a) Wote wana haki ya kumiliki mali kama nyumba, shamba n.k. kwa majina yao binafsi b) Wote wana haki ya kutoa idhini katika uuzaji au kwa pamoja kuweka dhamana mali yoyote ya familia c) Wote wana haki ya kuendelea kuishi katika nyumba ya familia iwapo mume/mke amemtelekeza mwenzake d) Mke ana haki ya kuendelea kupewa matunzo yake na ya watoto wakati wa ndoa hata inapotokea kwamba mume amemtelekeza au wameachana kwa amri ya mahakama. Na mume ana haki ya kupewa matunzo amepata ugonjwa ama ulemavu unaomfanya asiweze tena kujiingizia kipato e) Wote wana haki ya kutokupigwa na/au kufanyiwa ukatili wa aina yoyote f) Wote wana haki ya kupeana unyumba g) Wote wana haki ya kutumia mali ya ndoa h) Wote wana haki kuomba amri ya talaka.