-Baada ya pingamizi kuwasilishwa mahakamani, maombi ya mirathi huchukua mfumo wa shauri la kawaida la dau na mwombaji wa mirathi hupewa muda wa kujibu malalamiko ya mweka pingamizi. -Mahakama husikiliza pingamizi hilo na inaporidhika na sababu zilizotolewa katika pingamizi inaweza kubatilisha uthibitishwaji wa mtekeleza mirathi au kukataa uteuzi wa mwombaji wa usimamizi wa mirathi.