ya mtu?

+

Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huzungumzia na kutambua haki ya faragha ya mtu.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, ni kosa mtu kutoa taarifa za uongo au kupotosha wakati wa usajili wa mchakataji au mkusanyaji wa taarifa binafsi?

+

Ndiyo, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kutoa taarifa za uongo au kupotosha wakati wa usajili wa mchakataji au mkusanyaji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, baada ya kukoma kwa kipindi cha kwanza cha uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa binafsi, anaweza kuteuliwa tena kwa vipindi vingapi?

+

Baada ya kukoma kwa kipindi cha kwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anaweza kuteuliwa kwa kipindi kingine kimoja tu na siyo zaidi.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina jumla ya wajumbe wangapi?

+

Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina jumla ya wajumbe saba.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, chombo cha usimamizi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kinaitwaje?

+

Chombo cha usimamizi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Mchakataji anatakiwa kuomba ridhaa ya maandishi ya mhusika wa taarifa kabla ya kuchakata taarifa binafsi nyeti. Je, kama mhusika wa taarifa hiyo ni mtoto au mtu ambaye hana akili timamu, nani anaweza kutoa ridhaa hiyo ya maandishi?

+

Endapo mhusika wa taarifa ambaye ridhaa yake inaombwa ni mtoto au mtu asiye na akili timamu, ridhaa huweza kutoka kwa mzazi, mlezi, mrithi, wakili wake au mtu yeyote anayetambulika kisheria kwa niaba yake anayepaswa kutoa ridhaa hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Kwa mujibu wa sheria, mtu haruhusiwi kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iwapo kutokana na madaraka aliyonayo anaweza kuwa na ushawishi kwa Tume. Je, hii ni kwanini?

+

Haitakiwi mtu kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kama kutokana na madaraka aliyonayo anaweza kuwa na ushawishi katika Tume ili kudumisha uadilifu wa Tume na kwa madhumuni ya kuepusha mgongano wa maslahi.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wanaweza kuteuliwa wote kutoka Tanzania Zanzibar?

+

Hapana, kwa mujibu wa sheria, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hawawezi kuteuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mmoja akiteuliwa kutoka Tanzania Bara, mwingine atateuliwa kutoka Tanzania Zanzibar.

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, pale ambapo mkusanyaji ana taarifa binafsi anaruhusiwa kufichua taarifa hizo kwa mtu tofauti na mhusika wa taarifa bila sababu yoyote inayokubalika kisheria?

+

Hapana, mkusanyaji akiwa na taarifa binafsi haruhusiwi kuzifichua taarifa hizo kwa mtu tofauti na mhusika wa taarifa bila sababu yoyote inayokubalika kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je, mkusanyaji anaruhusiwa kukusanya taarifa binafsi iwapo taarifa husika inakusanywa kwa madhumuni ambayo hayahusiani na kazi ya mkusanyaji?

+

Hapana, mkusanyaji anatakiwa kukusanya taarifa binafsi kwa madhumuni halali na yanayohusiana na kazi yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, mkusanyaji wa taarifa binafsi anaruhusiwa kukusanya taarifa binafsi kwa njia zisizo halali?

+

Hapana, mkusanyaji wa taarifa binafsi haruhusiwi kukusanya taarifa kwa njia ambazo si halali.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je, watu ambao siyo wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wanaruhusiwa kuwa wanakamati katika kamati za Bodi ya Tume?

+

Hapana, sheria inaelekeza kuwa ni wajumbe tu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wanaruhusiwa kuwa wanakamati wa kamati mbalimbali ndani ya Bodi.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Je, mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi anaweza kusajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Usajili wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka kumi kwa wakati mmoja bila kuhuisha usajili wake?

+

Hapana, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inaelekeza wazi kuwa kipindi cha usajili wa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi ni miaka mitano tu. Baada ya hapo, mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi anaweza kuhuisha tena usajili.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je, ni sahihi kwa mkusanyaji ambaye, bila sababu za msingi, anafichua taarifa binafsi kwa njia yoyote ambayo haiendani na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa?

+

Hapana, si sahihi kwa mujibu wa sheria mkusanyaji kufichua taarifa binafsi kwa njia ambayo haiendani na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je, taarifa binafsi zinaweza kusafirishwa nje ya mipaka ya nchi kinyume cha masharti ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Hapana, taarifa binafsi hazitakiwi kusafirishwa nje ya mipaka ya nchi kinyume cha masharti ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatakiwa kufanya uchunguzi dhidi ya mlalamikiwa aliyekiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi bila kuzingatia usiri wowote?

+

Hapana, Tume inapaswa kufanya uchunguzi dhidi ya mlalamikiwa aliyekiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa siri.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Kwa mujibu wa sheria, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anatakiwa kuwa na ujuzi au utaalamu katika nyanja ya ulinzi wa taarifa. Je, unadhani kwanini hii ni muhimu?

+

Hii ni muhimu kwasababu Mkurugenzi Mkuu anatakiwa kuwa na ufahamu wa kitu anachokisimamia. Kama kiongozi katika Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, anatakiwa kuwa na utaalamu tajwa kwa ajili ya usimamizi fasaha na fanisi.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Je, nani mwenye jukumu kisheria kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinahifadhiwa katika namna inayoruhusu utambuzi wa mhusika wa taarifa kwa muda usiozidi ule unaohitajika kwa madhumuni ya uchakataji wa taarifa binafsi husika?

+

Hili ni jukumu la mkusanyaji au mchakataji kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Je, nani mwenye wajibu kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinachakatwa kwa namna ambayo itahakikisha usalama wa taarifa binafsi, ikijumuisha ulinzi dhidi ya uchakataji usioruhusiwa au ulio kinyume cha sheria na dhidi ya hasara, uharibifu au madhara yoyote, kwa kutumia hatua sahihi za kiufundi au za kiutawala?

+

Huu ni wajibu wa mchakataji wa taarifa husika kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinachakatwa kwa namna hiyo tajwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria kuipa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi taarifa yoyote ambayo ni ya uongo au ya kuotosha wakati wa uchunguzi wa malalamiko. Je, unadhani ni kwanini kanuni hii ni ya muhimu?

+

Kanuni hii ni muhimu kwa maoni yangu kwasababu kama ikiruhusiwa mtu yeyote kutoa taarifa za uongo kwa Tume wakati inapofanya uchunguzi wa malalamiko inaweza kusababisha Tume isifikie maamuzi sahihi.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je, sheria inasemaje kuhusu nani anatakiwa kuwa katibu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Katibu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je, Kiongozi mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anateuliwa na nani kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Kiongozi mkuu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi) huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je, nani kiongozi mkuu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa mujibu wa sheria?

+

Kiongozi mkuu wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, kipindi cha usajili ni miaka mingapi kuanzia tarehe ya kutolewa kwa cheti cha usajili wa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi?

+

Kipindi cha usajili ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kutolewa kwa cheti cha usajili wa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je, mhusika wa taarifa binafsi anatakiwa kufanya nini ili anufaike kifedha baada ya mkusanyaji wa taarifa kuchakata taarifa zake binafsi (mhusika)?

+

Kwa mujibu wa sheria, mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Kwa mujibu wa sheria, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo yenye jukumu la kupokea na kushughulikia malalamiko yote ya ukiukwaji wa masharti ya sheria. Je, malalamiko yanatakiwa kuchunguzwa na kukamilika ndani ya kipindi cha muda gani baada ya kupokelewa?

+

Malalamiko yanayopokelewa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yanatakiwa kuchunguzwa na kumalizika ndani ya siku tisini tangu tarehe ya kupokelewa.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Sheria hutungwa ikiwa na malengo maalumu. Taja malengo matatu tu ya kutungwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hapa nchini Tanzania?

+

Malengo ya kutungwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni kudhibiti uchakataji wa taarifa binafsi, kulinda faragha za watu binafsi na kuwapa wahusika wa taarifa haki na nafuu katika kulinda taarifa binafsi kutokana na uchakataji usiofuata utaratibu.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, mambo ya ulinzi wa taarifa binafsi hapa nchini Tanzania yako chini ya wizara gani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

+

Mambo ya ulinzi wa taarifa binafsi hapa nchini Tanzania yako chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Je, maombi ya kuhuisha usajili wa kuwa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya muda gani kabla ya tarehe ya kuisha kwa kipindi cha usajili?

+

Maombi ya kuhuisha usajili yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe ya kuisha kwa kipindi cha usajili.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Unaelewa nini maana ya mchakataji wa taarifa binafsi?

+

Mchakataji ni mtu au taasisi ambayo kazi yake ni kuchakata taarifa binafsi kwa ajili na kwa niaba ya mkusanyaji wa taarifa binafsi chini ya maelekezo ya mkusanyaji.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Mhusika wa taarifa ana haki ya kumtaka mkusanyaji wa taarifa binafsi kupitia utaratibu maalumu, kusitisha au kutoanza uchakataji wa taarifa binafsi yoyote inayomhusu. Je, ni sababu gani inayokubalika kisheria na inayoweza kumfanya mhusika wa taarifa binafsi kufanya hivyo?

+

Mhusika wa taarifa naweza kumtaka mkusanyaji wa taarifa binafsi kusitisha au kutoanza uchakataji wa taarifa ikiwa uchakataji huo unaweza kusababisha madhara makubwa kwake au kwa mtu mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Unaelewaje maana ya Mhusika wa taarifa kama inavyotumika katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mhusika wa taarifa ni mtu ambaye taarifa zake binafsi zinakusanywa au zinachakatwa kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je, unadhani ni sababu gani zinaweza kumfanya mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kukoma kuwa mjumbe wa Bodi tajwa wakati wowote?

+

Mjumbe wa Bodi anaweza kukoma kuwa mjumbe wakati wowote baada ya kupoteza uwezo wa kutimiza majukumu yake kutokana na ugonjwa wa mwili au akili, utovu wa nidhamu au kujiuzulu.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Kutohudhuria vikao vya Bodi bila kutoa taarifa ni mojawapo ya sababu ambazo huweza kumfanya mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kukoma kuwa mjumbe. Je, mjumbe wa Bodi anaweza kukoma kuwa mjumbe kwa sababu hii kama ameshindwa kuhudhuria vikao vingapi mfululizo?

+

Mjumbe wa Bodi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anaweza kukoma kuwa mjumbe kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anashika madaraka kwa kipindi cha miaka mingapi baada ya kuteuliwa?

+

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi anashika nafasi kwa kipindi cha miaka mitano tu baada ya kuteuliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi huteuliwa na nani?

+

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi huteuliwa na Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je, nani mwenye jukumu la kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinatosheleza na ni muhimu kwa madhumuni ya uchakataji kama ilivyokusudiwa?

+

Mkusanyaji au mchakataji ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinatosheleza na ni muhimu kwa madhumuni ya uchakataji kama ilivyokusudiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Je, nani mwenye wajibu kisheria kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinachakatwa kihalali, kwa haki na kwa uwazi?

+

Mkusanyaji au mchakataji ndiye mwenye wajibu kisheria kuhakikisha kuwa taarifa binafsi zinachakatwa kihalali, kwa haki na kwa uwazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Mhusika wa taarifa ana haki ya kufahamishwa kuwa taarifa zake binafsi zinachakatwa na madhumuni ya uchakataji. Je, ni sababu zipi ambazo zinaweza kufanya mkusanyaji asilazimike kutoa taarifa hizo kwa mhusika wa taarifa?

+

Mkusanyaji wa taarifa binafsi halazimiki kutoa taarifa kwa mhusika endapo taarifa hizo siyo sahihi, zinahusika katika uchunguzi kwa mujibu wa sheria au zimezuiliwa kwa amri ya mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Kwa mujibu wa sheria, mkusanyaji wa taarifa binafsi anatakiwa kuhakikisha kuwa mhusika anatambua madhumuni ya ukusanyaji wa taarifa binafsi. Je, ni sababu gani huweza kupelekea takwa hilo la kisheria kutolazimika kulifuata?

+

Mkusanyaji wa taarifa halazimiki kufuata takwa hilo la kisheria kama taarifa binafsi husika zimekwishawekwa wazi au utekelezaji wake umeshindikana katika mazingira husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Kama kanuni ya jumla, rufaa ni haki ya mlalamikaji. Je, mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hususani pale ambapo upande mmoja haukuhudhuria wakati lalamiko limeitwa kusikilizwa anaweza kukata rufaa wapi?

+

Mlalamikaji ambaye hajaridhika na uamuzi wa Tume baada ya upande mmoja kutohudhuria anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je, ni taasisi zipi hapa nchini Tanzania ambazo zinajihusisha na ukusanyaji wa taarifa binafsi za watu.

+

Moja, Makampuni ya simu, Mbili, Hospitali, Tatu, Vyuo vikuu, Nne, Benki

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Nini maana ya “mpokeaji wa taarifa binafsi” kama inavyotumika katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mpokeaji wa taarifa binafsi ni mtu au taasisi ambayo inapokea taarifa binafsi kutoka kwa mkusanyaji.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Je, mtu anatakiwa kuwa na sifa gani ili kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mtu anatakiwa kuwa amehitimu shahada ya TEHAMA, uhandisi, sheria, uchumi, fedha au utawala, ana uzoefu usiopungua miaka kumi na ana utaalamu katika nyanja ya ulinzi wa taarifa ili kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Rufaa ni haki ya kila mtu pale ambapo hajaridhika na maamuzi. Je, mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hususani pale Tume inapokataa kumsajili kama mchakataji au mkusanyaji wa taarifa binafsi anaweza kuwasilisha rufaa yake kwa nani?

+

Mtu yeyote ambaye hajaridhika na uamuzi wa Tume anaweza kuwasilisha rufaa kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je, nani mwenye jukumu kwa mujibu wa sheria kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mwenye jukumu la kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume ni Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Je, nani mwenye jukumu la kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda sera za uendeshaji na usimamizi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mwenye jukumu la kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda sera za uendeshaji na usimamizi wa Tume ni Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hushika nafasi kwa kipindi cha muda gani?

+

Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hushika nafasi kwa kipindi cha miaka mine.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Je, nani mwenye mamlaka ya kuitisha kikao maalumu au kikao cha dharula cha Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Mwenyekiti, au akiwa hayupo, Makamu Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka hayo.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Je, Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kuunda kamati zozote ndani ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Ndiyo, Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kuunda kamati zozote ndani ya Tume.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Sheria inamtaka mkusanyaji kutengeneza kanuni za maadili na sera. Je, kanuni na sera hizo zinahitaji kupitiwa na kuidhinishwa?

+

Ndiyo, kanuni na sera zote ambazo hutengenezwa na mkusanyaji wa taarifa binafsi hutakiwa kupitiwa na kuidhinishwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Je, ni kosa kwa mchakataji ambaye anafichua taarifa binafsi iliyochakatwa na mchakataji bila idhini ya awali ya mkusanyaji wa taarifa husika?

+

Ndiyo, mchakataji ambaye anafichua taarifa iliyochakatwa na mchakataji bila idhini ya mkusanyaji anatenda kosa kisheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Mhusika wa taarifa anaweza kuwasilisha lalamiko lolote kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Je, mhusika ana haki ya kuwakilishwa katika Tume?

+

Ndiyo, mhusika ana haki ya kuwakilishwa na wakili au afisa wake wa nafasi za juu au mwakilishi aliyeidhinishwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Je, mhusika wa taarifa binafsi ana haki ya kufahamishwa na mkusanyaji yeyote endapo taarifa binafsi zinachakatwa na mkusanyaji huyo au mkusanyaji mwingine kwa niaba ya mkusanyaji huyo?

+

Ndiyo, mhusika wa taarifa binafsi ana haki ya kufahamishwa kuwa taarifa zake binafsi zinachakatwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, mkusanyaji anapaswa kutengeneza kanuni za maadili au sera kwa ajili ya ulinzi wa taarifa binafsi?

+

Ndiyo, mkusanyaji anapaswa kutengeneza kanuni za maadili au sera zinazobainisha maadili na miiko inayopaswa kuzingatiwa wakati wa ukusanyaji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Je, mkusanyaji wa taarifa binafsi ana wajibu kisheria wa kulinda taarifa binafsi dhidi ya upotevu wa kizembe?

+

Ndiyo, mkusanyaji wa taarifa binafsi ana wajibu kulinda taarifa binafsi dhidi ya upotevu wa kizembe.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je, mkusanyaji wa taarifa binafsi aliyesajiliwa anaweza kuwa na wawakilishi wake?

+

Ndiyo, mkusanyaji wa taarifa binafsi anaweza kuwa na wawakilishi wake

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Je, mhusika wa taarifa binafsi ana haki ya kulindwa kwa taarifa zake binafsi zinaposafirishwa kwenda nje ya nchi?

+

Ndiyo, ni haki ya mhusika wa taarifa.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Je, ni kosa la jinai kuizuia au kuikwamisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutekeleza mamlaka yake?

+

Ndiyo, ni kosa la jinai kuizuia au kuikwamisha Tume kutekeleza mamlaka yake na adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je, mhusika wa taarifa anayepata madhara kwa sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanywa na mkusanyaji wa taarifa ana haki ya kulipwa fidia?

+

Ndiyo, sheria inaeleza wazi kuwa mhusika yeyote anayepata madhara kwa sababu ya mkusanyaji wa taarifa kukiuka masharti ya sheria, mkusanyaji huyo anatakiwa kumlipa fidia mhusika huyo kwa madhara aliyosababishiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kumruhusu mtu yeyote kupekua na kupakua taarifa yoyote iliyoingizwa katika rejesta ya wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi?

+

Ndiyo, sheria inaipa mamlaka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kumruhusu mtu yeyote kupekua na kupakua taarifa yoyote iliyoingizwa katika rejesta.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kuteua washauri na wataalamu mbalimbali kama watumishi wa Tume?

+

Ndiyo, sheria inaipa mamlaka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuteua washauri na wataalamu mbalimbali kama watumishi wa Tume.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je, Tume ina wajibu wa kumpa notisi (taarifa) ya uchunguzi mkusanyaji anayehusika na malalamiko kabla ya kuanza uchunguzi dhidi yake?

+

Ndiyo, sheria inaitaka Tume kumpa notisi ya uchunguzi mkusanyaji anayehusika na malalamiko kabla ya kuanza uchunguzi dhidi yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina wajibu wa kutoa sababu za kukataa usajili wa mwombaji anayekusudia kuwa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi?

+

Ndiyo, Sheria inaitaka Tume kumtaarifu mwombaji kwa maandishi juu ya uamuzi wake na sababu ya uamuzi huo.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je, mhusika wa taarifa binafsi anaweza kumtaka mkusanyaji wa taarifa binafsi kuacha kuchakata taarifa zake binafsi (mhusika) kwa madhumuni ya matangazo ya biashara?

+

Ndiyo, Sheria inampa haki mhusika wa taarifa binafsi kumtaka mkusanyaji wa taarifa kuacha kuchakata taarifa zake kwa madhumuni ya biashara.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Kila mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi anatakiwa kwa mujibu wa sheria awe amesajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Je, mkusanyaji au mchakataji anaruhusiwa kuomba kwa Tume kuhuisha au kubadili taarifa yoyote iliyoingizwa katika rejesta?

+

Ndiyo, sheria inamruhusu mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi kuomba kuhuisha au kubadili taarifa yoyote.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inahusika na uimarishwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali?

+

Ndiyo, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inahusika kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali pamoja na vyombo binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inahusika na taarifa binafsi zilizokusanywa kwa njia ya kielektroniki?

+

Ndiyo, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inahusika pia na taarifa binafsi zilizokusanywa kwa njia ya kielektroniki.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatumika pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (yaani Tanzania Bara na Zanzibar)?

+

Ndiyo, Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatumika pande zote za muungano isipokuwa kwa upande wa Zanzibar haitumiki kwa mambo yasiyo ya muungano.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je, taarifa binafsi ambayo ipo kwenye mkanda au filamu inalindwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Ndiyo, taarifa binafsi iliyopo kwenye mkanda au filamu inalindwa pia chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kufuta usajili wa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi?

+

Ndiyo, Tume ina mamlaka ya kumfutia usajili mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inaweza kukataa lalamiko lolote la mlalamikaji. Je, Tume ina wajibu wa kutoa sababu za kukataa lalamiko husika?

+

Ndiyo, Tume inapaswa kutoa sababu za kukataa lalamiko husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ina mamlaka ya kuzuia usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya nchi?

+

Ndiyo, Tume inaweza kwa mujibu wa sheria kuzuia usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya nchi.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, nani mwenye jukumu la kuanzisha utaratibu wa ushirikiano na mamlaka za nchi nyingine zinazosimamia ulinzi wa taarifa binafsi na kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusiana na utelekezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Ni jukumu la Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuanzisha utaratibu wa ushirikiano na mamlaka za nchi nyingine zinazosimamia ulinzi wa taarifa binafsi na kuishauri Serikali katika masuala yanayohusiana na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, nani anatakiwa kuwajibika kisheria pale ambapo kosa lolote chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi limetendwa na kampuni au shirika?

+

Pale ambapo kosa limefanywa na kampuni au shirika, kampuni au shirika hilo na kila afisa wa shirika au kampuni hiyo ambaye ndiye mwidhinishaji wa kufanyika kwa kosa hilo hutakiwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Nini maana ya Rejesta ya Wakusanyaji na Wachakataji wa taarifa binafsi?

+

Rejesta ya Wakusanyaji na Wachakataji wa taarifa binafsi ni daftari la kusajili taarifa za wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, mtu anayekusudia kuwa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi anatakiwa kuwasilisha maombi ya usajili kwenye chombo gani?

+

Sheria inaelekeza kuwa mtu yeyote anayekusudia kuwa mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi anatakiwa kuwasilisha maombi ya usajili kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, sheria inaelekeza malalamiko kuwasilishwa kwa lugha gani?

+

Sheria inaelekeza malalamiko kuwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili au kiingereza.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, kabla ya kukusanya taarifa binafsi za mhusika, ni mambo gani ambayo mkusanyaji wa taarifa anatakiwa kuhakikisha kwamba mhusika anayafahamu vema?

+

Sheria inaelekeza wazi kuwa kabla ya kukusanya taarifa binafsi, mkusanyaji anatakiwa kuhakikisha kuwa mhusika anatambua madhumuni ya ukusanyaji wa taarifa binafsi, anafahamu kuwa ukusanyaji wa taarifa binafsi ni kwa madhumuni yaliyoidhinishwa na kuwa anawafahamu wapokeaji wa taarifa binafsi waliokusudiwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Mtu yeyote ana haki ya kuruhusiwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kupekua na kupakua taarifa yoyote iliyoko kwenye rejesta. Je, mtu huyo anatakiwa kulipa malipo yoyote kwa huduma hiyo?

+

Sheria inaeleza kuwa mtu atatakiwa kulipa ada iliyoainishwa na Tume ili aruhusiwe kupekua na kupakua taarifa yoyote iliyoingizwa kwenye rejesta ya wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je, mchakataji anaruhusiwa kuchakata taarifa binafsi za vinasaba, taarifa inayohusu watoto, makosa au hukumu ya jinai, hatua za kiusalama au taarifa za kibayometriki bila ridhaa ya mhusika wa taarifa hizo?

+

Sheria inaeleza, kama kanuni ya jumla, kuwa mchakataji hatakiwi kuchakata taarifa binafsi nyeti (ambazo hujumuisha mifano ya taarifa za aina hizo tajwa) bila ridhaa ya maandishi ya mhusika wa taarifa.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Nini maana ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni kanuni na taratibu zinazoweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa lengo la kuweka kiwango cha chini cha matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi na kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali na vyombo binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Unaelewa nini maana ya taarifa binafsi?

+

Taarifa binafsi ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote kama vile taarifa zinazohusu rangi, asili ya kitaifa, kikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu binafsi, taarifa zinazohusu elimu, historia ya matibabu, jinai, ajira na kadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Kwa mujibu wa sheria, malalamiko yanayowasilishwa kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yanatakiwa kuchunguzwa na kumalizika ndani ya siku tisini baada ya tarehe ya kupokea malalamiko hayo. Lakini, kuna wakati ambapo Tume inaweza kuongeza muda ulioainishwa. Je, ni kipindi cha muda gani ambacho Tume huweza kuongeza?

+

Tume huweza kuongeza kipindi cha siku tisini tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Tume inaweza kukataa lalamiko la mtu yeyote. Je, Tume inapaswa kumtaarifu mlalamikaji kuhusu kukataliwa kwa lalamiko lake ndani ya muda gani?

+

Tume inapaswa kumtaarifu mlalamikaji kuhusu kukataliwa kwa lalamiko lake ndani ya siku saba baada ya tarehe ya uamuzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inaweza kukataa malalamiko baada ya kuwasilishwa na mlalamikaji?

+

Tume inaweza kukataa malalamiko iwapo haijabainisha chanzo, muda wake umepita au suala linalolalamikiwa lipo katika mahakama.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Je, nani huanzisha na kutunza rejesta ya wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo huanzisha na kutunza rejesta ya wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Katika hali ya kawaida, kila mtu ana wajibu wa kimaadili kumwelimisha mwenzake. Je, kwa mujibu wa sheria, ni nani ana jukumu la kutoa elimu kwa umma kwa kadri inavyofaa kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo yenye jukumu kwa mujibu wa sheria kutoa elimu kwa umma juu ya utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je, nani mwenye wajibu kwa mujibu wa sheria kufanya tafiti na kufuatilia maendeleo ya teknolojia kuhusiana na uchakataji wa taarifa?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo yenye jukumu la kufanya tafiti na kufuatilia maendeleo ya teknolojia kuhusiana na uchakataji wa taarifa.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Malalamiko ya watu kuhusu madai ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu yanapaswa kuchunguzwa na kushughulikiwa ipasavyo. Je, nani mwenye jukumu la kupokea, kuchunguza na kushughulikia malalamiko kuhusu madai ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo yenye jukumu la kupokea na kushughulikia malalamiko ya watu juu ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha zao.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je, nani mwenye mamlaka ya kupitia na kuidhinisha kanuni na sera zinazotengenezwa na mkusanyaji wa taarifa binafsi?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ndiyo yenye mamlaka kupitia na kuidhinisha kanuni na sera zinazotengenezwa na mkusanyaji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Eleza maana ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni chombo kinachofuatilia utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kusajili wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Unaelewa nini maana ya uchakataji wa taarifa binafsi?

+

Uchakataji wa taarifa binafsi ni uchambuzi wa taarifa binafsi kwa njia za kiotomatiki au vinginevyo, kama vile kukusanya, kurekodi au kushikilia taarifa binafsi, ikiwa na pamoja na kuzipanga upya, kuzibadilisha, kuziwianisha n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Je, nini hutumika kama uthibitisho kuwa mkusanyaji au mchakataji amesajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi?

+

Uthibitisho kuwa mkusanyaji au mchakataji amesajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni cheti cha usajili ambacho mwombaji anapewa baada ya kuwa amekidhi matakwa ya usajili.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Mkusanyaji au mchakataji anapaswa kuteua afisa ulinzi wa taarifa binafsi. Je, nini wajibu wa msingi wa afisa huyu anayeteuliwa na mchakataji au mkusanyaji wa taarifa binafsi?

+

Wajibu wa msingi wa afisa ulinzi wa taarifa binafsi ni kuhakikisha kuwa hatua za kiudhibiti na za kiusalama zinachukuliwa ili kulinda taarifa taarifa binafsi zinazokusanywa au kuchakatwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Je, wajumbe wengine wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, wanatakiwa kuwa na sifa na uzoefu katika maeneo gani?

+

Wajumbe wengine wa Bodi tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wanatakiwa kuwa na sifa na uzoefu katika mojawapo ya maeneo ya TEHAMA, sheria, uhandisi, fedha au utawala.

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Je, wajumbe wengine wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) hushika nafasi kwa kipindi cha muda gani?

+

Wajumbe wengine wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) hushika nafasi kwa kipindi cha miaka mitatu tu.

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, je wajumbe wengine wanateuliwa na nani?

+

Wajumbe wengine wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi tofauti na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti huteuliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Sheria Kiganjani
Learn More
100

Je, ni kwanini kunatakiwa kuwepo na wajumbe wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wenye utaalamu wa TEHAMA?

+

Wajumbe wenye utaalamu katika TEHAMA wanatakiwa kuwepo katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwasababu mambo ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kwa kipindi hiki ambapo kuna kasi kubwa ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano, hufanyika katika vyombo vya kiteknolojia kama vile kompyuta.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand