Usimamizi wa mirathi hufanywa kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu. Matumizi mabaya ya dhamana ya usimamizi wa mirathi ni kosa la jinai na mhusika anaweza kushitakiwa mahakamani kwa makosa ya madai au jinai. Msimamizi anaweza pia kunyang'anywa hadhi hiyo iwapo mahakama itaridhishwa kwamba amekiuka maadili ya majukumu yake.