i. Lazima kuwepo na sheria inayoainisha kwa uwazi kwamba matendo flani yanapofanywa na watu kuwa ni jinai.
ii. Sheria hiyo lazima pia ianishe adhabu kwa matendo hayo ambayo ni makosa ya jinai.
iii. Wajibu wa kuthibitisha shitaka dhidi ya mshitakiwa ni wa yule anyelalamika, na kwa Tanzania ni Jamhuri, hivyo upande wa mashitaka unapaswa kuthibitisha shitaka lake dhidi ya mshitakiwa pasipo kuacha shaka.
iv. Mtuhumiwa atachukuliwa kuwa hana hatia mpaka itakapodhibitika hivyo.
v. Mtu yoyote hatapelekwa gerezani pasipo kufikishwa kwanza Mahakamani.