Legal Questions

Questions & Answers

Find answers to common legal questions and learn more about your rights

1

Je, kuna aina ngapi na zipi za ardhi?

+

Aina Tatu, ambazo ni Ardhi ya Kijiji, Ardhi ya Hifadhi na Ardhi ya Jumla.

Sheria Kiganjani
Learn More
2

Je, Ardhi ni nini?

+

Ardhi ni sehemu yote iliyo juu na chini ya uso wa nchi, vitu vyote vyenye kuota kiasili juu ya nchi, majengo na miundo mingineyo iliyokaziwa kwa kudumu juu ya ardhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
3

Je, ni nini maana ya Ardhi ya Hifadhi?

+

Ardhi ya Hifadhi ni ardhi maalumu iliyotengwa au kuhifadhiwa kwa matumizi maalumu ya kitaifa au kijamii kwa manufaa ya raia au wanajamii wote, kwa mfano; hifadhi ya misitu, hifadhi ya vyanzo vya maji, hifadhi ya barabara, nk

Sheria Kiganjani
Learn More
4

Je, ni nini maana ya Ardhi ya jumla?

+

Ardhi ya jumla ni ardhi yote iliyobaki baada ya kutoa ardhi ya vijiji na ardhi ya hifadhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
5

Je, ni nini maana ya Ardhi ya kijiji?

+

Ardhi ya kijiji ni ardhi iliyopo katika maeneo na mipaka ya vijiji. Kutokana na taratibu za tawala za wilaya na hati ya usajiri ya kijiji.

Sheria Kiganjani
Learn More
6

Je, ni namna gani mtu anaweza kujipatia ardhi kwa minajili ya kukodi/kupanga?

+

Ardhi yaweza kupangishwa ama kukodishwa kwa kipindi maalum, ilimradi muda ambao mpangaji atapewa uwe pungufu ya muda ambao mwenye ardhi ana haki ya kutumia ardhi husika. Kwa mfano, kama mwenye ardhi ana hati ya miaka 99 mkataba wa kupangisha ama kukodisha ardhi hiyo utapaswa kuwa wa kipindi ambacho ni pungufu ya miaka hiyo

Sheria Kiganjani
Learn More
7

Je, hakimiliki ya kimila ina hadhi sawa na hakimiliki ya kupewa?

+

Hakimiliki zote za ardhi zina hadhi sawa mbele ya sheria

Sheria Kiganjani
Learn More
8

Je, ili kijiji kiweze kutoa hati miliki kinatakiwa kufuata taratibu gani?

+

Halmashauri ya kijiji inapaswa kwanza kuwa na cheti cha ardhi ya kijiji ambacho, pamoja na mambo mengine kitaonyesha mipaka na ukubwa wa ardhi ya kijiji husika. Baada ya hapo kijiji, kikishajiwekea mpango wa matumizi bora ya ardhi na kutenga maeneo mbalimbali kwa shughuli tofauti, kinaweza kugawa hati miliki kulingana na matumizi yaliyopangwa kwa kila eneo

Sheria Kiganjani
Learn More
9

Je, lengo kubwa la hatimiliki ya kimila ni kuchukulia mikopo tu?

+

Hapana. Faida zingine za kuwa na hatimiliki ni pamoja na kuhakikisha kwamba haki zote zilizopo katika ardhi husika na umilikaji wa ardhi zinatambilika na kulindwa kisheria. Pia, husaidia kudhibiti uvamizi holela

Sheria Kiganjani
Learn More
10

Je, madini ni sehemu ya ardhi?

+

Hapana. Petroli na aina zote za madini zinazopatikana chini ardhi siyo sehemu ya ardhi

Sheria Kiganjani
Learn More
11

Je, ni nini maana ya Hati Miliki ya Ardhi?

+

Hatimiliki ni cheti maalum kinacho tolewa kwa mujibu wa sheria ya ardhi kwa mmiliki wa ardhi. Hati miliki hutolewa kulingana na matumizi ya ardhi husika yaliyoainishwa

Sheria Kiganjani
Learn More
12

Je, ni kwa namna gani mtu anaweza kujipatia ardhi kwa kutwaa?

+

Kujitwalia ardhi hufanyika pale ambapo mtu anaingia katika eneo lisiloendelezwa, kama vile pori na kusafisha kisha kuliweka katika matumizi.

Sheria Kiganjani
Learn More
13

Je, kuna aina ngapi za Hati Miliki?

+

Kuna aina kuu mbili za Hati Miliki. Hizi hujumuisha Hati Miliki ya kimila ambayo hutolewa kwa mtu ambaye tayari anamiliki ardhi kwa njia ya kurithi bila maandishi yoyote, na hati miliki inayotolewa na kamishina baada ya kuombwa, hususan katika maeneo ya mijini. Lakini pia mtu anaweza kupata hati miliki kwa matumizi ya uwekezaji, kama vile mashamba makubwa, viwanda, nk

Sheria Kiganjani
Learn More
14

Je, kuna aina ngapi za umilikaji ardhi?

+

Kuna aina kuu mbili za umilikaji wa ardhi nchini Tanzania. Nazo ni umilikaji ardhi kimila na umilikaji ardhi kwa hati.

Sheria Kiganjani
Learn More
15

Je, ardhi ya Tanzania inamilikiwa na nani?

+

Kwa ujumla ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Watanzania wote na Raisi ndiye msimamizi na mdhamini mkuu wa ardhi kwa niaba ya wananchi wote.

Sheria Kiganjani
Learn More
16

Je, kuna Umuhimu gani wa kupata Hati Miliki?

+

Kwanza, Hati Miliki ni kielelezo au utambulisho wa uhakika wa umiliki wa Ardhi na maendelezo yake. Pili, hati yaweza kutumika kama dhamana ya mkopo. Tatu, hati inaweza kumsaidia mmiliki wa ardhi katika mchakato wa kubadilisha umiliki wa ardhi yake.

Sheria Kiganjani
Learn More
17

Je, Makamu wa Kamishna na Makamishna Wasaidizi wana kazi gani?

+

Makamishna wasaidizi ndio maafisa ardhi waliopo katika halmashauri za wilaya, halmashauri miji, manispaa na majiji. Na hufanya kazi ya usimamizi wa ardhi kwa niaba ya Kamishna wa Adhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
18

Je, ni taratibu gani za kupata Hati Miliki ya Ardhi ya mijini?

+

Maombi yanafanyika kwa kujaza fomu maalum ambayo hupatikana katika ofisi ya ardhi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Halmashauri) ya eneo husika

Sheria Kiganjani
Learn More
19

Je, ni jinsi gani mtu anaweza kupata Ardhi Tanzania?

+

Mtu anaweza kumiliki ardhi kwa ama Kugawiwa na serikali, Kurithishwa, Kupewa, Kutwaa au Kununua.

Sheria Kiganjani
Learn More
20

Je, ni nani anaweza kumiliki ardhi?

+

Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania anaweza kumiliki ardhi mahali popote Tanzania Bara. Kwa Tanzania Zanzibar, haki hii imetengwa kwa ajili ya wazanazibari pekee. Lakini pia, Kikundi cha watu ambao ni raia wa Tanzania walio katika umoja unaotambulika au ni wabia au washirika, wanaweza kumiliki ardhi.

Sheria Kiganjani
Learn More
21

Je, ni vitu gani vya kuzingatioa kisheria kabla haujajipatia ardhi kwa kutwaa?

+

Muda; mtu aliyejetwalia eneo, akiendelea kulitumia kwa muda usiopungua miaka kumi na miwili (12) kama vile yuko kwenye ardhi yake na kuweza kufanya kila atakavyo bila kukumbushwa, kukemewa, kulipishwa kodi au bila ya bughudha ya aina yeyote ya umiliki, kama eneo hilo si ardhi ya hifadhi huhesabiwa kuwa anamiliki ardhi ile kihalali.

Sheria Kiganjani
Learn More
22

Je, mwanamke anaweza kujipatia ardhi kwa njia ya kurithi?

+

Mwanamke anaweza kupata ardhi kwa njia ya urithi kama ilivyo kwa mwanaume. Hii inajumuisha kurithi ardhi kutoka kwa mume wake au wazazi wake na kupitia wosia au mgawanyo bila wosia.

Sheria Kiganjani
Learn More
23

Je, hatimiliki ya kimila inaweza kutumika kuwekea dhamana mahakamani?

+

Ndiyo, Hati za kimila zinaweza kutumika kama dhamana mahakamani, sawasawa na hatimiiliki ya kupewa (granted certificate of occupancy)

Sheria Kiganjani
Learn More
24

Je, kampuni na taasisi zinaweza kumiliki ardhi kama ilivyo kwa mtu binafsi?

+

Ndiyo, kwa sababu kisheria kampuni hutambulika kama mtu, ambapo ina uwezo wa kisheria wa kumiliki mali kwa jina lake yenyewe.

Sheria Kiganjani
Learn More
25

Je, kuna tofauti kati ya HAKIMILIKI na HATIMILIKI ya ardhi?

+

Ndiyo. Hakimiliki ya ardhi ni ile hali ya kuweza kumiliki na kutumia ardhi, haki ambayo inatajwa katika sheria husika. Hatimiliki ni cheti cha umilikaji wa ardhi ambacho mtu hukipata baada ya kukamilisha masharti ya umilikaji kama yalivyowekwa na sheria.

Sheria Kiganjani
Learn More
26

Je, ardhi ya Tanzania inaweza kubadilishwa kutoka aina moja ya ardhi kwenda aina nyingine (Uhawilishaji)?

+

Ndiyo. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania anaweza kubadilisha ardhi kutoka aina moja kwenda aina nyingine

Sheria Kiganjani
Learn More
27

Je, umiliki ardhi kimila bila cheti cha hakimiliki (hatimiliki) ya kimila una nguvu?

+

Ndiyo. Sheria za kimila na desturi za eneo husika zinaupa hadhi sawa na ule umiliki wa kutumia hati ya kupewa

Sheria Kiganjani
Learn More
28

Je, ni kwa namna gani mtu anaweza kupata ardhi kwa kugawiwa na serikali?

+

Ni kwa njiia ya kuomba katika ardhi ya jumla au ya kijiji. Katika ardhi ya jumla kamishina akiishajiridhisha na uhalali wa maombi anakugawia ardhi hiyo. Katika ardhi ya kijiji, serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kugawa ardhi kwa ridhaa ya mkutano mkuu wa kijiji

Sheria Kiganjani
Learn More
29

Je, Kamishna wa Ardhi ana kazi gani?

+

Ni mtendaji na afisa mtalaamu mkuu anayetoa ushauri kwa serikali katika masuala yote yanayohusiana na utawala, usimamizi, umiliki na utumiaji wa ardhi katika masuala endelevu.

Sheria Kiganjani
Learn More
30

Je, ni taratibu gani zinapaswa kufuatwa wakati eneo linapotangazwa kuwa la upimaji ama mipango miji?

+

Pale ambapo eneo limetangazwa kuwa la upimaji/mipango miji/lililopangwa (planned area) mtu yeyote anaye miliki au aliyekuwa akimiliki eneo hilo atapewa notisi ya kuhama. Hata hivyo, mtu huyo atastahili kupata fidia ya haki, ya haraka na timilifu kabla ya kuhamishwa

Sheria Kiganjani
Learn More
31

Je, ni namna gani mtu anaweza kujipatia ardhi kwa kununua?

+

Uuzaji wa umilikaji wa matumizi ya ardhi unaweza kufanyika baina ya mtu mmoja na mwingine kwa kuzingatia utaratibu maalum uliowekwa

Sheria Kiganjani
Learn More
32

Je, ni ipi nafasi ya Waziri wa Ardhi katika maswala yanayohusu ardhi?

+

Waziri wa Ardhi ndiye msimamizi mkuu wa kisiasa nchini katika utengenezaji na usimamizi wa Sera ya Ardhi ya Taifa ambayo inatoa mwongozo wa kisera katika matumizi ya ardhi nchini Tanzania.

Sheria Kiganjani
Learn More

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: info@sheriakiganjani.co.tz

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand