i. Kuwepona hati ya upekuzi.
ii. Kufanyika kwa upekuzi bila hati ya upekuzipale ambapo sheria inatoa mwanya kutokana namazingira. Kwa mfano, mtuhumiwa kuaminikakuwa ana silaha au kitu chochote kinachohatarishausalama na amani kwa umma.
iii. Kufanyika kwa upekuzi nyakati za mchana yaanikati ya jua kucha na kupwa (kati ya mawio namachweo). Hata hivyo upekuzi unaweza kufanyikamuda mwingine wowote kama mahakama imetoaidhini ya kufanya hivyo.
iv. Kufanyika kwa upekuzi mbele ya mashahidi ambaowanaweza kuwa: kiongozi wa mtaa au shina au mtumzima yeyote mwenye akili timamu.
v. Kama itatokea kuna vitu au mali imechukuliwakwa ajili ya ushahidi, basi ni lazima iandikishwe namhusika au mwenye mali kutia sahihi kuthibitishakutwaliwa kwa mali hizo.
vi. Kutunzwa katika sehemu salama vitu au malizilizochukuliwa kabla ya kurejeshwa kwa mmilikihalali.