Kwa mujibu wa ibara ya 5 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mlemavu anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Pia kwa mujibu wa kifungu namba 51 (2) cha sheria ya watu wenye ulemavu , mlemavu anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi.