Baada ya kusitisha ajira, mwajiri anapaswa kumlipa mfanyakazi malipo yafuatayo; a) Malipo kwa kazi yote aliyoifanya kabla ya kuachishwa kazi, na ambayo haijalipiwa. b) Likizo yoyote ambayo ni stahili ya mwajiriwa, ambayo haijachukuliwa. c) Mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi, kama mwajiri attamua kusitisha mkataba mara moja. d) Nauli ya mfanyakazi, wategemezi na mizigo yake kwenda mahali ambako alikuwa anaishi kabla ya kuajiriwa kwa mujibu wa kumbukumbu alizoandikisha wakati wa kuajiriwa e) Malipo mengine stahiki kwa mujibu wa sheria, kama vile malipo ya hifadhi ya jamii, kiinua mgongo, nk kulingana na makubaliano ya mkataba.