Wosia wa maandishi ni lazima uzingatie yafuatayo;
Uandikwe kwa kalamu ya wino usiofutika kwa rahisi.
Anayetoa wosia lazima awe na akili timamu.
Wosia utaje tarehe ulipoandikwa.
Wosia utaje kuwa anayetoa wosia anafanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.
Wosia ushuhudiwe na mashahidi wawili wanaojua kusoma na kuandika. Shahidi mmoja awe wa ukoo na mwingine awe mtu baki kama muusia anajua kusoma na kuandika.
Wosia hushuhudiwa na mashahidi wasiopungua wanne, mashahidi wawili wawe wa ukoo na wawili wawe watu baki kama muusia hajui kusoma na kuandika.
Wanaotarajia kurithi hawaruhusiwi kushuhudia wosia huo.
Wosia utiwe na saini ya muusia mbele ya mashahidi wake au kama hajui kusoma na kuandika aweke alama ya dole gumba la kulia.
Wosia utiwe saini na mashahidi.