Kuna aina tatu za ufungishaji ndoa, ambazo ni: a) Ufungishaji Ndoa Kidini: Ndoa zinazofungishwa kidini hufuata taratibu za dini au madhehebu husika ambayo wanandoa ni waumini wa dini hiyo au madhehebu hayo. b) Ufungishaji Ndoa Kiserikali: Sheria ya ndoa pia inaruhusu wanandoa kufunga ndoa kwa kufuata taratibu za kiserikali. Mara nyingi ndoa za kiserikali zinakuwa zikifungwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya na zimekuwa zikifahamika maarufu kama ndoa za bomani. c) Ufungishaji Ndoa Kimila :Hizi ni ndoa zinazofungwa kwa kufuata taratibu za kabila husika ambalo wanandoa wanatoka