Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je, chama cha wafanyakazi au chama cha waajiri kinatakiwa kujisajili kwa mujibu wa sheria ndani ya muda gani baada ya kuanzishwa?

+

Chama cha wafanyakazi au chama cha waajiri kinatakiwa kujisajili kwa mujibu wa sheria ndani ya miezi sita (6) baada ya kuanzishwa kwake.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, ni lazima kwa mfanyakazi kuwa mwanachama wa chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, mfanyakazi halazimishwi kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, mkataba wowote wa ajira ni lazima uwe katika maandishi kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, mkataba wa ajira si lazima uwe katika maandishi isipokuwa kama mwajiriwa kwa mujibu wa mkataba huo atafanyia kazi nje ya Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, ni halali wafanyakazi kuwafanyia vurugu au kuwashambulia wafanyakazi wengine?

+

Hapana, si halali wafanyakazi kuwashambulia au kuwafanyia vurugu wafanyakazi wengine. Hii ni kwasababu ya kukuza mazingira yasiyo ya kibaguzi.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Wakati mkataba wa ajira unapoisha, mwajiri anatakiwa kisheria kumlipa mwajiriwa malipo ya kuachishwa kazi angalau yanayolingana na mshahara wa siku saba kwa kila mwaka kamili wa kuwa katika ajira mfululizo kwa mwajiri huyo hadi miaka isiyozidi kumi (kiinua mgongo). Je, ni kwa mazingira gani mwajiri anaweza kutotakiwa kulipa malipo hayo kisheria?

+

i. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kabla ya kuisha mwaka wa kwanza wa ajira ii. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kihalali kwa sababu za mwenendo mbaya iii. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kwa sababu za kukosa uwezo au kutohitajika

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Kwa kawaida, kosa la kwanza la mwajiriwa haliwezi kuhalalisha kuachishwa kazi na mwajiri wake. Lakini kuna wakati ambapo kosa la kwanza tu la mwajiriwa linaweza kupelekea akaachishwa kazi moja kwa moja na kuachishwa kazi huko kukawa halali mbele ya sheria. Je, ni wakati gani mwajiriwa anaweza kuachishwa kazi kwa kosa la kwanza na ikawa halali kisheria?

+

Kosa la kwanza la mwajiriwa linaweza kuhalalisha kuachishwa kazi kama itathibitika kuwa uvunjaji wa sheria ni mkubwa kiasi kwamba utafanya uhusiano katika ajira uwe mgumu kuendelea.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Unaelewaje maana ya “kuachishwa kazi kusiko kwa haki”?

+

Kuachishwa kazi kusiko kwa haki ni kitendo cha mwajiri au mwakilishi wa mwajiri kumwachisha kazi mfanyakazi (mwajiriwa) kwa sababu ambazo si halali kwa mujibu wa sheria au sababu ambazo si za haki kisheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Kwa kawaida, mwajiri hatakiwi kumtaka mfanyakazi kurudisha malipo ya ujira. Lakini kuna mazingira ambapo mfanyakazi inabidi arudishe malipo ya ujira. Je, mazingira hayo ni yapi?

+

Mfanyakazi anatakiwa kurudisha malipo ya ujira kama alizidishiwa na mwajiri hapo awali kutokana na makosa katika kukokotoa ujira wake au amekiri mwenyewe kupokea kiasi zaidi ya ujira ambao anatakiwa kupokea kwa kawaida.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Kila mfanyakazi ana haki kisheria kushiriki katika mgomo au kugoma kuhusiana na mgogoro wa maslahi. Je, ni sababu zipi zinaweza kumfanya mwajiriwa achukuliwe hatua za kinidhamu baada ya kugoma kuhusiana na mgogoro wa maslahi?

+

Mfanyakazi anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kugoma kuhusiana na mgogoro wa maslahi kama mfanyakazi anabanwa na makubaliano halali yanayotaka jambo linalobishaniwa kati yake na mwajiri kupelekwa katika usuluhishi, suala linalobishaniwa ni malalamiko, mfanyakazi husika anabanwa na mkataba wa hiyari unaoratibu jambo hilo linalobishaniwa, na sababu zingine kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Mfanyakazi ambaye ni mwanamke aliyejifungua ana haki ya kupewa muda wakati wa saa za kazi kumnyonyesha mtoto. Je, anatakiwa kupewa muda gani wa kumnyonyesha mtoto wake wakati wa saa za kazi?

+

Mfanyakazi mwenye mtoto anayenyonya anatakiwa kupewa muda wa kumnyonyesha mtoto wake wakati wa saa za kazi kwa jumla ya masaa mawili kwa siku.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Kwa mujibu wa sheria, mwajiri anatakiwa kusajili mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi. Je, mpango huo husajiliwa kwa nani au kwenye ofisi gani?

+

Mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi husajiliwa kwa Kamishna wa Kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, sheria inasemaje kuhusu mwajiri kumtaka mfanyakazi kufanya kazi kwa masaa zaidi ya matano kwa siku?

+

Mwajiri kumtaka mfanyakazi kufanya kazi kwa masaa zaidi ya matano inaruhusiwa kisheria. Hairuhusiwi mwajiri kumtaka mwajiriwa kufanya kazi masaa zaidi ya kumi na mbili (12) kwa siku.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je, mwajiriwa ana haki gani kisheria pale ambapo mwajiri wake anafanya ajira kushindwa kuvumilika?

+

Mwajiriwa ana haki ya kujiuzulu muda wowote kama mwajiri wake anafanya ajira kushindwa kuvumilika na kujiuzulu huko kunakuwa sawa na kuacha kazi kwa kulazimika.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Kiujumla, mwajiri anatakiwa kutoa taarifa kwa mwajiriwa anapotaka kusitisha mkataba wa ajira. Je, kuna mazingira yoyote kisheria ambapo mwajiri anaweza kusitisha mkataba bila kutoa taarifa kwa mwajiriwa? Yapi?

+

Ndiyo, kuna wakati mwajiri anaweza kusitisha mkataba wa ajira bila kutoa taarifa kwa mwajiriwa hususani kama mwajiriwa amevunja kiini cha mkataba (kuvunja mkataba kimsingi). Hii ni pale ambapo mwajiriwa ameshindwa kutimiza sharti la msingi katika mkataba.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je, mfanyakazi ana haki ya kupandishwa cheo?

+

Ndiyo, mfanyakazi ana haki ya kupandishwa cheo kazini.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Mwajiri anaweza kumsimamisha kazi mwajiriwa pale ambapo kuna tuhuma kali za mwenendo mbaya au kukosa uwezo kwa mwajiriwa husika zinafanyiwa uchunguzi. Je, katika wakati huo wa kuachishwa kazi kupisha uchunguzi, mwajiri ana wajibu wa kumlipa mshahara kamili bila punguzo lolote mwajiriwa?

+

Ndiyo, mwajiri anatakiwa kumlipa mshahara kamili bila punguzo lolote mwajiriwa baada ya kumsimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma kali za kukosa uwezo au mwenendo mbaya dhidi ya mwajiriwa huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Baadhi ya mikataba ya ajira huwa haioneshi ukomo wa mkataba. Je, katika hali kama hii, mwajiriwa anaruhusiwa kuacha kazi muda wowote?

+

Ndiyo, mwajiriwa anaruhusiwa kuacha kazi muda wowote pale ambapo mkataba hauoneshi kikomo. Mwajiriwa atatakiwa kutoa taarifa ya kuacha kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je, ni wajibu wa nani kuthibitisha kuwa ubaguzi dhidi ya mfanyakazi haukufanyika pale ambapo mwajiriwa ameshtaki kuwa amefanyiwa ubaguzi kwa sababu yoyote na mwajiri wake?

+

Ni wajibu wa mwajiri kuthibitisha kuwa ubaguzi unaolalamikiwa haukufanyika.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Juhudi za kurekebisha nidhamu zinatakiwa kuchukuliwa na kutumiwa kurekebisha tabia za wafanyakazi kwa kutumia mfumo wa kupanga hatua za nidhamu kama vile unasihi na maonyo. Je, nini lengo au nia ya maonyo kwa mwajiriwa?

+

Nia au lengo la maonyo kwa mwajiriwa ni kumtaarifu kuwa akitenda tena kosa kama hilo inaweza kusababisha kuchukuliwa hatua kali zaidi za kinidhamu.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Je, ni sahihi mwajiri kumkata mshahara mwajiriwa wake kwa sababu ya likizo ya uzazi?

+

Sheria inaelekeza kuwa mfanyakazi anatakiwa kupewa likizo ya uzazi yenye malipo. Hivyo, si sahihi mwajiri kukataa kumlipa mwajiriwa kwa sababu hakufanya kazi wakati wa likizo ya uzazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Mtoto ana haki ya kuajiriwa. Je, sheria inasema ni mtoto mwenye umri wa miaka mingapi anaweza kuajiriwa?

+

Sheria inaelekeza wazi kuwa mtoto anayeweza kuajiriwa ni yule ambaye ana umri wa miaka kuanzia kumi na nne (14) na zaidi. Hairuhusiwi mtu yeyote kumwajiri mtoto aliyeko chini ya miaka kumi na nne (14). Mtoto huyo anaruhusiwa kuajiriwa kwenye kazi ambazo ni halali na nyepesi kutokana na umri wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je, sheria inasemaje kuhusu suala la chama chochote cha wafanyakazi kumbagua mwanachama yeyote wakati wa kumwingiza, uwakilishi au kumfuta uanachama?

+

Chama cha wafanyakazi hakiruhusiwi kisheria kumbagua mwanachama kwa misingi yoyote katika kuingiza, uwakilishi au kufuta uanachama.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je, ni sahihi mwanamke mjamzito kulazimishwa na mwajiri wake kufanya kazi usiku miezi miwili kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua?

+

Hapana si sahihi mwajiri kumtaka mwajiriwa ambaye ni mwanamke mjamzito kufanya kazi usiku miezi miwili kabla ya siku tarajiwa ya kujifungua.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Sheria inaelekeza kuwa ni kosa kumpa mtu kazi ya lazima. Je, hii inajumuisha kazi inayotolewa kwa mtu ikiwa ni matokeo ya kutiwa hatiani na mahakamaa?

+

Hapana, hii haijumuishi mtu kupewa kazi na mahakama baada ya kutiwa hatiani kwa kosa lolote.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini zinamruhusu mwajiri kumwachisha kazi mwajiriwa bila kufuata masharti ya mkataba wa ajira?

+

Hapana, kanuni ya jumla inamtaka mwajiri kufuata masharti ya mkataba wa ajira katika kumwachisha kazi mwajiriwa wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je, kuchukua hatua za kiupendeleo ili kuleta usawa au kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi ni mojawapo ya aina za ubaguzi katika sehemu ya kazi kwa mujibu wa sheria?

+

Hapana, kuchukua hatua za kiupendeleo ili kuleta usawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi si mojawapo ya aina za ubaguzi kazini.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Je, mwajiri ana haki ya kumtaka mfanyakazi kufanya kazi masaa ya ziada bila kuwepo kwa makubaliano hayo?

+

Hapana, mwajiri hatakiwi kumtaka mfanyakazi kufanya kazi masaa ya ziada isipokuwa kama kuna makubaliano hayo

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Kila mfanyakazi ana haki ya kupewa likizo yenye malipo. Je, mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini ana haki ya kupata likizo yenye malipo?

+

Hapana, Sheria inatoa kanuni ya jumla kuwa mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini hana haki ya kupata likizo yenye malipo.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, ni sahihi mfanyakazi aliyejifungua kulazimishwa na mwajiri kurudi kazini ndani ya wiki mbili baada ya mtoto wake kuzaliwa?

+

Hapana, si sahihi. Mfanyakazi aliyejifungua hatakiwi kufanya kazi ndani ya wiki sita baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake, labda tabibu awe amethibitisha kuwa anaweza kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Kwa kawaida, mwajiri hatakiwi kufanya makato yoyote kutoka kwenye ujira wa mfanyakazi. Lakini kuna nyakati ambazo hili linaruhusiwa. Je, ni nyakati gani hizo?

+

i. Kama makato yanakubaliwa au yanaruhusiwa chini ya sheria iliyoandikwa, mkataba wa hiari, upangaji wa mishahara, amri ya mahakama au tuzo ya usuluhishi; ii. Kama mfanyakazi anadaiwa (yaani ana deni) na amekubali kwa maandishi kukatwa kuhusiana na deni hilo alilo nalo.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Kwa ujumla, kisheria ni kwamba mwajiri hatakiwi kumwachisha kazi mfanyakazi wake kwa sababu ya ugonjwa au kuumia kazini. Lakini kuna mazingira sababu ya ugonjwa au kuumia kazini inaweza kuwa halali kumwachisha kazi mfanyakazi. Je, ni kwa mazingira gani sababu ya ugonjwa au kuumia kazini inaweza kuwa sababu halali ya kumwachisha kazi mfanyakazi?

+

i. Kama mfanyakazi husika hana uwezo wa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa ii. Kukosa uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu (kukosa uwezo wa kufanya kazi kwa kudumu)

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Wakati mkataba wa ajira unapoisha, mwajiri anatakiwa kisheria kumlipa mwajiriwa malipo ya kuachishwa kazi angalau yanayolingana na mshahara wa siku saba kwa kila mwaka kamili wa kuwa katika ajira mfululizo kwa mwajiri huyo hadi miaka isiyozidi kumi (kiinua mgongo). Je, ni kwa mazingira gani mwajiri anaweza kutotakiwa kulipa malipo hayo kisheria?

+

i. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kabla ya kuisha mwaka wa kwanza wa ajira ii. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kihalali kwa sababu za mwenendo mbaya iii. Kama mwajiriwa ameachishwa kazi kwa sababu za kukosa uwezo au kutohitajika

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Unadhani ni vitendo gani vinaweza kufanywa na mwajiriwa na kufanya mwajiri kumwachisha kazi mwajiriwa huyo na uachishwaji huo ukawa ni halali mbele ya sheria?

+

i. Kama mwajiriwa huyo amefanya udanganyifu mkubwa ii. Kama mwajiriwa amefanya uharibifu wa mali kwa makusudi iii. Kama mwajiriwa anahatarisha usalama wa watu wengine kwa makusudi iv. Kama mwajiriwa ana uzembe mkubwa kazini v. Kuonyesha dharau kubwa isiyovumilika katika hali ya kawaida

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Waajiri hufanya vitendo gani ambavyo huhusisha kuvunja kiini cha mkataba wa ajira, hivyo hatimaye hupelekea baadhi ya waajiriwa kukomesha mkataba haraka?

+

i. Kukataa kulipa mishahara ii. Udhalilishaji kwa maneno au vitendo au vitendo au unyanyasaji wa kijinsia iii. ubaguzi usio wa haki

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Kuna aina mbili za kutokukidhi matakwa ya kazi kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), za mwaka 2007. Kuna aina mbili za kutokukidhi matakwa ya kazi kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), za mwaka 2007.

+

i. Kutokukidhi matakwa ya kazi kwa mwajiriwa katika kazi yake kutokana na sifa au tabia yake, ii. Kutokukidhi matakwa ya kazi kwa mwajiriwa katika mazingira yake ya kazi akiwa na uhusiano mbaya na wafanyakazi wenzake, wateja au watu wengine ambao ni muhimu katika biashara hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Kuna wakati masaa ya kupumzika ya mwajiriwa yanaweza kupunguzwa kutoka kumi na mawili mpaka nane. Taja mazingira ambayo yanaweza kupelekea kufanya hivyo.

+

i. Lazima kuwe na makubaliano ya maandishi baina ya mwajiri na mwajiriwa ii. Kama mwajiriwa anaishi maeneo hayo hayo ya kazi

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Ni zipi aina za mkataba kwa mujibu wa sheria?

+

i. Mkataba kwa kipindi cha muda ambao haujatajwa, ii. Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za wataalamu na mameneja, iii. Mkataba wa kazi maalum.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Mkataba wa ajira huweza kukoma muda wowote kutokana na sababu mbalimbali. Sababu zipi ambazo zinaweza kufanya mkataba wa ajira kukoma wenyewe?

+

i. Mkataba wa ajira unaweza kukoma kwasababu ya kifo (yaani pale mfanyakazi anapofariki). ii. Mkataba wa ajira unaweza kukoma wenyewe pale mwajiri anapopoteza utaalamu wa shughuli husika. iii. Mkataba wa ajira unaweza kukoma wenyewe pale ambapo mwajiriwa ametimiza umri uliokubaliwa au wa kawaida wa kustaafu.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Ni mambo gani mfanyakazi akifanyiwa na mwajiri wake unaweza kusema kuwa ameachishwa kazi na mwajiri wake?

+

i. Pale ambapo mwajiri amesababisha iwe vigumu kwa mwajiriwa kuendelea na kazi, ii. Pale ambapo mwajiri amekataa kumruhusu mwajiriwa kurejea kazini baada ya likizo ya uzazi au ulezi n.k.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je, ni njia gani za kumwachisha kazi mwajiriwa ambaye baada ya kufikisha umri wake wa kustaafu ameendelea na kazi?

+

Kanuni za kawaida za kumwachisha kazi mwajiriwa hutumika isipokuwa kama mwajiri na mwajiriwa wakikubaliana jambo lingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je, mwajiri anaweza kuwaachisha kazi waajiriwa waliofanya mgomo wakafanya uvunjifu wa amani kwa kufanya vurugu na uharibifu mkubwa wa mali?

+

Kanuni zinaelekeza kuwa kinga waliyo nayo wafanyakzi kufanya mgomo bila kuachishwa kazi haikingi dhidi ya mwenendo mbaya unaohusiana na mgomo kama vile vurugu na uharibifu mkubwa wa mali. Hivyo, mwajiri anaweza kuwaachisha kazi wafanyakazi hao.

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je, Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini zinasemaje kuhusu suala la vyama vya wafanyakazi kumbagua mfanyakazi kujiunga na chama kwa sababu ya mahali anapotoka?

+

Kanuni zinaelekeza wazi kuwa vyama vya wafanyakazi havipaswi kumbagua mfanyakazi yeyote kujiunga na chama husika kwa kigezo cha mahali atokapo.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Wafanyakazi wana haki ya kufanya mgomo. Je, ni kwa wakati gani jeshi la polisi linaweza kuingilia kati wakati wa mgomo wa wafanyakazi?

+

Kwa mujibu wa kanuni, polisi wanaweza kuingilia kati tu kama kuna uvunjifu wa amani au sheria, hasa kama kuna tishio la vurugu au uharibifu wa mali

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Wafanyakazi wana haki ya kufanya mgomo. Je, ni kwa wakati gani jeshi la polisi linaweza kuingilia kati wakati wa mgomo wa wafanyakazi?

+

Kwa mujibu wa kanuni, polisi wanaweza kuingilia kati tu kama kuna uvunjifu wa amani au sheria, hasa kama kuna tishio la vurugu au uharibifu wa mali

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Unaelewa nini maana ya likizo ya mwaka?

+

Likizo ya mwaka ni muda wa mapumziko usiopungua siku ishirini na nane (28) mfululizo ambao mwajiri anatakiwa kutoa kwa mfanyakazi wake kuhusiana na kila mzunguko wa likizo. Likizo hii hutolewa kila mwaka.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Mfanyakazi ana haki ya kupewa likizo ya mwaka yenye malipo kwa mujibu wa sheria. Je, likizo ya mwaka ni siku ngapi kisheria?

+

Likizo ya mwaka ni siku zisizopungua ishirini na nane (28) mfululizo.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je, likizo ya uzazi kwa mwanaume mwajiriwa huwa ni siku ngapi kwa mujibu wa sheria?

+

Likizo ya uzazi kwa mwanaume inatakiwa kuwa walau siku tatu (3).

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Unaelewa nini maana ya likizo ya uzazi?

+

Likizo ya uzazi ni muda wa mapumziko anaopewa mwanamke mwajiriwa kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua au mwanaume mwajiriwa baada ya mke wake kujifungua.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Unaelewaje maana ya “Mahakama ya Kazi”?

+

Mahakama ya Kazi ni Divisheni ya Kazi ya Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo huhusika na kesi za masuala ya kazi tu hapa nchini Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Kuna wizara mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kila wizara ina majukumu yake ya msingi. Je, unadhani masuala ya kazi hapa nchini Tanzania yanashughulikiwa chini ya wizara gani?

+

Masuala ya kazi yanashughulikiwa chini ya Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Mapumziko kazini ni suala la msingi sana kwani hupumzisha akili na viungo vya mwili. Hivyo, mwajiri pia ana wajibu wa kumpa mapumziko mfanyakazi ambaye amefanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa tano. Je, mfanyakazi anatakiwa kupewa muda gani wa mapumziko baada ya kufanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa tano?

+

Mfanyakazi ana haki ya kupewa mapumziko ya muda usiopungua dakika sitini (60) baada ya kufanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa tano.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Je, mfanyakazi ambaye ni mwanamke mjamzito anaweza kuanza likizo ya uzazi muda gani baada ya kutoa taarifa kwa mwajiri wake kwa mujibu wa sheria?

+

Mfanyakazi huyo anaweza kuanza likizo yake ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne (4) kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua au katika tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Je, Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini zinasemaje kuhusu ubaguzi dhidi ya mfanyakazi mwenye Virusi vya UKIMWI?

+

Mfanyakazi mwenye Virusi vya UKIMWI hatakiwi kubaguliwa kwa namna yoyote na mwajiri wake, waajiriwa wenzake wala Chama cha Wafanyakazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Unaelewa nini kuhusu \"mkataba wa ajira\"?

+

Mkataba wa ajira ni makubaliano (yenye nguvu ya kisheria) kati ya pande mbili ambapo mmoja anakubali kumfanyia kazi upande mwingine kwa ahadi ya kulipwa kiasi cha fedha au kitu kingine kwa mujibu wa makubaliano.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Je, muda wa majaribio unatakiwa usizidi muda gani kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini?

+

Muda wa majaribio unatakiwa usizidi miezi kumi na mbili (yaani usizidi mwaka mmoja).

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je, mwajiri anapaswa kufanya nini wakati wa kipindi cha majaribio kwa mwajiriwa?

+

Mwajiri anapaswa kufuatilia na kutathmini ufanisi na kufaa kwa mwajiriwa muda hadi muda na kukutana na waajiriwa mara kwa mara ili kujadili tathmini ya waajiriwa na kutoa mwongozo pale inapobidi. Mwongozo huo unaotolewa na mwajiri unaweza kuwa maagizo, mafunzo na ushauri kwa mwajiriwa wakati wa majaribio.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Kanuni ya jumla inampa haki mwajiri ya kutowajibika kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko. Lakini kuna mazingira ambayo mwajiri anaweza kutakiwa kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko. Je, ni mazingira gani hayo?

+

Mwajiri anatakiwa kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko kama mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi au kuwepo kwa ajili ya kazi wakati wa mapumziko.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Kwa kawaida siku moja ina masaa ishirini na nne. Je, mwajiri anatakiwa kumpa mwajiriwa masaa mangapi mfululizo ya kupumzika baada ya kumaliza kazi kwa siku moja na kabla ya kuanza tena kazi?

+

Mwajiri anatakiwa kumpa mwajiriwa muda wa masaa kumi na mbili mfululizo ya kupumzika kwa kila siku baada ya muda wa kuanza mapumziko na kabla ya kuanza kazi kwa mara nyingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Taja mambo matatu ambayo mwajiri inabidi ayazingatie kabla ya kumwachisha kazi mwajiriwa ambaye yuko katika kipindi cha majaribio.

+

Mwajiri anatakiwa kumpa taarifa mwajiriwa kuhusiana na mashaka aliyo nayo mwajiri juu ya utendaji kazi wake (mwajiriwa), mwajiri anatakiwa kumpatia mwajiriwa fursa ya kujibu mashaka hayo ya mwajiri na pia mwajiri anapaswa kumpatia mwajiriwa muda wa kutosha kuongeza ufanisi au kurekebisha tabia na ameshindwa kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Taja mambo matatu ambayo mwajiri inabidi ayazingatie kabla ya kumwachisha kazi mwajiriwa ambaye yuko katika kipindi cha majaribio.

+

Mwajiri anatakiwa kumpa taarifa mwajiriwa kuhusiana na mashaka aliyo nayo mwajiri juu ya utendaji kazi wake (mwajiriwa), mwajiri anatakiwa kumpatia mwajiriwa fursa ya kujibu mashaka hayo ya mwajiri na pia mwajiri anapaswa kumpatia mwajiriwa muda wa kutosha kuongeza ufanisi au kurekebisha tabia na ameshindwa kufanya hivyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Kanuni ya jumla inasema kuwa mwajiri hatakiwi kumtaka mfanyakazi kufanya kazi muda wa mapumziko, lakini kuna mazingira yametajwa na sheria kuwa mwajiri anaweza kumtaka mfanyakazi kufanya kazi wakati wa mapumziko. Je, ni mazingira gani hayo?

+

Mwajiri anaweza kumtaka mfanyakazi kufanya kazi wakati wa mapumziko ikiwa tu kama kazi hiyo haiwezi kufanywa na mfanyakazi mwingine.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je, unadhani ni kwa mazingira gani mwajiri hatakiwi kumlipa mfanyakazi kwa ajili ya likizo ya ugonjwa?

+

Mwajiri hatakiwi kumlipa mfanyakazi kwa ajili ya likizo ya ugonjwa kama mfanyakazi husika ameshindwa kuwasilisha cheti cha matibabu kilichotolewa na tabibu aliyesajiliwa au tabibu yeyote mwingine anayekubalika na mwajiri, na ambacho kukubalika kwake hakutakiwi kukataliwa bila sababu za msingi.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je, mwajiri anaweza kufanya nini iwapo hajaweza kuchunguza kwa makini kama mwajiriwa ana uwezo wa kufanya kazi au anafaa kwa ajira husika baada ya muda wa majaribio kuisha?

+

Mwajiri ikiwa hajaweza kuchunguza kwa makini kama mwajiriwa aliyeko katika muda wa majaribio ana uwezo wa kufanya kazi husika anaweza kuongeza muda wa majaribio kwa kipindi cha kutosha baada ya kufanya mashauriano na mwajiriwa husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je, nani mwenye wajibu wa kuthibitisha mbele ya mahakama au taasisi yoyote ya usuluhishi kuwa uachishwaji kazi uliofanywa na mwajiri dhidi ya mwajiriwa ulikuwa wa haki?

+

Mwajiri ndiye anatakiwa kuthibitisha kuwa kuachishwa kazi kwa mfanyakazi wake kulikuwa kwa haki.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Nani ana jukumu, kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini, la kuhakikisha kuwa kunakuwepo fursa sawa mahali pa kazi?

+

Mwajiri ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kuwa kunakuwepo fursa sawa mahali pa kazi bila ubaguzi wowote.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Mwajiriwa wa kiume ambaye amefiwa na mtoto au mke wake ana haki ya kupewa likizo. Je, likizo baada ya kifo cha mtoto au mke wa mwajiriwa hutakiwa kuwa siku ngapi kisheria?

+

Mwajiriwa anatakiwa kupewa likizo ya siku zisizopungua nne (4) baada ya kufiwa na mtoto au mke wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Mwajiriwa ana haki ya kupumzika na kutofanya kazi sikukuu za umma kama vile siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu Nyerere (Rais wa kwanza wa Tanzania) na Siku ya Uhuru. Je, mwajiriwa huyo atakuwa na haki gani kama akifanya kazi sikukuu za umma?

+

Mwajiriwa atakuwa na haki ya kulipwa mara mbili ya ujira wa kawaida kwa kila saa atakayofanya siku hiyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je, mfanyakazi ambaye ni mwanamke aliyejifungua watoto mapacha (wawili) anatakiwa kupewa siku ngapi za likizo ya uzazi?

+

Mwanamke ambaye ni mfanyakazi aliyejifungua watoto mapacha anatakiwa kupewa siku mia moja (100) za likizo ya uzazi yenye malipo.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Uthibitisho ni jambo la msingi sana katika masuala mbalimbali. Je, unadhani mwanamke mjamzito anaweza kuleta uthibitisho gani unaokubalika kisheria ili mwajiri wake aamini kuwa ana ujauzito na kuweza kumpa likizo ya uzazi?

+

Mwanamke mjamzito anaweza kuleta cheti cha tabibu aliyemfanyia vipimo kuthibitisha kuwa ana ujauzito.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Mwanaume ana haki ya kupewa likizo ya uzazi baada ya mkewe kujifungua. Je, likizo hiyo anatakiwa kuichukua ndani ya muda gani baada ya mtoto kuzaliwa?

+

Mwanaume mwajiriwa ana haki ya kupata likizo ya uzazi ndani ya siku saba tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Mkataba wa ajira unatakiwa kumtaka au kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi mpaka masaa kumi na mbili kwa siku. Je, hii inajumuisha muda wa kula?

+

Ndiyo, hii inajumuisha muda wa kula wa mfanyakazi husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je, inaruhusiwa kisheria mwajiri na mwajiriwa kukubaliana kusitisha mkataba wa ajira?

+

Ndiyo, inaruhusiwa kisheria mwajiri na mwajiriwa kusitisha mkataba kwa makubaliano maalum.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je, Kamishna wa Kazi ana mamlaka kisheria kumtaka mwajiri yeyote kutayarisha mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi?

+

Ndiyo, Kamishna wa Kazi amepewa mamlaka na sheria kumtaka mwajiri yeyote kutayarisha mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi na kusajili huo mpango kwa Kamishna.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Ubaguzi hauruhusiwi katika sehemu ya kazi. Je, kudhalilishwa kwa mfanyakazi ni aina ya ubaguzi kwa mujibu wa sheria?

+

Ndiyo, kudhalilishwa kwa mfanyakazi ni aina mojawapo ya ubaguzi dhidi ya mfanyakazi huyo.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je, kutokukidhi matakwa ya kazi kunaweza kuwa sababu ya mwajiriwa kuachishwa kazi?

+

Ndiyo, kutokukidhi matakwa ya kazi ni mojawapo ya sababu ya kuachishwa kazi kwa mwajiriwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je, mkataba wa ajira unaweza kukoma wenyewe pale ambapo mwajiriwa ametimiza umri uliokubaliwa au wa kawaida wa kustaafu?

+

Ndiyo, kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), za mwaka 2007, mkataba wa ajira unaweza kukoma wenyewe pale ambapo mwajiriwa ametimiza umri uliokubaliwa au wa kawaida wa kustaafu.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je, mwajiri ana wajibu wa kumpa fursa ya kujibu au fursa ya kujirekebisha mwajiriwa aliyeko katika kipindi cha majaribio baada ya kuona kuwa mwajiriwa huyo hafanyi kazi kufikia viwango au anaweza kuwa hafai kwa nafasi aliyo nayo?

+

Ndiyo, kwa mujibu wa Kanuni, mwajiri anatakiwa kumpatia fursa ya kujibu au kujirekebisha mwajiriwa aliyeko katika muda wa majaribio baada ya kuona kuwa hafanyi kazi au anaweza kuwa hafai katika kazi husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je, mwajiri ana wajibu wa kumpa fursa ya kujibu au fursa ya kujirekebisha mwajiriwa aliyeko katika kipindi cha majaribio baada ya kuona kuwa mwajiriwa huyo hafanyi kazi kufikia viwango au anaweza kuwa hafai kwa nafasi aliyo nayo?

+

Ndiyo, kwa mujibu wa Kanuni, mwajiri anatakiwa kumpatia fursa ya kujibu au kujirekebisha mwajiriwa aliyeko katika muda wa majaribio baada ya kuona kuwa hafanyi kazi au anaweza kuwa hafai katika kazi husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je, Mahakama ya Kazi ina mamlaka ya kumwamuru mwajiri kumrudisha mfanyakazi kazini na kulipwa mishahara yake yote aliyokosa baada ya kuona kuwa mfanyakazi aliachishwa kazi kinyume na haki yake kisheria?

+

Ndiyo, Mahakama ya Kazi ina mamlaka hayo kumwamuru mwajiri kumrudisha mwajiriwa wake kazini baada ya kuona kuwa uachishwaji kazi wa mwajiriwa huyo haukuwa wa haki kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je, mfanyakazi yeyote ana haki ya kujua kiwango cha mshahara wake kabla ya kuanza kazi?

+

Ndiyo, mfanyakazi ana haki ya kujua kiwango cha mshahara wake kabla ya kuanza kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Ni kawaida kwa mwajiri kuamua kupunguza idadi ya wafanyakazi. Je, mwajiri anapotaka kupunguza wafanyakazi ana wajibu wa kisheria kutoa taarifa kwa wafanyakazi wake wote?

+

Ndiyo, mwajiri ana wajibu wa kisheria kutoa notisi (taarifa) kwa wafanyakazi juu ya kusudio lake la kupunguza wafanyakazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je, mwajiri anaweza kuchukulia suala la vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa na baadhi ya wafanyakazi wake kama makosa ya kinidhamu na kuchukua hatua za kinidhamu?

+

Ndiyo, mwajiri anaruhusiwa kisheria kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wafanyakazi wanaofanya vitendo vya kibaguzi kwani vitendo vya kibaguzi ni makosa ya kinidhamu kazini.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je, mwajiri ana wajibu wa kumlipa mfanyakazi mshahara wa kipindi cha likizo ya mwaka?

+

Ndiyo, mwajiri anatakiwa kumlipa mwajiriwa mshahara wa kipindi cha likizo ya mwaka.

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Je, mwajiriwa aliyeko katika kipindi cha majaribio ana haki ya kujiunga katika chama cha wafanyakazi?

+

Ndiyo, mwajiriwa aliyeko katika kipindi cha majaribio ana haki pia ya kujiunga katika chama cha wafanyakazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Je, mwajiwa ambaye yuko kwenye kipindi cha majaribio ana haki ya kujua masharti kabla ya kuanza kazi?

+

Ndiyo, mwajiriwa ambaye yuko katika kipindi cha majaribio ana haki ya kujua masharti kabla ya kuanza kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Je, mfanyakazi ambaye ni mwanamke aliyejifungua ana haki ya kuongezewa siku zingine za likizo baada ya mtoto wake aliyezaliwa kufariki ndani ya mwaka mmoja? Je, ni siku ngapi?

+

Ndiyo, sheria inaelekeza kuwa mfanyakazi aliyejifungua ana haki ya nyongeza ya siku zingine themanini na nne (84) za likizo yenye malipo kama mtoto aliyezaliwa amefariki ndani ya mwaka mmoja wa kuzaliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je, wakati mfanyakazi amepewa likizo ya mwaka anatakiwa kulipwa mshahara wa kiasi ambacho angelipwa kama angekuwa anafanya kazi kwa muda huo?

+

Ndiyo, sheria inamtaka mwajiri kumlipa mfanyakazi wake akiwa katika likizo ya mwaka mshahara ule ule ambao angemlipa kama angekuwa anaendelea kufanya kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Je, sheria inasemaje kuhusu suala la kumlazimisha mtu kuajiriwa au kwa kumpa vitisho ili aajiriwe?

+

Ni kosa kutoa kazi ya lazima ikiwemo mtu kumtisha ili akubali kuajiriwa

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Je, ni wajibu wa nani kuandaa na kuchapisha mpango wa kuzuia ubaguzi na kukuza fursa sawa katika ajira mahali pa kazi?

+

Ni wajibu wa kila mwajiri kuandaa na kuchapisha mpango wa kuzuia ubaguzi na kukuza fursa sawa katika ajira mahali pa kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je, ni wajibu wa nani kuchukua hatua chanya katika kuhakikisha ujira sawa kwa wanaume na wanawake kwa kazi yenye thamani sawa?

+

Ni wajibu wa mwajiri kuhakikisha anachukua hatua chanya katika kuhakikisha ujira sawa kwa wanaume na wanawake kwa kazi yenye thamani sawa

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Pale ambapo mfanyakazi amelemazwa akiwa kazini, mwajiri hatakiwi kumwachisha kazi moja kwa moja hata kama ulemavu huo ni wa muda mrefu. Badala yake mwajiri anatakiwa kutumia njia zingine mbadala mbali na kumwachisha kazi. Je, njia hizo zinaweza kuwa kama zipi?

+

Njia hizo zinaweza kuwa kama kubadilishwa kwa mfanyakazi huyo aliyepata ulemavu kwa muda, kumpatia kazi nyepesi, kumpa kazi mbadala, kustaafu kabla ya wakati, pensheni na njia zingine zinazoweza kuwa nzuri kwa mujibu wa sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je, mwajiriwa anaweza kustaafu akiwa na umri gani pale ambapo hakuna umri wa kustaafu uliokubaliwa katika mkataba?

+

Pale ambapo hakuna umri uliokubaliwa wa kustaafu, mwajiriwa anaweza kustaafu katika umri wa kawaida wa kustaafu kulingana na taratibu za mwajiri siku za nyuma na taratibu za mahali pa kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Kwa kawaida huwa kunakuwa na kipindi cha majaribio kwa baadhi ya waajiriwa. Je, nini sababu ya kipindi cha majaribio kwa mujibu wa Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini?

+

Sababu ya kipindi cha majaribio kwa kawaida ni kumwezesha mwajiri kufanya tathimini ya kujua kama mwajiriwa ana uwezo wa kazi na anafaa katika ajira.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Je, ni sababu zipi zinatakiwa kuzingatiwa ili kufikia maamuzi kujua muda unaotosha wa kipindi cha majaribio?

+

Sababu zinazotakiwa kuzingatiwa kwa mujibu wa Kanuni ni aina ya kazi, viwango vinavyohitajika, utamaduni na taratibu katika sekta husika.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Mfanyakazi ana haki ya kupewa likizo ya ugonjwa ya angalau siku mia moja ishirini na sita (126) katika kila mzunguko wa likizo. Je, siku zote hizo 126 mfanyakazi anatakiwa kulipwa mshahara mzima wakati hafanyi kazi?

+

Sheria inaelekeza kuwa mfanyakazi hawezi kulipwa mshahara mzima kwa siku zote hizo. Badala yake, siku sitini na tatu (63) za kwanza ndizo zinatakiwa kulipwa mshahara na siku sitini na tatu (63) zinazofuata zinatakiwa kulipwa nusu mshahara.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Kwa mujibu wa sheria, imezuiliwa kkwa mwajiri kumtaka mwanamke mjamzito kufanya kazi usiku. Je, usiku unaomaanishwa hapa kwa mujibu wa sheria ni kuanzia saa ngapi mpaka saa ngapi?

+

Sheria inaelekeza kuwa usiku ni masaa baada ya saa mbili usiku na kabla ya saa kumi na mbili asubuhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Je, mfanyakazi ambaye ni mwanamke na anayetarajia kuchukua likizo yake ya uzazi anatakiwa kutoa taarifa kuhusiana na kusudio lake kwa mwajiri wake kwa muda gani kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua?

+

Sheria inamtaka mwanamke mjamzito kutoa taarifa kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi walau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua.

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Je, ni kosa kumlazimisha mtu kufanya kazi yoyote ambayo ni sehemu ya wajibu wa kawaida wa kiraia kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

+

Sheria inasema kuwa kumshawishi mtu au kumpa kazi ya lazima ambayo ni sehemu ya wajibu wake wa kiraia akiwa kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania si kosa.

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini pamoja na Kanuni zake inatumika kwa wafanyakazi wote nchini Tanzania lakini kuna makundi machache ambapo sheria hii haitumiki isipokuwa vifungu vichache tu. Je, makundi hayo ni yapi?

+

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini pamoja na kanuni zake haitumiki kwa makundi yafuatayo: i. Jeshi la Wananchi la Tanzania ii. Jeshi la Polisi iii. Jeshi la Magereza iv. Jeshi la Kujenga Taifa

Sheria Kiganjani
Learn More
100

Unaelewaje maana ya “Tume ya Upatanishi na Usuluhishi”?

+

Tume ya Upatanishi na Usuluhishi ni taasisi ambayo inashughulikia upatanishi na usuluhishi wa migogoro ya kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
101

Nani ni mdau wa masuala ya kazi na ajira hapa nchini Tanzania?

+

Wadau wa masuala ya kazi na ajira ni kama ni wafuatao: Waajiri, Waajiriwa, Serikali, Vyama vya wafanyakazi, Vyama vya waajiri, Mahakama na Taasisi mbalimbali za usuluhishi wa migogoro.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand