Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je Tanzania imesaini mkataba wa kimataifa wa haki za watoto?

+

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je sera ya Taifa ya Maendeleo ya Wanawake na jinsia ina malengo gani?

+

-Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Wanawake na jinsia ina malengo yafuatayo, -Kuweka mazingira muafaka yatakayowezesha wanawake na wanaume kutekeleza majukumu yao katika jamii kwa kuzingatia mahitaji yao kijinsia. -Kusawazisha mapungufu yanayojitokeza katika ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za maendeleo.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa inayolinda haki za wanawake?

+

-Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa inayolinda haki za wanawake kama, -Mkataba wa kimataifa wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 -Mkataba nyongeza wa Haki za Wanawake Barani Afrika wa mwaka 2003

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je sheria inaruhusu ndoa kwa wanawake wa umri gani?

+

Kwa mujibu kifungu namba 13 cha sheria ya ndoa, mwanamke mwenye umri wa miak kumi na tatu kwa idhini ya wazazi wake au mahakama anaweza kufunga ndoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je wanawake wanayo haki ya huduma ya elimu

+

Kwa mujibu wa ibara ya 11(1) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya elimu kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je wanawake wanao usawa mbele ya sheria?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 13 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanao usawa mbele ya sheria kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je wanawake wanayo haki ya afya?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya afya kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je mlemavu ana haki ya kuishi?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katika ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mlemavu anayo haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je mlemavu ana haki ya faragha?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 16 (1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, mlemavu kama walivyo watu wengine anayo haki ya faragha

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je wanawake wanayo haki ya faragha?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 16 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya faragha kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je sheria inasemaje kuhusu ukatili dhidi ya wanawake?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 16 ya katiba ya muungano wa Tanzania, ukatili dhidi ya wanawake hauruhusiwi. Pia, mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imekwisha isaini, inazuia ukatili dhidi ya wanawake.

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je wanawake wanayo haki ya kwenda mahali popote watakapo pasi kuvunja sheria za nchi?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 17 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya kwenda mahali popote watakapo pasi kuvunja sheria za nchi kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je mlemavu anahaki ya kutoa maoni?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 18 (a) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, mlemavu kama walivyo watu wengine anayo haki ya kutoa maoni.

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Je wanawake wanayo haki ya kutoa maoni?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 18 (a) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, wanawake kama walivyo watu wengine wanayo haki ya kutoa maoni.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je wanawake wanayo haki ya ajira?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 22(1) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya ajira kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je wanawake wanayo haki ya kupata ujira kwa kazi wanazofanya?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 23 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya kupata ujira kama walivyo watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je wanawake wanayo haki ya kumiliki mali?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 24 ya katika ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya kumiliki mali kama ilivyo kwa watu wengine. -Pia kifungu namba 56 cha sheria ya ndoa inatoa haki ya mwanamke kumiliki mali.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je wanawake wanayo haki ya kushiriki katika siasa?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 5 na ibara ya 20 ya Katiba Ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya kushiriki katika siasa kama ilivyo kwa watu wengine.

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Je wanawake wanayo haki ya kupiga kura?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 5 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, wanawake wanayo haki ya kupiga kura.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Je mlemavu ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi?

+

Kwa mujibu wa ibara ya 5 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mlemavu anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi. Pia kwa mujibu wa kifungu namba 51 (2) cha sheria ya watu wenye ulemavu , mlemavu anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Je mtu anayesadikika kuwa baba wa mtoto ana wajibu wa kutoa matunzo kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je mtoto ana haki ya dhamana?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 101 cha sheria ya mtoto, mtoto ana haki ya dhamana.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je mtoto anaweza kuweka kizuizini/rumande ya polisi pamoja na watu wazima?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 102 cha sheria ya mtoto, mtoto hapaswi kuwekwa rumande pamoja na watu wazima isipokuwa kama ni ndugu yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je mtoto ana haki ya kutoa mawazo?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 11 ya Sheria ya Mtoto, Mtoto anayo haki ya kutoa maoni yake, kusikilizwa na kushiriki katika utoaji maoni.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je wanawake wanayo haki ya mgawanyo wa mali pale nahakama inapotoa taraka?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 114 cha sheria ya ndoa, wanawake wanayo haki ya mgawanyo wa mali pale mahakama inapotoa taraka.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je wanawake wanayo haki ya kuendelea kutunzwa na wenzi wao kipindi wanapokuwa kwenye ndoa au wanapotengana?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 115 cha sheria ya ndoa, wanawake wanayo haki ya kuendelea kupokea matunzo kutokwa kwa wenzi wao kwa kipindi wawapo kwenye ndoa au wanapotengana.

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Je mtoto anaweza kutumikia kifungo cha gerezani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 119 (1) cha sheria ya mtoto, mtoto hawezi tumikia kifungo cha gerezani.

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Je Mahakama inaweza kuboresha au kubadilisha matakwa yaliyo katika amri ya matunzo?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 121 na 122 cha sheria ya ndoa, mahakama inao uwezo wa kubadilisha au kuboresha masharti ya amri ya matunzo kwa muda wowote kadri itavyo ionekana inafaa.

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je mtoto ana haki ya kuchagua uraia?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 13 cha sheria ya uraia, mtoto hana haki ya kuchagua uraia.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Je mtoto ana haki ya kukana uraia?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 13 cha sheria ya uraia, mtoto hana haki ya kukana uraia.

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Je mwanamke anaweza kushinikizwa kuishi na mume wake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 140 cha sheria ya ndoa, mwanamke hawezi kushinikizwa kuishi na mume wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Je ni sifa zipi za mtoto anaye hitaji uangalizi maalumu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 16 cha sheria ya mtoto, mtoto anahitaji uangalizi maalumu endapo akiwa na sifa zifuatazo, -Mtoto yatima -Mtoto aliye na wazazi au walezi wasiotoa malezi bora -Mtoto aliye chini ya malezi ya wazazi au walezi ambao ni walevi au kwa sababu za kiuhalifu hawafai kuishi na mtoto huyo. -Mtoto ambaye anatendewa ukatili na wazazi au walezi wake -Mtoto ambaye anahusishwa na ukahaba au kuishi na walezi au wazazi wanaotuhumiwa kufanya ukahaba.

Sheria Kiganjani
Learn More
33

Je nani mwenye uwezo wa kupeleka ombi la mtoto kuwa katika uangalizi maalumu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 18 cha sheria ya mtoto, afisa ustawi wa jamii ndiye mwenye mamlaka ya kupeleka maombi mahakamani ya mtoto kuwa katika uangalizi maalumu.

Sheria Kiganjani
Learn More
34

Je ni chombo kipi chenye mamlaka ya kutoa amri ya mtoto kuwekwa kwenye uangalizi maalumu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 18 cha sheria ya Mtoto, Mahakama yoyote yaweza kutoa amri ya mtoto kuwekwa katika uangalizi maalumu.

Sheria Kiganjani
Learn More
35

Je mtoto ana haki gani endapo wazazi wakitengana?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 26(1) cha sheria ya Mtoto, mtoto anazo hazi zifuatazo endapo wazazi wake wakitengana -Kuendelea kupatiwa elimu bora kama aliyokuwa akipatiwa na wazazi wake kabla ya kutengana. -Kuishi na moja ya wazazi wake kadri ya mahakama itakavyoona inafaa. -Kuwa huru kutembelea na kuishi na mzazi wake yeyote ilisipokuwa kama kufanya hivyo kutathiri masomo yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
36

Je mlemavu ana haki ya kupata huduma ya afya?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 26(1) cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya huduma ya afya.

Sheria Kiganjani
Learn More
37

Je mtoto anaweza kuhukumiwa kunyongwa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 26(2) cha sheria ya makosa ya jinai, mtoto hawezi kuhukumiwa kunyongwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
38

Je mlemavu ana haki ya huduma ya elimu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 27 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya huduma ya elimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
39

Je waajiri wanao wajibu wa kuajiri watu wenye ulemavu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 31 (1) cha sheria ya watu wenye ulemavu, waajiri wanao wajibu wa kuajiri watu wenye ulemavu.

Sheria Kiganjani
Learn More
40

Je mlemavu ana haki ya ajira

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 31 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya ajira.

Sheria Kiganjani
Learn More
41

Je waajiri wanapaswa kutokuonesha ubaguzi kwa watu wenye ulemavu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 33 (1) cha sheria ya watu wenye ulemavu waajiri wanao wajibu wa kutobagua watu wenye ulemavu katika maeneo yafuatayo -Matangazo ya kazi -Sifa za kuajiri -Katika viwango vya mishahara -Katika mafao ya kazi -Katika utoaji wa vifaa vya kazi

Sheria Kiganjani
Learn More
42

Je mlemavu ana haki gani awapo eneo la kazi?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 34 (1) cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya mazingira wezeshi ili kumudu kufanya kazi awapo eneo la kazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
43

Je ni mtu gani anaweza kuomba mahakama kutoa amri ya mtoto kulelewa na mtu Fulani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 34(1) cha sheria ya Mtoto, wafuatao wanaweza kuleta ombi la mahakamani la mtoto kulelewa na mtu fulani -Mtoto -Mzazi wa mtoto -Mlezi wa mtoto -Afisa ustawi wa jamii

Sheria Kiganjani
Learn More
44

Je majengo yanayotoa huduma kwa umma yanapaswa kuwa wezeshe kwa walemavu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 35 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya miundombinu wezeshi.

Sheria Kiganjani
Learn More
45

Je mlemavu ana haki ya kupata miundombinu wezeshi ya kupata habari?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 38 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya miundombinu wezeshi ya kupata habari.

Sheria Kiganjani
Learn More
46

Je mlemavu anayo haki ya miundo mbinu wezeshe katika maeneo ya utalii?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 39 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya miundombinu wezeshi katika maeneo ya utalii.

Sheria Kiganjani
Learn More
47

Je mtoto ni nani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 4 (1) ya Sheria ya Mtoto Mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka kumi na nane (18).

Sheria Kiganjani
Learn More
48

Je wazazi wanao wajibu wa kutoa matunzo kwa mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 41 cha sheria ya Mtoto, wazazi wanao wajibu wa kuchangia katika matunzo ya mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
49

Je amri ya ungalizi maalumu inadumu kwa kipindi gani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 47 cha sheria ya mtoto, amri ya uangalizi maalumu wa mtoto unaweza koma endapo -Mtoto akitimiza umri wa miaka kumi na nane -Mtoto akifariki kabla ya kutimiza umri wa miaka 18 -Mtoto akiajiriwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
50

Je malalamiko dhidi ya uvunjaji wa haki za walemavu yanapaswa kutolewa wapi?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 47 ya sheria ya mlemavu, mtu yeyote mwenye taarifa ya uvunjifu wa haki za mlemavu anaweza kutoa taarifa kwa afisa ustawi au kamati maalumu zilizoanzisha na sheria ya watu wenye ulemavu.

Sheria Kiganjani
Learn More
51

Je walemavu wana haki ya miundombinu wezeshi ya barabara?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 48 (1) cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya miundombinu wezeshi ya barabara.

Sheria Kiganjani
Learn More
52

Je mlemavu anayo haki ya kushiriki katika siasa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 51 (1) cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya kushiriki katika siasa.

Sheria Kiganjani
Learn More
53

Je mlemavu ana haki ya kushiriki katika michezo?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 52 cha sheria ya watu wenye ulemavu, mlemavu anayo haki ya kushiriki katika michezo.

Sheria Kiganjani
Learn More
54

Je maombi ya kuasili yanapaswa kufanyika katika mahakama gani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 54 cha sheria ya mtoto, maombi ya kuasili yanapaswa kufanywa katika mahakama kuu au mahakama ya hakimu mkazi kwa kuzingatia aina ya mleta maombi.

Sheria Kiganjani
Learn More
55

Je mtoto anaweza kuasiliwa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 54 cha sheria ya mtoto, mtoto anaweza kuasiliwa.

Sheria Kiganjani
Learn More
56

Je jamii inawajibu wa kuwalinda watu mwenye ulemavu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 54 cha sheria ya watu wenye ulemavu, jamii inao wajibu wa kuwalinda watu wenye ulemavu.

Sheria Kiganjani
Learn More
57

Je mtu anaweza kuleta maombi ya kuasili mtoto ambaye ni ndugu yake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 55(2) cha sheria ya mtoto, mtu anaweza kuasili mtoto ambaye ni ndugu yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
58

Je mwanamke aliye kwenye ndoa anayo haki ya kuingia katika mkataba?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 56 cha sheria ya ndoa, mwanamke aliye kwenye ndoa anayo haki ya kuingia katika mkataba.

Sheria Kiganjani
Learn More
59

Je watoa huduma za simu kwa umma wanawajibu wa kuzingatia watu wenye ulemavu wa kusikia?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 56 cha sheria ya watu wenye ulemavu, watoa huduma za simu kwa umma wanao wajibu wa kuzingatia watu wenye ulemavu wa kusikia kwa kuwawekea vifaa maalumu vya kuwasiliana.

Sheria Kiganjani
Learn More
60

Je kuasili mtoto kunahitaji idhini ya wazazi wa mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 57(1) cha sheria ya mtoto, kuasili mtoto kunahitaji idhini ya wazazi au mzazi wa mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
61

Je mtoto ana haki ya kufahamu wazazi wake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 6 (1) ya Sheria Mtoto, Mtoto anayo haki ya kufahamu wazazi wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
62

Je mtoto ana haki ya kupata uraia?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 6 (1) ya Sheria Mtoto, Mtoto anayo haki ya kupata uraia.

Sheria Kiganjani
Learn More
63

Je mtoto ana haki ya kupewa jina?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 6 (1) ya Sheria Mtoto, Mtoto anayo haki ya kupewa jina.

Sheria Kiganjani
Learn More
64

Je mtoto ana haki ya kufahamu ndugu zake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 6 (1) ya Sheria ya Mtoto, Mtoto anayo haki kufahamu ndugu zake.

Sheria Kiganjani
Learn More
65

Je kuasili kunapaswa kuzingatia maslahi ya mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 61(1) (a) cha sheria ya mtoto, kuasili mtoto kunapaswa kuzingatia maslahi ya mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
66

Je ni kosa kubagua mtu mwenye ulemavu ?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 62 (b) cha sheria ya watu wenye ulemavu, ni kosa kubagua mtu mwenye ulemavu.

Sheria Kiganjani
Learn More
67

Je ni kosa kisheria kumficha mtu mwenye mlemavu na kumzuia kupata haki ya elimu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 62 (c) cha sheria ya watu wenye ulemavu, ni kosa kumficha mtu mwenye ili asipate haki ya elimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
68

Je ni kosa kumzuia mtu mwenye mlemavu kuingia katika maeneo ya utalii wa asili?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 62 (e) cha sheria ya watu wenye ulemavu, ni kosa kumzuia mtu mwenye mlemavu kuingia katika maeneo ya utalii wa asili.

Sheria Kiganjani
Learn More
69

Je sheria ya watu wenye ulemavu inatoa adhabu gani kwa mtu atakaye vunja matakwa ya sheria ya watu wenye ulemavu.

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 62 (I) (i) na (ii) cha sheria ya watu wenye ulemavu, adhabu zitolewazo kwa mtu/taasisi itakayo vunja matakwa ya sheria ya watu wenye ulemavu ni kama ifuatavyo, -Kwa taasisi ni faini isiyopungua milioni mbili na isiyozidi milioni ishirini -Kwa mtu binafsi faini isiyopungua laki tano na isiyozidi milioni saba au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

Sheria Kiganjani
Learn More
70

Je mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kurithi mali za wazazi wake waliomuasili?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 65(1) cha sheria ya mtoto, mtoto aliyeasiliwa ana haki ya kurithi mali za wazazi wake waliomuasili.

Sheria Kiganjani
Learn More
71

Je mwanamke anayo haki ya kuingia makubaliana ya kutengana na mume wake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 67 cha sheria ya ndoa, mwanamke anayo haki ya kuingia makubaliano na kutengana na mumewe.

Sheria Kiganjani
Learn More
72

Je mjane ana haki gani kisheria?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 68 cha sheria ya ndoa, mjane anazo haki zifuatazo, -Kuishi mahali popote apendapo -Kutokuolewa tena au kuolewa na mwanaume yoyote ampendaye bila kuathiri matakwa ya sheria ya ndoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
73

Je mwanamke anayo haki ya kudai fidia kwa kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 69 cha sheria ya ndoa, mwanamke anaweza fungua kesi ya fidia dhidi ya mwanaume aliyevunja ahadi ya ndoa dhidi yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
74

Je mtoto ana haki ya kulelewa na wazazi wake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 7 (1) na 7 (2) ya Sheria ya Mtoto, Mtoto anayo haki ya kulelewa na wazazi wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
75

Je amri ya mahakama ya kuruhusu mtoto kuasiliwa inapaswa kusajiliwa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 70 (1) cha sheria ya mtoto, amri ya Mahakama ya kuruhusu mtoto kuasiliwa inapaswa kusajiliwa

Sheria Kiganjani
Learn More
76

Je mwanamke anaweza kufungua shauri la madai ya fidia dhidi ya mwanamke aliyeshikwa ugoni na mume wake?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 72 cha sheria ya ndoa, mwanamke anayo haki ya kufungua shauri la madai dhidi ya mwanamke aliyeshikwa ugoni na mume wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
77

Je mtoto analiyeasiliwa anaweza kupelekwa nje ya nchi na mtu aliyemwasili?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 73(1) cha sheria ya mtoto, mtoto aliyeasiliwa anaweza kupelekwa nje ya nchi kwa idhini maalumu.

Sheria Kiganjani
Learn More
78

Je mtu asiye raia wa Tanzania anauwezo wa kuasili mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 74(1) cha sheria ya mtoto, mtu asiye raia anaweza kuasili mtoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
79

Je mtoto ana haki ya kufanya kazi?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 77 (1) cha sheria ya mtoto, mtoto anayo haki ya kufanya kazi nyepesi.

Sheria Kiganjani
Learn More
80

Je mtoto anayo haki ya kufanya aina gani ya kazi akiwa na umri gani?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 77(2) cha sheria ya mtoto, mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne (14) ndiye mwenye haki ya kufanya kazi nyepesi.

Sheria Kiganjani
Learn More
81

Je mtoto ana haki ya huduma ya afya?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 8 (1) (d) cha sheria ya mtoto, mtoto anayo haki ya kupata haki ya huduma ya afya.

Sheria Kiganjani
Learn More
82

Je mtoto ana haki ya elimu?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 8 (1) na 8 (2) ya Sheria ya Mtoto, Mtoto anayo haki ya kupata elimu.

Sheria Kiganjani
Learn More
83

Je wazazi/ walezi wana wajibu gani kwa mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 8 (1) ya sheria ya mtoto, wazazi/ walezi wanawajibu ufuatao kwa mtoto wa kumhakikishia haki zifuataza, chakula malazi mavazi Huduma ya afya Elimu Uhuru Kucheza na kupumzika

Sheria Kiganjani
Learn More
84

Je nini maana ya ndoa?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 9 (1) cha sheria ya ndoa, ndoa ni muunganiko baina ya jinsia mbili tofauti ( mwanaume na mwanamke) ambao wamekusudia kuishi pamoja katika kipindi chote cha maisha yao.

Sheria Kiganjani
Learn More
85

Je mtu yeyote anaweza toa taarifa ya uvunjifu wa haki ya mtoto?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 95 (1) cha sheria ya mtoto, mtu yeyote aliye na taarifa ya uvunjifu wa haki ya mtoto anapaswa kutoa taarifa ya uvunjifu huo kwa serikali ya mtaa.

Sheria Kiganjani
Learn More
86

Je mtoto anapaswa kushitakiwa katika mahakama ipi?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 97 (1) cha sheria ya mtoto, mtoto anaweza shitakiwa katika mahakama maalumu ya watoto.

Sheria Kiganjani
Learn More
87

Je wanawake wanayo haki ya kuomba na kutoa taraka?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba 99 cha sheria ya ndoa, wanawake wanayo haki ya kuomba na kutoa taraka kwa mwenzi wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
88

Je mahakama itazingatia vigezo gani katika kutoa amri ya matunzo ya mwanamke?

+

Kwa mujibu wa kifungu namba cha sheria ya ndoa, mahakama itazingatia vigezo vifuatavyo katika kutoa amri ya matunzo kwa mwanamke, -Mila na desturi za jamii husika -Kiwango cha majukumu amabayo mahakama imeweka kwa kila upande

Sheria Kiganjani
Learn More
89

Je mtoto ana haki gani awapo kizuizini?

+

Kwa mujibu wa sheria ya mtoto, mtoto ana haki ya kuwasiliana na wazazi wake, ndugu au mwanasheria wake.

Sheria Kiganjani
Learn More
90

Je mlemavu ana haki ya ndoa?

+

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania, mlemavu kama walivyo watu wengine anayo haki ya ndoa.

Sheria Kiganjani
Learn More
91

Je mabaraza ya ardhi yanazingatia ushiriki wa wanawake?

+

Mabaraza ya ardhi kama yalivyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Ardhi yanatoa fursa sawa na hivyo kuruhusu ushiriki wa wanawake katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
92

Je wanamke aliyefanyiwa ukatili anapaswa kutoa taarifa wapi?

+

Mwanamke aliyefanyiwa ukatili anapaswa kutoa taarifa kwenye ofisi ya ustawi wa jamii au kituo cha polisi kilicho jirani naye.

Sheria Kiganjani
Learn More
93

Je sheria ya Adhabu ya makosa ya jinai inalinda haki za wanawake?

+

Sheria ya Adhabu ya makosa ya jinai namba 16 inalinda haki za wanawake kwa kuweka adhabu kali kwa makosa ya kujamiana kama ukeketaji, ubakaji na udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike.

Sheria Kiganjani
Learn More
94

Je sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inalinda haki za wanawake?

+

Sheria ya Ardhi ya Tanzania inatoa haki sawa kwa wanawake katika kupata, kumiliki, kutumia, kuuza na kugawa ardhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
95

Je sheria ya elimu inalinda haki za watoto wa kike?

+

Sheria ya elimu inatoa fursa kwa watoto wa kike kupatiwa elimu kama ilivyo kwa watoto wa kiume.

Sheria Kiganjani
Learn More
96

Je sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 inalinda haki za wanawake?

+

Sheria ya kazi na mahusiano kazini ya Tanzania inatoa fursa kwa wanawake kuwa na fursa ya kufanya kazi na kulipwa ujira onaostahili. Mfano, sheria hiyo inatoa haki ya wanawake kufaidi mafao ya uzazi.

Sheria Kiganjani
Learn More
97

Je sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inalinda haki za wanawake?

+

Sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 inatoa haki kwa wanawake walio katika ndoa kama haki ya taraka n.k

Sheria Kiganjani
Learn More
98

Je sheria za mirathi zinatoa haki kwa wanawake.

+

Sheria za mirathi nchini Tanzania, zinatoa fursa kwa wanawake kupata mirathi sawa na jinsia ya kiume.

Sheria Kiganjani
Learn More
99

Je kuna sheria ya wanawake ya Tanzania?

+

Tanzania haina sheria moja inayozungumzia haki na wajibu kwa wanawake.

Sheria Kiganjani
Learn More
100

Je kuna sera ya wanawake nchini Tanzania?

+

Tanzania inayo sera ya Taifa ya Maendeleo ya Wanawake na jinsia ya mwaka 2000.

Sheria Kiganjani
Learn More
101

Je kuna sheria ya mtoto ya Tanzania?

+

Tanzania inayo sheria ya mtoto iliyotungwa na Bunge na kutiwa saini na raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mwaka 2009, sheria hiyo inatambuliwa kama Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand