Kusajili ndoa kuna faida zifuatazo; a) Usajili wa ndoa na cheti cha ndoa unarahisisha taratibu na mashauri yanayohusu mirathi kwa kujua aina ya ndoa na yupi ni mke/mme halali,hivyo kusaidia kulinda haki ya mjane au mgane. b) Umiliki wa mali: kusajili ndoa yako kunasaidia katika kutambulisha wanandoa halali na pia inasaidia katika kujua nani ana haki ya kumiliki mali za ndoa c) Ushahidi: Usajili pia unasaidia katika kuweka ushahidi kwamba wahusika ni wanandoa. Katika mashauri ya talaka cheti kitahitajika mahakamani katika kuthibitisha hadhi ya wadaawa.