MHOLA LEGAL AID CALL CENTER (0800 712350)

Ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) ambalo linashirikiana na serikali au taasisi zisizo za kiserikali katika kujenga uwezo kwa wanawake na watoto, kwa kutoa elimu na uhamasishaji juu ya haki zao, huduma za kisheria na afya.

Mnamo mwaka 2019 Sheria Kiganjani ilishirikiana na MHOLA kwenye mradi wa kurahisisha mawasiliano baina ya Mhola na wananchi au wanufaikaji wa huduma zote zinazotolewa na taasisi hiyo, hususani shughuli za msaada wa kisheria zinazotolewa na taasisi hiyo katika mkoa wa Kagera.

Ambapo Sheria Kiganjani kupitia wataalamu wake tulifanikiwa kufunga kikamilifu mitambo ya simu (Call Centre) katika wilaya nne ambazo ni Bukoba, Muleba, Karagwe na Ng’ara.

Mfumo huu umeweza kuwarahisishia sana wananchi wa Kagera kuwasiliana na wasaidizi wa kisheria kupitia namba za simu zilizowekwa katika kata husika, na hivyo kuweza kuifikia taasisi ya MHOLA na kupata msaada kwa urahisi tofauti na kipindi cha nyuma ambapo iliwalazimu wanufaikaji wa Miradi ya Mhola kutembea umbali mrefu au kutumia gharama kubwa ili kufika kwenye vituo husika wilayani.

Vilevile mfumo huu una uwezo wa kurekodi maongezi ya simu, kwa lengo la kukagua ubora wa wahudumu pindi wanatoa msaada kwa wateja, lakini pia unatunza kumbukumbu zote kimaandishi kwa wilaya zote tajwa.

Timu Yetu