i. Kupata utambulisho kutoka kwa askari polisianayefanya mahojiano. Hii ni pamoja na kuelezeajina, cheo chake na sababu za kutiwa nguvuni.
ii. Kuelezwa kwa lugha fasaha inayoeleweka kwamtuhumiwa.
iii. Kupata tahadhari kutoka kwa askari polisi anayehojikwamba hawajibiki kujibu maswali yote isipokuwayale yanayohusu maelezo binafsi (wasifu wake) najina lake. Hivyo mtuhumiwa ana haki ya kutojibu.
iv. Kuwasiliana na mwanasheria wake au ndugu zakeakiwa mikononi mwa polisi, isipokuwa kama kunasababu ya msingi ya kuzuiliwa asiwasiliane na haowahusika.
v. Kuthaminiwa utu wake pamoja na haki zake zabinadamu.
vi. Kupatiwa matibabu anapokuwa yu mgonjwa auamejeruhiwa katika hatua za ukamataji.