- Baada ya pingamizi kuwekwa dhidi ya maombi ya usimamizi wa mirathi, muombaji anapaswa kuiomba mahakama imuite aliyeweka pingamizi hilo ili aiambie mahakama kama anakubaliana na maombi ya usimamizi wa mirathi au hakubaliani nayo na atoe sababu za kutokukubaliana na maombi hayo. -Maombi ya usimamizi wa mirathi hubadilika na kuchukua mfumo wa shauri la dau. Aliyeweka pingamizi hugeuka kuwa mdai na muombaji wa usimamizi wa mirathi hugeuka kuwa mshtakiwa. -Muweka pingamizi anaposhindwa kufika mahakamani au anapokubaliana na maombi ya usimamizi wa mirathi pingamizi lake litahesabika kama limefutwa na mahakama itaendelea na shauri la maombi ya usimamizi wa mirathi na muweka pingamizi hataruhusiwa kuleta pingamizi tena.