Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je, uhujumu uchumi unaweza kuathiri ufaulu shuleni?

+

Hii inawezekana hasa katika kipindi hiki ambapo kumekuwa na elimu bure, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kila mwezi kama ruzuku kufadhili elimu bure, hivyo endapo wasimamizi wa fedha hizo na sera za uchumi kwa ujumla watashindwa kutekeleza majukumu yao hii inaweza kuathiri ufaulu wa wanafunzi na wengi wao wataishia mitaani.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, uhujumu uchumi unaweza kuleta uhasama na chuki katika jamii?

+

Hii inawezekana kabisa hasa pale kiongozi katika jamii au mtu yoyote, atakapogundulika kuwa anajihusisha na vitendo vya kuhujumu uchumi, hivyo jamii inaweza kumchukia na hata kuwa na uhasama dhidi yake kwani anatumia mali za umma kwa manufaa yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Sera ya uhujumu uchumi ni nini?

+

Hii ni mipango maalumu inayoonesha namna serikali inavyopambana na vitendo vya uhujumu na namna sheria ya uhujumu uchumi inavyoweza kutimiza azima yake ya kuzuia na kupambana dhidi ya vitendo vya uhujumu uchumi.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, sera ya rushwa ni nini?

+

Huu ni mpango maalumu, au utaratibu uliopo ambao lengo lake ni kutafuta namna ya kupata suluhu ya jambo flani, au ni mpango unaonesha namna mapambano juu ya jambo fulani yanavyofanyika au yatakavyofanyika.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, Takukuru inafanya kazi gani?

+

kama inavyo jieleza yenyewe, Takukuru inafanya kazi kubwa hasa ya kutoa elimu juu ya mapambano juu ya vitendo vya rushwa, inasimamia midahalo mbali mbali ambayo inaendeshwa kwa lengo kuu la kutoa elimu juu ya vitendo vya rushwa nakadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, kuna kitengo maalumu kinacho shughulikia kuripoti kesi za makosa ya uhujumu uchumi?

+

Kama tulivyo ona hapo awali kwamba kuna divisheni maalumu inayo fanya kazi za kuchunguza, kuripoti na kutoa ushahidi mahakamani pale makosa ya uhujumu uchumi yanapo endeshwa au kusikilizwa, nayo inaitwa (Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa).

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, Tanzania kuna taasisi inayohusika na maswala ya rushwa?

+

Kimsingi ipo Taasisi inayojihusisha na kupambana na rushwa iitwayo TAKUKURU, iliyo anzishwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je, Tanzania kuna taasisi inayohusika na maswala ya rushwa?

+

Kimsingi ipo Taasisi inayojihusisha na kupambana na rushwa iitwayo TAKUKURU, iliyo anzishwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, Tanzania kuna taasisi inayohusika na maswala ya rushwa?

+

Kimsingi ipo Taasisi inayojihusisha na kupambana na rushwa iitwayo TAKUKURU, iliyo anzishwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, uhujumu uchumi unaweza kuathiri ukuaji wa sekta binafsi nchini?

+

Kimsingi uhujumu uchumi unaathari katika ukuaji wa sekta binafsi nchini, hasa pale ambapo watu wenye dhamana ya kusimamia sera na sheria za ukuaji wa sekta binafsi watakapo fanya vitendo kinyume na taratibu zilizo wekwa na sheria hizo, au kutumia bajeti zilizo tengwa kwa manufaa binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je, nini kifanyike ili kuzuia rushwa ya ngono?

+

kutoa elimu zaidi kwa rika zote kwa uwazi bila kuona aibu ili jamii kwa ujumla iweze kuelewa zaidi juu ya rushwa ya ngono na athari zake.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, kuna vitendo vya rushwa maeneo ya kazi?

+

Ndio, hii ni ahadi itolewayo kwa mwajiri ili aweze kutimiza lengo la mwajiri wake au mfanyakazi mwenzake bila ya ridhaa yake kutoka moyoni, au pesa ili aweze kupewa upendeleo flani kinyume na utaratibu.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je, rushwa huweza pelekea mimba za utotoni kwa wanafunzi waliopo mashuleni?

+

Ndiyo, inawezekana tena kwa kiasi kikubwa kwani kuna baadhi ya walimu wanatumia nafasi waliyo nayo kuwaahidi wanafunzi hasa watoto wa kike alama katika masomo au kwa kuwapa zawadi, kutokana na hali ya maisha ya wale wanafunzi na hatimaye mimba mashuleni.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Je, rushwa inapelekea mmomonyoko wa maadili?

+

Ndiyo, rushwa inaweza kuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwani utakuta kijana hata kama alikuwa kwenye foleni na mzee wakisubiri huduma flani huyo kijana kwa kukosa maadili anaweza kutoa rushwa ili ahudumiwe yeye kwanza.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je, rushwa inaweza kupelekea ajali barabarani?

+

Rushwa huweza kupelekea ajali, kwani askari anaehusika siku hiyo atashindwa kuchukua hatua stahiki kwa dereva anaendesha mwendo kasi au anaendesha bila kuangalia alama za usalama barabarani hasa pale anapopewa rushwa au zawadi ya aina yoyote kutoka kwa dereva na hatimae kupelekea ajali ambazo zingeweza kuzuilika, pia huweza kupelekea hata vifo.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je, rushwa inapelekea huduma duni, kwa jamii?

+

Rushwa inapelekea huduma duni kwa jamii kwani watoa huduma wengi, wataweka weledi mkubwa kwa yule anae wapatia rushwa na kwa wanajamii kupewa huduma duni na kwa wakati mwingine kukosa kabisa huduma.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, rushwa inapelekea huduma duni, kwa jamii?

+

Rushwa inapelekea huduma duni kwa jamii kwani watoa huduma wengi, wataweka weledi mkubwa kwa yule anae wapatia rushwa na kwa wanajamii kupewa huduma duni na kwa wakati mwingine kukosa kabisa huduma.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Maeneo gani rushwa ya ngono imeshamili zaidi?

+

Rushwa ya ngono ipo zaidi Maeneo ya kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa, majumbani kati ya mwenye nyumba na dada wa kazi, mwenye nyumba na mpangaji wake, vyuoni, mashuleni nakadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Maeneo gani rushwa ya ngono imeshamili zaidi?

+

Rushwa ya ngono ipo zaidi Maeneo ya kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa, majumbani kati ya mwenye nyumba na dada wa kazi, mwenye nyumba na mpangaji wake, vyuoni, mashuleni nakadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Nini athari za rushwa ya ngono?

+

 Rushwa ya ngono inaweza kupelekea kupata mimba zisizo tarajiwa, magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI, KASWENDE, GONOREA N.K,

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Je, sera ya rushwa ni nini?

+

: Huu ni mpango maalumu, au utaratibu uliopo ambao lengo lake ni kutafuta namna ya kupata suluhu ya jambo flani, au ni mpango unaonesha namna mapambano juu ya jambo fulani yanavyofanyika au yatakavyofanyika.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Nini chanzo cha rushwa hospitalini?

+

Chanzo cha rushwa hospitalini ni uelewa mdogo juu ya miiko ya kazi hasa sheria ya afya na tamaa binafsi za nesi au mganga, kukosa maadili.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Nini chanzo cha rushwa ya ngono?

+

Chanzo cha rushwa kinaweza kuchangiwa na umasikini, tamaa, au matumizi mabaya ya madaraka.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je, dhana ya rushwa ni ipi?

+

Dhana ya rushwa ni hali inayotokea ambapo mtoaji wa rushwa anamuahidi mpokeaji kuwa atampa kitu fulani kama zawadi au kitu chochote chenye thamani ili amfanikishie lengo lake, lakini kuna kuwa haijathibitishwa kabisa kisheria kuwa kuna mtu alipokea na kukubali kupewa rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, uhujumu uchumi unaweza kusababisha mtu kukosa/kufukuzwa kazi?

+

Hii imekuwa ikijitokeza hasa katika viongozi wa serikali kwani tumekuwa tukiona wengi wakisimamishwa kazi au kufukuzwa kazi, au wakandarasi wanaojenga miradi mbali mbali wanapo jihusisha na vitendo vya uhujumu uchumi

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je, maeneo ya biashara napo kunaweza kuwapo na vitendo vya rushwa?

+

Hii inatokea kwa wafanyabiashara na wateja wao au wakusanya kodi na wafanya biashara, huweza kutoa rushwa ya aina yoyote ili kuweza kutimiza haja zao ovu, kama kukwepa kodi nakadhalika.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Je, uhujumu uchumi unaweza kuondoa au kupunguza uaminifu?

+

Hii inawezekana hasa pale ambapo kiongozi au mtu yoyote atakae kuwa anajihusisha na vitendo vya uhujumu uchumi, kama ni mtumishi wa serikali basi atakosa kuaminiwa na serikali na wafanyakazi wengine kwa ujumla, na hivyo kuwa na sifa mbaya kwenye jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Je, waendesha boda boda nao wanajihusisha na vitendo vya rushwa?

+

hii inawezekana kabisa kwani baadhi ya waendesha boda boda huweza kuwadanganya hasa wanafunzi kwa kuwapa lifti ili kuweza kutimiza azima zao ovu za tama ya ngono, lakini pia hata wao huweza kuahidiwa pesa au zawadi mbali mbali.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, rushwa inaweza kupelekea maendeleo duni katika jamii?

+

Hii inawezekana kwani tumekuwa tukiona katika maeneo mengi viongozi wengi mamekuwa wakisimamia vibaya fedha za serikali zinapoletwa katika maeneo yao na kuishia kutumia zile fedha kwa kujinufaisha na hatimae maendeleo duni.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Je, rushwa inaweza pelekea mtu kujiua?

+

Hii inawezekana tena kwa kiasi kikubwa kwani wahanga wengi wa rushwa hasa rushwa ya ngono, huweza kukumbwa na msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea kufanya maamuzi magumu ikiwemo kujiua.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Je, rushwa ya ngono ni nini?

+

Hii ni aina ya rushwa ambayo mhanga anaombwa ili aweze kupewa huduma flani au ajira, au upendeleo flani kutoka kwa mtoa huduma au mwajiri

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Je, Rushwa katika uchaguzi ni ipi?

+

Hii ni aina ya rushwa inayotolewa na wagombea kwenda kwa wananchi ili waweze kupigiwa kura, au kutoka kwa wagombea kwenda kwa wasimamizi wa uchaguzi ili waweze kupata upendeleo fulani.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Je, uhujumu uchumi unaweza kuchelewesha kukamilika kwa miradi ya kimaendeleo?

+

Hii ni pale ambapo watu wenye dhamana ya kusimamia miradi ya kimaendeleo watakapo tumia fedha zilizo tengwa kwa ajili ya miradi hiyo watakaposhindwa kutimiza wajibu wao, au kua na usimamizi hafifu wa miradi hiyo, na hivyo kufanya miradi mingi kuchukua mda mrefu hadi kukamilika.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je, rushwa inaweza kupelekea kupata wahitimu wasiokuwa na weledi?

+

Hii, inawezekana hasa vyuoni ambapo wahadhili huweza kuomba rushwa ya ngono kwa wanavyuo wakike kwa lengo la kuwaongezea alama wasizo stahili na hatimae kuwa na whitimu wengi mtaani wasiokuwa na weledi.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Rushwa katika vyombo vya usafiri ni ipi?

+

Hizi ni pesa au zawadi ya aina yoyote inayotolewa na dereva wa chombo cha usafiri kwenda kwa askari wa usalama barabarani ili aweze kusamehewa makosa fulani yanayotokana na mwendo kasi au kosa la aina nyingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je, mhanga wa rushwa ni nani?

+

Huyu ni mtu yoyote alie athiriwa na vitendo vya rushwa, huweza kuwa rushwa ya ngono au rushwa ya aina yoyote, au mtu alie wahi kupata madhara flani yatokanayo na rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je, rushwa hospitalini inaweza kupelekea vifo vya mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua?

+

inaweza kupelekea vifo tena kwa kiasi kikubwa kwani kuna wakunga wengine mahospitalini huweza kutaka rushwa kutoka kwa mama alieshikwa na uchungu na akikosa hiyo rushwa huweza kutelekezwa au kunyimwa baadhi ya vifaa kama vile glovzi kwa madai hadi akanunue zake maskini akiwa hana uwezo kwa wakati ule mama huweza kujifungua bila uangalizi na hatimae kuweza kupelekea kifo chake au cha mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je, mtu akikutwa na nyaraka za serikali anakuwa anahujumu uchumi?

+

Jibu ni ndiyo kwani moja kati ya vitendo vya uhujumu uchumi ni pamoja na kufanya uwindaji haramu wa wanyama pori na hasa kwa kutafuta pembe za ndovu, na ngozi za wanyama mbali mbali kwa lengo la kujipatia kipato kinyume na sheria zinazo husika katika eneo hilo.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Je, uhujumu uchumi unaweza kuwa chanzo cha umasikini kwa mtu mmoja mmoja katika jamii?

+

Jibu ni ndiyo, kwani hii inatokea hasa pale watu waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya uchumi watakaposhindwa kutekeleza majukumu yao, mfano kwa kuchukua fedha za walipa kodi kwa kuwaahidi kitu flani kama leseni na kushindwa kutekeleza lengo hilo, hivyo wengi kushindwa kumudu gharama za uendeshaji wa biashara na hivyo kuathiri uchumi wao.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je, jukumu la kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa ni la nani?

+

jukumu la kupambana na rushwa ni la kila mmoja kwani athari zitokanazo na vitendo vya rushwa huweza kumwathiri kila mtu katika jamii aidha moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, hivyo mapambano dhidi ya rushwa ni vita ambayo inamuhitaji kila mtu.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je, nini athari za rushwa hospitalini?

+

kama yalivyo maeneo mengine rushwa hospitalini inaweza kupelekea vifo visivyo tarajiwa, kwani mgonjwa hasa maskini asie na kitu cha kutoa huweza kukaa kwenye foleni mda mrefu au kupewa huduma tofauti na yule alie toa rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je, nini athari za rushwa hospitalini?

+

kama yalivyo maeneo mengine rushwa hospitalini inaweza kupelekea vifo visivyo tarajiwa, kwani mgonjwa hasa maskini asie na kitu cha kutoa huweza kukaa kwenye foleni mda mrefu au kupewa huduma tofauti na yule alie toa rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je, rushwa inapunguza nidhamu maeneo ya kazi?

+

Kama yalivyo maeneo mengine rushwa inapunguza nidhamu, hasa kati ya mwajiri na mwajiriwa kama kuna vitendo vya rushwa baina yao.

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Je, uhujumu uchumi unaweza kusababishwa na mfumuko wa bei nchini?

+

Kimsingi kama tulivyo ona hapo awali kuwa kukwepa kodi nayo inajumuishwa katika makosa ya uhujumu uchumi, hivyo basi bei za bidhaa nyingi zikiwa juu sana watu watashindwa kutekeleza majukumu yao kama yalivyo ainishwa katika sheria za kodi na hivyo kuhujumu uchumi.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Je, nani mwenye jukumu la kufanya upelelezi juu ya maswala ya rushwa?

+

Kimsingi kama tulivyo ona tangu awali kuwa TAKUKURU ni chombo kilicho anzishwa kisheria kushughulikia maswala ya rushwa, hivyo pia chombo hicho kinayo mamlaka ya kufanya upelelezi juu ya maswala ya rushwa na kutoa ushahidi mahakamani pale itakapohitajika.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Je, rushwa inaweza kurudisha nyuma juhudi za serikali kwa ujumla?

+

Kimsingi rushwa inarudisha nyuma juhudi za serikali na ndio maana serikali kupitia mamlaka zenye dhamana imeweza kuanzisha mbinu mbali mbali za kuweza kupambana na vitendo vya rushwa, ili kuweza kutimiza azima yake ya kuleta maendeleo katika jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je, Tanzania kuna chombo kinachohusika na makosa ya rushwa?

+

Kimsingi Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika kupambana dhidi ya rushwa, kwani imeweza kuanzisha divisheni maalumu inayohusika na makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa ikiwemo.

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Je, wazazi wanaongea na watoto wao juu ya elimu ya rushwa ya ngono?

+

Kimsingi wazazi wengi huona aibu kuwaelimisha watoto wao hasa wakike juu ya vitendo vya rushwa ya ngono kwa kuoneana aibu na baadae kuishia kulaumu pale ambapo binti yao yatamkuta n.k

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je, polisi nao wanajihusisha na vitendo vya rushwa?

+

Kituo cha polisi nacho ni moja ya sehemu inayo lalamikiwa sana juu ya kujihusisha na vitendo vya rushwa, kwani polisi wengi hushindwa kuzingatia sheria ya maadili ya polisi kazini na kuishia kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Je, sheria ipi inatambua rushwa ya uchaguzi?

+

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa kitaifa Namba 1 ya mwaka 1985, sheria hii inatambua makosa mbali mbali yatokanayo na vitendo vya rushwa hasa kipindi cha uchaguzi na kuainisha hatua mbali mbali zinazoweza kuchukuliwa ikiwemo adhabu mbali mbali.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Je nini maana ya utakatishaji fedha na inaweza kuwa njia ya uhujumu uchumi?

+

Maana ya utakatishaji fedha ni namna ya kujipatia fedha haramu yaani zimepatikana kutokana na shughuli isiyo halali kisheria na kutafuta njia mbali mbali kuziwezesha fedha hizo zionekane kuwa ni halali, pia kutakatisha fedha ni njia moja wapo ya kuhujumu uchumi na ndio maana sheria imeweka adhabu kali kwa watu watakao husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Je, madawati ya jinsia yanashiriki katika mapambano dhidi ya rushwa?

+

Madawati ya jinsia kama chombo mojawapo kinacho saidia jamii juu ya maswala ya kijinsia kimekuwa kikipokea taarifa mbali mbali kutoka kwa wahanga wa rushwa ya ngono na kuwasaidia kufika katika mamlaka husika, lakini pia madawati ya jinsia yanatoa ushauri na elimu na nyenzo mbali mbali za kuweza kuripoti vitendo vya rushwa hasa ya ngono.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Je, makosa ya rushwa ni ya jinai au madai?

+

Makosa ya rushwa ni ya jinai na ndio maana katika mahakama zetu huendeshwa kama makosa mengine ya jinai kama vile makosa ya wizi, kukutwa na nyaraka za serikali.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Je, mamlaka zote zinazohusika na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwa ujumla zipo chini ya wizara gani nchini?

+

Mamlaka na sheria zote zinazo husika na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi zipo chini ya wizara ya fedha ambayo inahusika na maswala yote ya fedha nchini kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali kama vile TAKUKURU.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Mhujumu uchumi ni nani?

+

Mhujumu uchumi ni mtu au kikundi cha watu ambao hufanya vitendo vya uhujumu uchumi. Mtu yeyote anaweza kuwa mhujumu uchumi ikiwa atashiriki katika vitendo vya uhalifu wa kiuchumi kama vile rushwa, ufisadi, udanganyifu wa kifedha, utakatishaji wa fedha haramu, na biashara ya bidhaa au huduma haramu. Hata hivyo, mhujumu uchumi mara nyingi hufanya vitendo hivyo kwa nia ya kupata faida binafsi au kujinufaisha wao na kikundi chao, huku wakijua kuwa vitendo hivyo vinaharibu uchumi wa nchi au eneo husika na hata kusababisha madhara kwa jamii kwa ujumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, kazi ya divisheni hiyo ni nini?

+

Moja kati ya kazi ya divisheni hii ni kuratibu kesi za rushwa katika mahakama kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na mahakama za chini, pia inafanya kazi ya kufungua na kuendesha kesi za rushwa na masuala yanayohusiana nayo, kusimamia na kushauri njia bora za uendeshaji wa kesi za rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Je, mtu mmoja mmoja anawezaje kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa?

+

Mtu mmoja mmoja anaweza kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa katika jamii anayoishi au eneo la kazi, kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika mamlaka zinazo husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhusika wa vitendo vya rushwa

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je, Tanzania kuna sheria ya kuzuia rushwa?

+

Ndio, Tanzania kuna sheria ya kuzuia rushwa iitwayo Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Je, uhujumu uchumi unaweza kuathiri ukuaji wa uchumi nchini?

+

ndiyo hii inawezekana kwani kama tulivyo ona tangu mwanzo kuwa uhujumu uchumi ni kushindwa kutekeleza au kwenda kinyume na sheria za uchumi nchini, hivyo basi kufanya hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwenye ukuaji wa uchumi kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja katika jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Je, rushwa ina athari kwenye miradi ya kimaendeleo?

+

Ndiyo ina athari kubwa sana kwani hupelekea usimamizi mbovu wa miradi ya kimaendeleo na hatimaye kupata miradi mibovu isiyo dumu kwa muda mrefu.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je, rushwa inapunguza utendaji kazi eneo la kazi?

+

Ndiyo inapunguza utendaji kazi kwani mfanyakazi anaweza kuacha kufanya kazi za msingi au kuacha kutimiza wajibu wake hadi apewe rushwa, hivyo kupunguza utendaji kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, rushwa inapunguza utendaji kazi eneo la kazi?

+

Ndiyo inapunguza utendaji kazi kwani mfanyakazi anaweza kuacha kufanya kazi za msingi au kuacha kutimiza wajibu wake hadi apewe rushwa, hivyo kupunguza utendaji kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, rushwa inaweza kupelekea ongezeko la watoto wa mitaani?

+

Ndiyo inawezekana kwani wahanga wa rushwa hasa rushwa ya ngono wanapo pata mimba huweza kujifungua watoto wanaokosa malezi bora kutokana na umaskini na hatimae kuishia kuwa watoto wa mitaani.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je, rushwa inaweza kukwamisha ndoto za mwanafunzi?

+

Ndiyo inawezekana kwani wanafunzi wengi ambao ni wahanga wa rushwa wanapo pata mimba wengi wao hushindwa kuendelea na masomo na hatimae kuishia kulea watoto wao

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je, Tanzania inashirikiana na mataifa mengine Duniani katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa?

+

Ndiyo Tanzania inashirikiana na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya rushwa, na ndio maana mnamo mwaka 2017 katika mkutano wa kimataifa wa kupinga rushwa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais kipindi hicho, Mh. Samia Suluhu Hassan, alinukuliwa akisema Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je, kuna usalama wa huyo mtu baada ya kutoa taarifa au kuripoti juu ya vitendo vya rushwa?

+

Ndiyo usalama upo kwani moja kati ya miiko ya kazi katika taasisi za serikali na Takukuru ikiwemo ni pamoja na usiri wa taarifa zilizo ripotiwa juu ya vitendo vya rushwa katika maeneo mbali mbali.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Je, Tanzania kuna sheria ya ulinzi wa mtoa taarifa?

+

Ndiyo, Tanzania kuna sheria ya ulinzi wa mtoa taarifa na taarifa binafsi zikiwemo na taarifa za vitendo vya rushwa, sheria hiyo inaitwa, (Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, sheria namba 11 ya mwaka 2022), sheria hii imetoa utaratibu maalumu juu ya ulinzi wa taarifa binafsi na ulinzi wa mtoa taarifa na za rushwa zikiwemo.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, uhujumu uchumi unaathiri ukuaji au ongezeko la pato la taifa?

+

Ndiyo, uhujumu uchumi unaathiri ukuaji wa pato la taifa kwani shughuli zote na sheria za kiuchumi nchini lengo lake kuu nchini ni kukuza pato la taifa, hivyo basi pale vitendo vya uhujumu uchumi vinapokithiri nchini vinaathiri ukuaji wa pato la taifa kwani makusanyo mengi yatashindwa kufikishwa kwenye mfuko wa hazina ya taifa

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je, ni kwa njia gani mtu akijiingizia kipato atakuwa amehujumu uchumi?

+

Pale mtu anapojiingizia kipato kwa njia haramu kama kuuza pembe za ndovu, au kuuza mali yoyote kwa maslahi binafsi hasa kinyume na sheria, katika njia hizo na zingine nyingi mtu huyo atakuwa amehujumu uchumi.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je, rushwa inaweza kuwa na athari katika vyombo vya habari?

+

Rushwa ina athari kubwa kwenye vyombo vya habari, kwani wahusika wa vitendo vya rushwa huweza kuwatishia wanahabari hasa pale wanapotaka kuripoti taarifa zao katika eneo husika, hivyo wanahabari wengi huogopa na kushindwa kuripoti taarifa hizo.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je, rushwa ina athari kwenye haki za binadamu?

+

Rushwa ina athari kwenye haki za binadamu, kwani haki ya mtu huweza kunyimwa au kuvunjwa pale anapo kosa kitu cha kutoa ili aweze kutimiziwa haki yake, mfano haki ya kufanya kazi ambayo ipo kwa mujibu wa katiba ya nchi, binti anaetafuta kazi na akaombwa rushwa ya ngono na mwajiri na akakataa anaweza kunyimwa kazi na hatimae haki yake ya msingi kuvunjwa

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, rushwa ina athari gani katika ukuaji au ongezeko la pato la taifa?

+

Rushwa inaathiri ukuaji wa pato la taifa kwani makusanyo mengi kutoka katika vyanzo vya mapato mbali mbali hushindwa kufika katika mfuko wa hazina ya taifa na kuishia kwenye mifuko ya watu au viongozi wasiokuwa na maadili ya kazi zao au wenye tama binafsi.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, rushwa inapelekea kuchelewa kukamilika kwa miradi ya kimaendeleo?

+

Rushwa inapelekea kuchelewa kwa miradi ya kimaendeleo, kwani fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya hiyo miradi hushindwa kufika eneo husika na kuishia kwenye mifuko ya watu na hatimae kuchelewesha huduma kwa jamii.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je, rushwa inapelekea usimamizi mbovu wa miradi ya kimaendeleo?

+

Rushwa inapelekea usimamizi mbovu wa miradi wa kimaendeleo kwani wahusika wakuu wa kusimamia hiyo miradi hushindwa kutimiza wajibu wao kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, rushwa inaweza kupelekea mtu kukosa kazi?

+

Rushwa inaweza fanya mtu kukosa kazi hasa mtu Yule anaejihusisha na vitendo rushwa au mtu Yule aliye ombwa rushwa akakataa hasa ile rushwa ya ngono kwa mtu anaetafuta kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, rushwa inaweza kupelekea mtu kukosa kabisa nafasi za uongozi serikalini?

+

Rushwa inaweza kufanya mgombea wa nafasi flani kukosa nafasi hiyo hasa pale itakapogundilika kuwa amekuwa akijihusisha na vitendo vya rushwa hapo awali, hivyo kukosa sifa za kuwa kiongozi wa kulitumikia taifa na jamii kwa ujumla

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je, rushwa inaweza kupelekea kupata viongozi wasiokuwa na uwezo?

+

Rushwa inaweza kupelekea kupata viongozi wasiokuwa na uwezo kwani watu wengi wenye uchu na madaraka huweza kuhonga pesa au mali flani ili waweze kupata nafasi flani katika uongozi bila hata kujali kama wako na uwezo au vinginevyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, rushwa inaweza kuwa kikwazo katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja?

+

Rushwa inaweza kuwa kikwazo katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwani Yule mtu anae kata kutoa au kukea rushwa anaweza kukosa kazi au huduma flani ya msingi na hatimae rushwa kuwa kama kikwazo kwake.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Nini maana ya rushwa?

+

Rushwa ni vitendo visivyo halali vya kutoa au kupokea kitu cha thamani ili kufikia lengo fulani, kwa kawaida ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa jamii na uchumi wa nchi. Rushwa inaweza kujumuisha kutoa au kupokea pesa, zawadi, huduma, au faida nyingine yoyote ya kifedha au ya kiuchumi kwa ajili ya kufanya kitendo kisichofaa au kukwepa kufanya kitendo ambacho kingefaa kufanywa.Katika kesi za uhujumu uchumi ambazo zinaathiri fedha za umma, kesi hizo zinaweza kusikilizwa na Mahakama ya Uhujumu Uchumi na Rushwa (The Economic and Corruption Court) ambayo ilianzishwa mwaka 2015 kusikiliza kesi za rushwa na uhujumu uchumi.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, nini chanzo cha rushwa ya ngono kwa wanahabari?

+

Rushwa ya ngono kwa wanahabari inachangiwa na mambo mengi, ikiwemo kupewa nafasi za kazi, au kuahidiwa kupandishwa cheo na mishahara yao kutoka kwa waajiri wao

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Je, ushawishi wa kujiondoa kugombea ni moja kati ya vitendo vya rushwa kipindi cha uchaguzi?

+

Sheria ya uchaguzi inatambua hili kama kosa kwani mtu anaweza kumshawishi mtu mwingine kujiondoa kugombea kwenye nafasi fulani kwa kumpa fedha au ahadi ya zawadi endapo atajiondoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je, sheria ya uhujumu uchumi ni nini?

+

Sheria ya uhujumu uchumi ni sheria inayolenga kudhibiti na kutoa adhabu kwa vitendo vya uhalifu katika uchumi kama vile utakatishaji wa fedha, rushwa, udanganyifu wa kifedha, na biashara haramu. Sheria hii inalenga kuhakikisha kuwa uchumi wa taifa unafanya kazi kwa uwazi na kwa njia ambayo inalinda maslahi ya umma. Sheria ya Uhujumu Uchumi hutumika katika nchi nyingi duniani kote na ina adhabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na faini, kifungo na hata kutaifishwa kwa mali iliyopatikana kwa njia za uhalifu.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je, shule zinashiriki vipi katika mapambano dhidi ya rushwa?

+

Shule kama sehemu maalumu ya kufikisha elimu katika jamii, pia zinatoa elimu kwa wanafunzi juu ya vitendo vya rushwa na athari zake kwa ujumla, ambapo wanafunzi hao wakirudi nyumbani huweza kuwaelimisha na wazazi/walezi wao juu ya vitendo vya rushwa na hatimae jamii yote kwa ujumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Je, makosa au kesi za uhujumu uchumi zinasikilizwa na mahakama gani?

+

Tanzania kuna mahakama mbalimbali zinazosikiliza kesi za uhujumu uchumi kulingana na kiwango cha kesi hiyo. Kwa mfano, kesi ndogo za uhujumu uchumi hushughulikiwa na mahakama za mwanzo (Primary Court), wakati kesi za kiwango cha juu zaidi hushughulikiwa na mahakama za juu kama vile Mahakama Kuu (High Court).

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Je, uchumi unahujumiwa kivipi?

+

Uchumi unahujumiwa pale ambapo watu wenye dhamana ya kusimamia sheria za uchumi, na sela za uchumi wan chi, mfano kushindwa kukusanya kodi au kukusanya kodi kwa lengo la kujinufaisha , au mtu mwingine yoyote akishindwa kutekeleza wajibu wake kama inavyo elekezwa na katiba ya nchi na sheria za uchumi kwa ujumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Uhujumu uchumi ni nini?

+

Uhujumu uchumi ni vitendo vinavyofanywa kwa makusudi na watu au makundi ya watu kwa lengo la kusababisha uharibifu kwenye uchumi wa nchi au eneo fulani. Vitendo hivyo vinaweza kuwa pamoja na uhalifu wa kiuchumi kama vile rushwa, ufisadi, udanganyifu wa kifedha, na utakatishaji wa fedha haramu. Uhujumu uchumi unaweza kusababisha hasara kubwa kwa uchumi wa nchi au eneo husika, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa pato la taifa, kuongezeka kwa umaskini, na kuharibika kwa miundombinu ya kiuchumi. Kwa hiyo, uhujumu uchumi ni suala kubwa ambalo linahitaji jitihada za pamoja kutoka kwa serikali, asasi za kiraia, na jamii kwa ujumla ili kupunguza athari zake.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je, uhujumu uchumi unaweza kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu?

+

Ukizungumzia haki za binadamu kama zilivyo ainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, pamoja na sheria zingine za kimataifa, wahujumu uchumi hushindwa kuziheshimu hasa haki ya kufanya kazi, haki ya kumiliki mali, na hatimaye kuvunjwa kwa haki hizo na zingine nyingi.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Je, vitendo vya rushwa vinaweza kupunguza uaminifu?

+

Vitendo vya rushwa huweza kupunguza uaminifu hata kuondoa kabisa uaminifu, kwani mtu anaejihusisha na vitendo vya rushwa atashindwa kuaminiwa eneo la kazi au hata katika jamii inayo mzunguka kwa ujumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Je, nini hasa chanzo cha rushwa?

+

vyanzo vya rushwa kimsingi ni vingi lakini kwa uchache zaidi rushwa inaweza kuchangiwa na tamaa, kukosa maadili, kutokutii miiko ya kazi, ujinga.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je, vyombo vya habari vinawezaje kushiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa?

+

Vyombo vya habari kama nguzo pekee ya kufikisha taarifa mbali mbali za matukio katika jamii, pia vinaweza kushiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Je, vyombo vya habari navyo vinaweza kuhusika na vitendo vya rushwa?

+

Vyombo, vya habari vinahusika na vitendo vya rushwa kwani hasa kunapokuwa na vitendo vya rushwa eneo flani vyombo vya habari huweza kupewa rushwa na wahusika ili wasiweze kuripoti taarifa hizo za rushwa katika maeneo husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je, wanafunzi wanashiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa?

+

Wanafunzi kama nyenzo mojawapo ya kufikisha elimu kwenye jamii, wanashiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwani hushiriki katika midahalo mbali mbali inayoendeshwa mashuleni juu ya elimu ya rushwa, na wengi wao hujiunga katika klabu mbali mbali zinazotoa elimu juu ya vitendo vya rushwa na hatimae kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Je, wanafunzi mashuleni wameitikiaje katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa?

+

Wanafunzi kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi nchini wamekuwa na mwitikio chanya katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwani wamekuwa wakitumia elimu wanayoipata kuweza kuripoti vitendo vya rushwa pale vinapojitokeza, katika mamlaka husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Je, wanahabari hao wanaripoti vitendo vya rushwa ya ngono maeneo husika?

+

Wengi wao wanashindwa kuripoti vitendo vya rushwa kwa hofu ya kufukuzwa kazi, kunyanyapaliwa, aibu, lakini pia wengine hushindwa kutoa taarifa kwa hofu ya kuzodolewa na wafanyakazi wenzao, kujengewa chuki na visasi na waajiri wao na ukizingatia wengi wanafanya kazi kama vibarua.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand