Kwa mujibu wa kifungu cha 100 mahakama haiwezi kusikiliza shauri la talaka kama ndoa haijadumu kwa miaka miwili. Ili shauri la talaka lipokelewe kabla ya miaka miwili ya ndoa kupita ni lazima mahakama itoe idhini. Idhini hiyo hutolewa pale tu ambapo mwanandoa mmoja anapata mateso yasiyo kuwa ya kawaida.